HALFANI SUDY
BOMU
O652 212391
Ilipoishia Jana..
"Naomba tutafutie nafasi kuonana na mheshimiwa rais, mkuu. Nakuhakikishia hili jambo linaenda kufika mwisho. Tutafutie nafasi ndogo tu ya kuongea na mheshimiwa rais" Adrian aliomba.
"OK ngoja niongee nae rais. Nitakujulisha kama atakubali kuonana na ninyi.." IGP John Rondo alisema.
Simu ikakatwa.
Tusome ya Leo...
Sehemu ya Thelathini na Tatu
Dakika kumi baadae simu ya Adrian Kaanan iliita.
Alikuwa ni IGP John Rondo.
Adrian aliipokea simu.
"Adrian, rais amekubali muende kuonana naye. Amesema muende watu wawili tu" IGP John Rondo alisema.
"Amesema twende tukamuone muda gani?" Adrian aliuliza.
"Sasahivi. Hivi huko Mheshimiwa rais Mgaya anawasubiri ninyi. Mtapitia hapa makao makuu, maana ametaka twende wote" IGP John Rondo alisema.
"Sawa mkuu, tutakuwa hapo sio muda mrefu kuanzia sasa" Adrian alisema kwa furaha.
Simu ikakatwa.
Adrian akawaeleza wenzake kila kitu alichoongea na IGP John Rondo.
Ikaamuliwa, Adrian Kaanan na Daniel Mwaseba wajiandae kwa safari ya ikulu kuonana na mheshimiwa rais.
***
Wakati huo, mzee Msangi alikuwa kitalu C. Mahali ambapo walikuwepo pia wakina Elia Kilasi, Mark the sniper, Lameck na Luca.
Muda mfupi uliopita mzee Msangi alikuwa ametoka Tegeta Nyuki, ambapo kwa macho yake alishuhudia uharibu uliofanywa na kina Daniel Mwaseba.
Hakuamini kabisa kwa jinsi watu hao walivyofanikiwa kumuokoa Hannan.
Mzee Msangi alikasirika sana! Akampa likizo Anna arejee kwao. Na moja kwa moja ndio akaja kitaku C.
Nayeye pia, akiwa na wenzake waliipokea taarifa ya kupotea Chifu, waziri wa fedha na wanafunzi wa St Joseph wakiwa hapo.
Mzee Msangi moja kwa moja aliamini hiyo ni kazi ya Imma Ogbo. Huku akiwa haamini hatua aliyoichukua Imma Ogbo.
Hii ilitia uzito katika harakati zake za kumkamata Dr Luis.
Lakini kitu ambacho Mheshimiwa rais alikuwa hakijui, pamoja na kumpa kazi ya kumsaka Dr Luis mzee Msangi, lakini mzee Msangi naye alikuwa na mpango binafsi wa kumpata Dr Luis. Katika mpango huo alikuwa akishirikiana na Mwenyekiti, Antony Kyando.
Mpango wao ulikuwa ni kutengenezewa kirusi cha ajabu cha DH+.
Kirusi cha DH+ kilikuwa ni kirusi kipya katika dunia ya sayansi. Kirusi hiko kilikuwa kirusi hatari. Na aliyekiumba alikuwa ni Dr Luis.
Antony Kyando alikuwa anakihitaji kwa nguvu zote kukipata kirusi hiko kwa ajili ya kukitumia kwa wapinzani wake. Na mtu pekee aliyekuwa anaweza kukitengeneza kirusi hiko cha ajabu hapa duniani, alikuwa ni mwanzilishi wake..Dr Luis.
***
Saa tatu na dakika tano usiku, Daniel Mwaseba, Adrian Kaanan wakiongozana na IGP John Rondo waliwasili ikulu huko Magogoni.
Kwakuwa kulikuwa na taarifa wa ujio wao hapakuwa na shida yoyote ile. Baada ya kukaguliwa na kuambiwa waache vitu vyao vyote zikiwemo silaha zao katika cumba cha ukaguzi, moja kwa moja wakapelekwa katika chumba cha mikutano.
Ndani ya chumba cha mahojiano, walisubiri kama dakika tano hivi, ndipo Mheshimiwa rais Mgaya akaingia katika chumba cha mikutano.
Rais Mgaya alikuwa amevaa suti nzuri ya rangi nyeusi na tai nyeupe, chini alivaa viatu vya rangi ya kahawia. Ukiacha uchovu katika sura yake, lakini alikuwa amependeza sana.
"Poleni sana kwa kuwaweka hapa. Nilikuwa namaliza kikao na kamati ya ulinzi na usalama.." Rais alisema huku akilazimisha kutabasamu.
"Haina shida Mheshimiwa rais. Hata hivyo hatujakaa muda mrefu sana" IGP John Rondo alijibu.
"Nashukuru sana IGP John. Nimeitika wito wenu. Nawasikiliza ninyi IGP John kitu gani mlichoniitia hapa. Leo ratiba ilikuwa ngumu sana. Nilikuwa sina nafasi kabisa. Tangu asubuhi imekuwa ni siku ya vikao tu, lakini ulivyonambia kuna watu wana majibu juu ya kutekwa kwa Chifu, Waziri Elisha Salu na wale watoto wadogo wa St Joseph, nikaona nitenge angalau muda huu mdogo kuja kuwasikiliza" Rais Mgaya alisema.
"Ni kweli mheshimiwa rais. Najua ulikuwa hujapata bahati ya kukutana na watu hawa. Huyu hapa ni Daniel Mwaseba. Ni mpelelezi katika idara ya usalama wa taifa. Huyu hapa anaitwa Adrian Kaanan. Ni afisa wangu ninayemuamini sana. Hawa kwa pamoja na wengine ambao hawajapata nafasi ya kuja hapa leo ndio vijana wetu wanaounda kikosi cha B1. Kikosi kilichopewa kazi ya kumsaka rafiki yako Dr Luis.."
Msako dhahri ulionekana katika sura ya rais Mgaya baada IGP John Rondo kusema hivyo. Ni Daniel Mwaseba pekee ndio aliouona mstuko huo.
"... Aaah kumbe ndo kikosi cha B1 hiki. Daniel nimesikia sifa zako mara kadhaa, nafurahi leo kuonana nae kwa uso na macho" Rais Mgaya alisema akijibaraguza.
"Nami nashukuru sana mheshimiwa rais kuonana na wewe. Ni nafasi ya kipekee sana hii. Tulikuwa hatujaonana tangu umeingia madarakani. Nakupongeza sana kwa uongozi wako uliotukuka" Daniel alisema.
"Nashukuru sana Daniel, na huyu umesema anaitwa Adrian?" Rais Mgaya aliuliza akimwangalia IGP John Rondo.
"Ndio. Adrian Kaanan. Kwasasa Adrian ni kiongozi wa askari wetu wa misheni za siri na muhimu kwa nchi" IGP John Rondo alisema.
Rais Mgaya na Adrian Kaanan wakapeana mikono nao.
"Sasa mimi sitokuwa muongeaji mkuu. Kazi yangu ilikuwa ni kuwatambulisha tu. Hawa wenyewe ndio watakwambia lengo la ombi hili la kukutana na wewe" IGP John Rondo alisema.
"Karibuni sana" Mheshimiwa rais Mgaya aliwakaribisha.
"Kama tulivyotambulishwa na na IGP John Rondo. Mimi na Adrian tunaunda kikosi cha B1. Tukiwa pamoja na wenzetu, David Ngocho, Hannan Halfan na Martin Hisia.
Mheshimiwa rais, sisi kama kikosi cha B1 tulipewa kazi ya kumtafuta Dr Luis aliyetekwa katika kikosi cha B1, na mimi nikiwa kiongozi wake.
Kwanza niseme tu ni mimi ndiye niliyepewa na Chifu kazi ya kwenda kumpokea Dr Luis siku ile pale airport. Kwa maana hiyo nasikitika kusema Dr Luis alipotea katika mikono yangu katika hoteli ya Dos Santos.
Dr Luis hakupotea tu, na mimi niliishia kutekwa katika harakati za kumwokoa. Watekaji walinipeleka huko Mkuranga bila kujua kwamba nilitoa taarifa kwa mwenzangu ambaye alifatilia nyendo za watekaji.
Walinifikisha Mkuranga na kunifungia katika chumba kimoja kidogo. Nilijitahidi kujiokoa katika kile chumba. Nilivyotoka nje nilimkuta mwenzangu akiwa kapigwa risasi. Katika harakati za kumwokoa ndipo nilishuhudia nyumba ile ikilipuliwa kwa Bomu na helkopta ya jeshi.
Na hiyo ikawa sababu ya kuundwa kwa kikosi hiki.
Kikosi cha B1 kilifanya kazi yake kwa umakini mkubwa sana. Kabla ya kugundua kwamba kuna mwenzetu anatusaliti. Tulijaribu kumchunguza mwenzetu, tukagundua kwamba alikuwa anapewa maagizo na mtu anayeitwa Elia Kilasi, kwa shinikizo, kwakuwa familia yake ilikuwa imetekwa.
Tuliichunguza namba ya Elia Kilasi. Tukagundua ana mawasiliano na mzee Msangi!"
"Unasemaje wewe! IGP huu ndio upuuzi ulioniitia hapa!" Rais Mgaya alifoka. Ilikuwa kama anasubiri sehemu atakayotajwa mzee Msangi.
"Mheshimiwa rais huu sio upumbavu. Ni kitu cha ukweli na tuna ushahidi nacho!" Daniel alisema kwa hasira.
"IGP John Rondo ondoa hawa vikaragosi hapa. Hawa ni wanafiki, wanataka kuizika kazi aliyoifanya mzee Msangi kwa skendo za kutengeneza!" Rais Mgaya alifoka.
"Mhesh..." Daniel hakumalizia kuita.
"Na kuwnzia sasa kikosi cha B1 kivunjwe. Watafutwe watu wengine wa kuifatilia kesi hii!"
"Mhesh.." Daniel Mwaseba hakumaliza alichotaka kuongea.
"Naomba uwasikilize mheshimiwa rais" IGP John Rondo aliingilia.
Rais Mgaya alikaa kimya.
"Tunaomba umuite mzee Msangi hapa kama hautuamini! Asimame hapa mbele yetu kama atabisha.." Daniel alisema.
Rais Mgaya alikubali kwa kichwa.
"Ndio hiko tu ndicho kilichowaleta hapa?" Rais Mgaya aliuliza.
Daniel alianza kuelezea juu ya uhusika wa Imma Ogbo na rais Abayo katika sakata hili.
Hapo rais Mgaya ndo hakukubali kabisa.
"Kuhusu mzee Msangi mmesema nimpigie simu aje hapa. Je kuhusu Rais Abayo mna ombi gani?" Rais Mgaya aliuliza.
"Tupe kibali cha kuingia ubalozi wa Nigeria hapa nchini. Tuna uhakika tutapata kitu juu alipo Dr Luis" Daniel aliomba.
Rais Mgaya ameonesha kutoyakubali maelezo ya kina Daniek Mwaseba..
Je sasa atayakubali maombi yao?
Riwaya hii inapatikana yote whatsapp, tuma 3000 kwenda 0652 212391 kisha mcheck mwandishi Whatsapp
0652 212391 atakutumia muda huohuo..