Bomu la wanafunzi litaiangusha hii serikali!

Bomu la wanafunzi litaiangusha hii serikali!

Tunakokwenda siyo. Maelfu ya wanafunzi wamekosa mikopo, wako mitaani na bila shaka watalazimika kuandamana kudai haki yao ya msingi, yaani Elimu. Polisi watatumia nguvu nyingi kuwanyamazisha, ila haitawezekana, kwa maana kwamba wananchi nao watawaunga mkono. Na hili swala litakuwa ni tatizo ambalo halitazimika kamwe.

Nadhani serikali iangalie hili swala la mikopo kwa wananfunzi kwa jicho la pili. Hili ni bomu na tishio kubwa sana kwa huu utawala
Ajiara kwa vijana + mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu!!!!!!
 
Me naona elimu imeshakufa kwa sababu ya viongoz kuichanganya na siasa mwanang kusoma bac kwa sasa ni bora achunge ngombe watamseidia baadae kuliko kuwan na maband akaambukia patupu
 
Kusomesha wananchi wake liwe ndio jukumu kuu.Sioni mantiki ya kununua Mashangingi,Ndege,Barabara za hewani huku watoto hawaendi shule.Kama unafikiri kusomesha ni Gharama Jaribu Ujinga.
Watoto gani hawaendi shule, wapo wa ngapi kati ya wangapi ambao hawasomi? Hivi wanafunzi wa veta, vyuo vya ualimu, nursing, vyuo vya utalii wanasoma kwa mkopo upi wa serikali, nenda Kenya au Uganda, Drc tuambie ni wanafunzi kiasi gani wanakopeshwa na serikali ukilinganisha na Tanzania?
 
Yaani kwa hoja hizi ndio mnajiaminisha kuwa serikali itatikisika kwa suala la mikopo? Hizi kelele zote ni njaa ya kushika pesa na wala si kusoma.

Unafahamu mkopo unatolewa chini ya sera ya cost sharing? Kama ni cost sharing basi nikuulize wewe unayelilia mkopo umechangia nini?
Leo ndiyo mnajua habari ya cost sharing, kwenye kampeni mlikuwa mnatokwaa povu la nini kwa kuahidi kutoa mkopo kwa kila mwanafunzi anayestahili. Wote wamedahiliwa na hivyo kustahili sasa mnakwepa kwa kutaka kuwatwika wazazi mzigo. Je, fedha za mkopo ni za nani kama si kodi ya wazazi haohao mnaowasimanga baada ya kupata madaraka?
 
Bongo hapa hapa? Na kataa mkuu, sisi wa Tanzania hatuna jeuri hiyo!!
Ukitaka kujua jeuri ya Watanganyika muulize Mjerumani mkuu. Katika vita ya Maji Maji ilibidi aagize mizinga kutka ujerumani, hii yote ni baada ya ngome zake kuanguka kwa makali ya mishale na mikuki. Utawala wowote hasa ule uliochaguliwa na watu haupaswi kuanza kuwafanyia dharau wananchi wake walioiweka madarakani hasa katika suala la elimu.
 
  • Thanks
Reactions: GUI
Watoto gani hawaendi shule, wapo wa ngapi kati ya wangapi ambao hawasomi? Hivi wanafunzi wa veta, vyuo vya ualimu, nursing, vyuo vya utalii wanasoma kwa mkopo upi wa serikali, nenda Kenya au Uganda, Drc tuambie ni wanafunzi kiasi gani wanakopeshwa na serikali ukilinganisha na Tanzania?
Kwa rasilimali zote tulizonazo hatuwezi kujilinganisha na wagonjwa uliowataja, tena ukomee hapohapo!!!
 
kodi unayolipa sio kwa ajili ya kukopesha,hilo ni jukumu lako na mkeo
Kweli nimeamini kuna watu humu ni wagonjwa wa akili; kwani mke wangu anaingiaje kwenye mjadala huu? Nadhani tujadiliane, tuache familia zetu nje ya mihemuko yetu, tafadhali!!!!
 
Kuna watu wanaropoka pumba tuu humu nchi unazoziona zimeendelea fuatilia Sera zake za elimu, zinawasapot wanafunzi wa elimu ya juu kwa asilimia kubwa, Leo mtu anakuja kusema somesheni watoto, kila mtu angekuwa na uwezo wa kusomesha mwanae elimu ya juu usingeskia kitu kinaitwa mkopo, na pia serikali iliona kuna umuhimu wa kuwasapot wanafunzi ndo maana ikaweka mkopo, na ndo maana wanasema bajeti haitoshi hawatapata wote ingawa walistahili
 
Kweli nimeamini kuna watu humu ni wagonjwa wa akili; kwani mke wangu anaingiaje kwenye mjadala huu? Nadhani tujadiliane, tuache familia zetu nje ya mihemuko yetu, tafadhali!!!!
Bila ya mke wako mngepataje huyo mtoto mnaelazimisha apate mkopo kwa matokeo ya starehe yenu.Mnatakiwa muwapangie watoto wenu utaratibu wa kuwasomesha,sio mnaanzisha vurugu kudai mikopo kama vile ni haki
 
Kukojoa ukojoe wewe,utegemee mwanao asomeshwe kwa mkopo wa serikali,watapata wenye vigezo kwa 100%,wengine kakopeni benki msomeshe wanenu,mmebweteka na kuona kama vile lazima,ile ilikua juhudi ya serikali kuingiza wanafunzi kwa wingi.Sasa kuna UDOM,MUHAS,UCLAS na UDSM vinatosha kabisa kufikia malengo ya serikali
Wakati mwingine kauli nzuri zinaficha ubongo wenye shida!
 
Kama wewe ni maskini, shule ya msingi na sekondari nani alikukopesha?
Hivi kwa akili yako unalinganishaje gharama za kusoma shule ya msingi/sekondari na gharama za chuo!? Hebu acha ushabiki usiokuwa na tija wewe, itendee haki akili yako (kama unayo)
 
Haki ya kusomesha inaanza kwa mzazi,mkopo haujaandikwa popote kwenye katiba,serikali haiwezi kuanguka kwa siasa hizi nyepesi.Somesheni watoto kwa pesa yenu,serikali inawajibu wa kujenga miundombinu ya elimu acheni kujisahau
Kwann shule ya msingi na sec nao wasilipe tu Ada ili tununue bombadia 3
 
Ulitaka usomee chini ya mwembe? Halafu hela ya madarasa ukopeshwe?
There is something called KARMA, if you think you have everything today to the extent of ignoring what people are going through because they dont have enough money then just wait. Whether today or the day after karma will find you then you'll regret all this nonsense you are writing now.
 
Haki ya kusomesha inaanza kwa mzazi,mkopo haujaandikwa popote kwenye katiba,serikali haiwezi kuanguka kwa siasa hizi nyepesi.Somesheni watoto kwa pesa yenu,serikali inawajibu wa kujenga miundombinu ya elimu acheni kujisahau
We jamaa nkikutukana hakika ntapata thawabu
 
Sikuwahi ongelea suala la mikopo huko kote nilikozunguka kuomba kura.alie kuwa anasema kipao mbeke cha kwanza ni Elimu mlimtelekeza sasa msinijaribu nitafukuza wanafunzi wote muende mkalime.
Yaani tuvyuo tumekuwa kma utitiri na vyote vinataka mikopo hela ziko wapi?
 
Haki ya kusomesha inaanza kwa mzazi,mkopo haujaandikwa popote kwenye katiba,serikali haiwezi kuanguka kwa siasa hizi nyepesi.Somesheni watoto kwa pesa yenu,serikali inawajibu wa kujenga miundombinu ya elimu acheni kujisahau
kasome katiba wewe ,acha kutafuta cheo kwa nguvu kuliko akili.Hujui maana ya katiba,hakuna sheria isiyotokana na katiba.
 
kasome katiba wewe ,acha kutafuta cheo kwa nguvu kuliko akili.Hujui maana ya katiba,hakuna sheria isiyotokana na katiba.
tofautisha haki ya kupata elimu na haki ya kupata mkopo wa elimu.nendeni mkakope benki,mlizoea kugawana pesa kama mafungu ya nyanya
 
  • Thanks
Reactions: bdo
tofautisha haki ya kupata elimu na haki ya kupata mkopo wa elimu.nendeni mkakope benki,mlizoea kugawana pesa kama mafungu ya nyanya
na vyeo vimeisha,utaishia kupata ukamanda wa CCM tu.
Akili ndogo.Kwani unaijua sheria iliyoanzisha HESLB?Au ccm akili tumboni?
 
Tunakokwenda siyo. Maelfu ya wanafunzi wamekosa mikopo, wako mitaani na bila shaka watalazimika kuandamana kudai haki yao ya msingi, yaani Elimu. Polisi watatumia nguvu nyingi kuwanyamazisha, ila haitawezekana, kwa maana kwamba wananchi nao watawaunga mkono. Na hili swala litakuwa ni tatizo ambalo halitazimika kamwe.

Nadhani serikali iangalie hili swala la mikopo kwa wananfunzi kwa jicho la pili. Hili ni bomu na tishio kubwa sana kwa huu utawala
Si kwa unafiki wa watanzania, acha kabisa kuwapa hamasa vijana kuandamana maana la kukosa mkopo linatosha wasiongeze na vilema na vifo itakuwa hasara kubwa kwa wazazi wao.

Ukitaka kuhakiki maneno yangu nenda vituo vya daladala uone mwanafunzi tena masikini wa darasa la kwanza akisukumwa na jitu shababi ili lipande kwanza kwenye daladala bila kuhakikisha kwanza anampandisha mtoto huyu mdogo!
Leo ndio useme waliokosa mkopo wataungwa mkono na raia?? Thubutuu!!!
 
Back
Top Bottom