HALFANI SUDY
BOMU
0652 212391
ILIPOISHIA..
Katika milango miwili wakatokea walinzi. Idadi yao ilikuwa yapata kumi.
Watano kutoka katika kila mlango. Walibeba wakina Daniel mkuumkuu, na kwenda kuwatupia nje ya geti la ikulu.
Hiyo ni baada ya kauli moja tu ya rais Mgaya.
Wakina Daniel wanafukuzwa ikulu na kuitwa wahuni!!
Hii ni sehemu ya Thelathini na sita
Daniel na Adrian walirejea maskani kwao. Njiani walikuwa kimya. Kila mmoja akitafakati kilichotokea ikulu.
"Kuna siri nzito rais anayo" Daniel aliwaza.
Walifika maskani kwao baada ya dakika hamsini na tano. Waliwakuta watu wote sebuleni wakiwasubiri wao.
Adrian alichukua usukani wa kuwaekeza wenzao kila kitu kilichotokea huko Ikulu. Daniel hakuweza hata kuzungumza, alikuwa amekabwa na donge la hasira.
Hii haikuwa habari njema hata kidogo kwa wote mle ndani.
Rais Mgaya alikuwa amewasaliti..
"Poleni sana ndugu zetu. Kwa mujibu wa maelezo yenu inaonesha kuwq rais Mgaya kuna kitu anaficha. Ingawa tumetolewa kufatilia kesi hii lakini hatupaswi kuacha hadi tujue ni kitu gani mheshimiwa rais anaficha?" Hannan alisema.
"Hannan, tunaweza kuendelea na kesi hii wenyewe. lakini itakuwa ngumu sana kwetu. Hatuna wa kushirikiana naye, kwa ujumla serikali imetutenga na suala hili. Kama tunaendelea na uchunguzi wetu basi kumbukeni tuna kazi kubwa sana ya kufanya. Je mko tayari tupambane wenyewe?" Daniel aliongea kwa mara ya kwanza tangu aingie mle ndani.
"Mimi nipo ndani. Liwe jua iwe mvua. Nitakuwa pamoja na wewe Daniel.." Martin aliwashangaza mle ndani. Alikuwa wa kwanza kukubali kuungana na Daniel Mwaseba.
"Nami nipo ndani ya misheni hii. Nitakuwa nawe bega kwa bega Daniel" Hannan akadakia.
"Nami pia nipo ndani! Nina uchungu na familia yangu. Nitakuunga mkono siku zote Daniel" David aliitikia.
"Sina haja ya kuongea sana. Sisi ni B1 na B1 haiwezi kufa kamwe. Wametuunganisha lakini hawawezi kututenganisha" Adrian naye alisema.
"Safi sana jamaa zangu. Mmenipa nguvu sana. Nimefuraahi sana kuona mnakuwa upande wangu. Taifa linatuhitaji sana, hatuwezi kukatishwa tamaa kwa maneno ya rais Mgaya. Maneno yake yatupe hali ya kupambana zaidi na zaidi!" Daniel alisema.
Daniel akaweka mkono, Hannan akaupandisha juu yake, akafuatia David, Adrian akafatia, kisha juu akamalizia Martin Hisia.
"Kazi nd'o inaanza!" Wakasema kwa pamoja.
Hiyo ilikuwa saa sita usiku.
***
Kulikucha. Siku nyingine tena ikachomoza jijini Dar es salaam.
Siku hii mpya ilikuja na habari iliyowastua sana watanzania. Ikikuwa kama alivyoahidi Imma Ogbo kwa Daniel Mwaseba jana yake.
Mwili wa waziri wa mipango na fedha, Elisha Salu, uliokotwa katikati ya uwanja wa Taifa kule Chang'ombe.
Kilichostua zaidi ni ujumbe uliokutwa pembeni ya maiti hiyo.
"Mtaokota maiti nyingine baada ya nusu saa!!"
Taarifa ya kifo cha waziri wa mipango na fedha ilimkuta rais Mgaya akiwa anasoma magazeti asubuhi.
Ilikuwa ni ada yake kusoma magazeti yote ya siku kila siku asubuhi.
Rais Mgaya aliipokea taarifa hiyo kwa mstuko mkubwa sana!!.
Moja kwa moja akampigia simu kamanda wa polisi wa mkoa wa Dar es salaam, kamanda Karim Gogo, akimtaka yeye na askari wake waashughulikie suala hilo kwa uwezo wao wote. Huku akimsisitiza pia juu ya kuwasaka na kuwaokoa watoto wengine sitini na mbili wa shule ya msingi St Joseph. Kamanda wa Polisi wa mkoa alikubali kwa utii agizo hilo. Bila kujua undani wa tukio hilo. Naye akaagiza askari wake waingie kazini, kuwasaka wahalifu hao.
Taarifa hiyo ya kifo cha waziri wa mipango na fedha iliwakuta wakina Daniel Mwaseba sebuleni, maskani kwao. Walikuwa wametulia wakipanga makakati yao. Taarifa hiyo iliongeza hofu juu ya usalama wa familia ya David, maana wao waliamini familia ya David ipo mikononi mwa watu hao. Mikononi mwa Imma Ogbo!
"Hawa jamaa sasa wameanza kuua watu. Hatujui ni nani atafuata baada ya mheshimiwa Elisha, pengine akawa Chifu au wale watoto wadogo wasio na hatia" Daniel aliwaambia wenzake.
"Mwanzoni hisia zetu wote zilituambia hawa watu wapo katika ubalozi wa Nigeria hapa nchini, lakini tatizo tumeshindwa kuthibitisha hisia zetu kwakuwa tumekosa kibali cha kuingia ubalozini kutoka kwa mheshimiwa rais Mgaya. Rais Mgaya amegoma kabisa sisi kuuchunguza ubalozi huo. Na ni ngumu sana kuvamia pale, maana hivi sasa balozi zote zina ulinzi mkali sana kutokana na lile tishio la kulipuliwa kwa ubalozi wa Uganda.
Lakini mimi nilikuwa nina wazo moja.." Adrian alisema.
"Una wazo gani Adrian?" Hannan aliuliza.
"Mnaonaje tukamteka balozi wa Nigeria!" Adrian alisema.
Ukumbi mzima ulikaa kimya.
Baada ya kama sekunde ishirini Hannan aliipata sauti yake.
"Hatuwezi kuzusha mgogoro wa kidiplomasia kweli?"
"Hapana Hannan, hatuwezi kuzusha mgogoro wa kidiplomasia, bali tutakuwa tunaelekea kuufikisha mwisho mgogoro huu.
Sisi sote hapa tunakubali kwamba serikali ya Nigeria inahusika kwa asilimia zote kwa haya mambo yanayotokea hapa nchini. Sasa kuna namna nyingine zaidi ya kumteka mwakilishi wa serikali hiyo? Aje hapa ili tumfungue, aseme kila kitu anachokijua kuhusu sakata hili. Na kama tukiona hahusiki kwa lolote, basi tunamwachia" Adrian alisema kwa kirefu.
"Umeongea vizuri sana Adrian. Mimi naunga mkono kila neno lako. Lakini tatizo lipo ni kwa jinsi gani tunampata huyo balozi. Kwasasa bila shaka si balozi tu zinazolindwa, hata mabalozi wenyewe wanalindwa pia. Watakuwa wapuuzi kiasi gani eti walinde jengo na kumuacha mtu?" David alisema.
"Sikia niwaambie. Sisi hapa, tukiamua inawezekana kumteka Balozi wa Nigeria. Sisi hapa, tukiamua pia tunaweza kuingia hata katika ubalozi wa Nigeria tena saa saba mchana, hata kama kuna ulinzi kiasi gani" Daniel alisema kwa uhakika.
Watu wote walimwangalia Daniel Mwaseba pale sebuleni.
Je nini kitatokea?
Riwaya hii inapatikana yote whatsapp..
Namba ya malipo ni 0652 212391
Kwa sh 3000 tu.
Sent from my TECNO-Y3+ using
JamiiForums mobile app