Bomu la IMTU limeshalipuka, bado la UDOM!


Safi sana mkuu kwa kuelewa somo langu!waingereza au wamarekani hawataki kabisa kuruhusu uchakachuaji wa fani ya udaktari au afya kwa ujumla.

Ni haki yao kuiita MUHAS,UDOM,IMTU n.k kama vyuo visivyo na viwango kulingana na viwango walivyojiwekea.sasa nakushangaa sana unapochukia kuona watanzania tukiita IMTU haijakidhi viwango vya kitanzania.
Kuna kipindi ilikuwa ni lazima kupita internship Muhimbili kama hukusomea udaktari hapo Muhimbili!sasa ni bora liende!
 

Ni kweli mimi ni mfuasi wa ligi tajwa,na sababu ya msingi ni moja tu...I believe in quality and not quantity.

Ni heri kuwa na vichwa mia moja kuliko vihiyo millioni moja.
 
Labda hata mzee wako analo analolijua au hata wangu pia lakini kuna vitu wewe unajua zaid yao wote !!!!

Sio ajabu mimi kujua pia zaid yako!!!!!

Mkubwa wako akikueleza sikiliza!
Naijua MUCHS,KCMC,BUGANDO,KAIRUKI,IFAKARA,IMTU,UDOM,MBARARA,MAKERERE,NAIROBI!!

Lakini leo tunaongelea IMTU na UDOM!!

Iko siku tutaiongelea MUHAS VS MUCHS
 

Now i can believe that your brain is being inflammed,...
 
Sarungi profesa,daktari wa mifupa?Vipi ilikuwaje ishu yake kwani?
Alisomea east europe na aliporudi akakutana na sera hizo za kudharauliana lakini at the end the day akawa profesa mzuri kuliko hata hao wa kujisikia (nilisimuliwa na Daktari mmoja marehemu sasa).
 

Nakushangaa kuwaita IMTU hawana viwango wakati na mwenyewe wa Muhimbili huna viwango.Kama IMTU,nawe huna kiwango kwavile hukufundishwa na wataalam competent na wakutosha kwenye hospitali zenye vifaa vya kutosha na vya kisasa.Na ndiyo maana ukiletewa complex case pamoja na uMuhimbili wako,unakuwa huna tofauti na IMTU;Kwa vile wote mtai refer nje kwenye wataalam competent wenye vifaa vya kutosha na vya kisasa.

Kwahiyo hata kwa viwango vya kitanzania,huwezi kumcheka mtu wa IMTU kwavile hata yeye ana uwezo wa kutibu malaria kama wewe tu.Au labda useme wewe daktari wa Muhimbili unaweza kutibu ugonjwa gani ambao daktari wa IMTU hawezi kutibu?
 
Ukielewa maana halisi ya 'kutibu' ndio utaweza kuwatofautisha wa Muhimbili na wa kata!kutibu malaria sio sawa na kuprescribe ant-malarials
 
Ni kweli mimi ni mfuasi wa ligi tajwa,na sababu ya msingi ni moja tu...I believe in quality and not quantity.

Ni heri kuwa na vichwa mia moja kuliko vihiyo millioni moja.
Daktari mwenzangu naona umecharuka!!!
Je unajua ya kuwa kuna nchi zimepunguza mortality si kuzalisha highly qualified doctors lakini kwa ku train village health workers tu?
Je unajua ya kuwa mafanikio yote ya kudhibiti TB na leprosy ni chini ya DTLC na RTLC ambao majority ni mere AMOs?
Je unajua ya kuwa kuna kitu kinaitwa fursa,inaweza ukawa na pass nzuri lakini ukakosa fursa na ikiw afursa hiyo utaipatia Russia au Cuba bado unaweza kuwa daktari bora kuliko hao wa Muhimbili.
Nimefanya kazi na fourth and fifth year medical students kutoka nchi za magharibi lakini sikuona manufaa makubwa zaidi ya kuwa mbele katika ku interpret vitu kama ECG.
Retreat kidogo utafakari msimamo wako.
Jioni njema.
 
Alisomea east europe na aliporudi akakutana na sera hizo za kudharauliana lakini at the end the day akawa profesa mzuri kuliko hata hao wa kujisikia (nilisimuliwa na Daktari mmoja marehemu sasa).

nimekupata mkuu..hawa jamaa wenyewe ni wababaishaji halafu wanadharau wenzao
 
Ukielewa maana halisi ya 'kutibu' ndio utaweza kuwatofautisha wa Muhimbili na wa kata!kutibu malaria sio sawa na kuprescribe ant-malarials

nipe tofauti ya 'kutibu' malaria na magonjwa mengine kati ya muhitimu wa Muhimbili na wa IMTU.Kuna mtu ameandika hapa kuwa ana jamaa zake waliohitimu IMTU wapo muhimbili wanatibu;basi wasingeruhusiwa kutibu hapo kama hawakidhi viwango?

Mbona hatujawahi kusikia zile kesi zilizoshindikana Tanzania na kupelekwa South Africa au India,zinabakizwa Tanzania kwavile tuna madaktari wazuri waliosomea Muhimbili wana uwezo wakuzi manage kesi hizo?
 

Mkuu ni kweli nimechafukwa kwani tunapoelekea ni kubaya !

I appreciate mchango wa wahudumu,manesi,clinicians na bila kusahau wahisani wa marekani et al katika sekta ya afya.

I personally have trained AMOs,COs Nurses and the like on TB,HIV,IMCI and the like,but the inflammatory fact is, they can never be an alternative to the real healthcare professionals.

Hapo tulikuwa tunazima moto tu kama mwalimu alipoanzisha kada ya AMO na leo hii tunahitaji MO !

Tusjidanganye kwa kurudia kosa,eti tufyatue MO wa kutosha hata kama hawana kiwango...ni kosa linalojirudia!

Tunahitaji MO na specialists wenye viwango for sustainability of the healthcare system.
 

Conservatisim na desperation zinakutesa sana we jamaa.
 
Aliyeleta mada hii naye ni BOMU linalosubiri kulipuka, hoja yake ni 'fallacy of generalisation" kwani sioni mahusiano yaliyopo kati ya tukio hili la IMTU na UDOM, tuacheni kuongea vitu kishabiki, inawezekana ni kweli UDOM panaweza pakawa na changamoto zake kutokana na uchanga wa chuo hicho, lakini sidhani kama changamoto zile zinaweza zikawa ni sababu ya kutosha ya kuibeza serikali kwa kukianzisha! Kwani wanaofanya mambo sivyo wote walisoma UDOM? Hao madaktari waliopasua kichwa badala ya goti la mgonjwa nao walisoma UDOM ama IMTU? Hivi kwani SUA au UDSM nazo si zilianza zikiwa changa kama UDOM? Lakini pia vyuo hivi vikongwe navyo si vinamapungufu yake, ama vimekamilika kabisa na tunaweza kuvifananisha na OXFORD ama HARVAD? Na zaidi, mbona UDOM ilianzishwa na walimu wengi tu toka SUA, UDSM na kwingineko, au nao waliishiwa maarifa walipofika UDOM? Mkuu mleta mada acha mawazo mgando! Mbona tunashuhudia vijana wengi tu toka UDOM wakiwa na perfomance nzuri tu maofisini, na saa ingine wanawazidi wale waliosoma vyuo vikongwe? Aaaaargh......!
 

Nilielewa kuwa u punguani na hauwezi kunielewa.

Kuna vigezo vinavyotumika kuwadahili na hivyo hujaviweka, kwa hiyo argument yako ni upuuzi mtupu unless utuoneshe kuwa kuna vigezo vya udahili vilikiukwa amma kwa makusudi, amma kwa bahati mbaya amma kwa wadahiliwa kughushi amma kwa wadahili kufumba macho kwa sababu yoyote ile. Bila hivyo, hiyo yako ni hoja muflis na kama ni mahakamani kesi imeshatupiliwa mbali zamani na gharama zote unalipa.
 
Hahaha duh salsa wewe hebu jenga hoja nzito ,tupe matukio yanayothibitisha kuwa IMTU in chuo kibovu(cha kata)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…