Bomu la Ajira litamlipukia Rais Magufuli

Bomu la Ajira litamlipukia Rais Magufuli

Naona
w




Wanaojua kinachofanyika barabara ya ddm-babati, itigi, tabora-kigoma, hatua za kuanza std gauge Dar- mza, kigoma na miradi mingine mikubwa ya miundombinu hawajisumbui kuuliza makusanyo ya tra yanakwenda wapi..tembea uone hata kwa miguu itakusaidia vitu vya kuuliza.
Alikosea kutoa huo mfano maana ameandika vizuri ila huo mfano umekuwa Wa kiajabu kidogo.....tuvute subira natumaini ajira nitakuja kumwagika
 
Tatizo wengine wanapigania maslahi ya vyama wengine wanapogania maslahi ya nchi ..

Hapa ni ngumu kuelewana....
Safi mkuu. Kunywa soda kwa Mangi hapo nakuja kulipa.
Mtu km Lizabon na wenzake wanatetea chama, ni ngumu kukuelewa.
 
wanafiki no wengi mno,mnaongelea afya na elimu tu mbona Kuna sector nyingi zaidi ya hizo bora apge chini kwelj kuajir
 
Bom la wanafunzi wa shule za kata halikuwalipukia,na isitoshe vijana wengi wanaojiita wasomi hawakuipigia kura ccm mmoja wapo ni wewe mleta thread.

Pia sasa hv ni mapema mno kutabiri akili ya mtanzania katika siasa,watanzania hawana msimamo wa kisiasa,nadhani unajua it took only three month to break the record of 8 years.
 
leo hii kuna shule za msingi zina walimu 4 na ufaulu wa wanafunzi hauzidi watoto 5 mfano, huko nanyumbu shule ya msingi chitowe. watoto wamefeli Sana hakuna walimu wa kuwafundisha kwani si rahisi walimu 4 to cover wanafunzi kutoka darasa la 1 hadi la 7 kwa masomo yote. Then afisa Elimu anamlaumu na kumtaka mwalimu mkuu ajieleze Kwanini watoto wamefeli is it fair? serikali itoe ajira inahubiri elimu bure bila walimu wa kutosha haina maana, wanatafuta mbinu kibao kukwepa kuajiri au ule uvumi kuwa serikali haina pesa ni Kweli? kama ni kweli basi waeleze hadharan kuwa hali ni ngumu haina uwezo.
 
Big up mkuu...maana nilianza kupoteza imani na wewe..ila cha kushukuru unarudi kwenye msimamo ambao sisi wote tunaupigania.
Mkuu hujamjua vizuri huyu,analazimisha aonekane ni mtu wa kusimama kwenye maslahi ya taifa,analazimisha trade mark yake humu lakini haelewi kuwa there is no such a thing as neutral,asubuhi atatetea kitu jioni atapinga kitu kile kile,don't take him serioysly
 
Rais Jakaya Kikwete Pamoja na mapungufu yake mengi ya corrupt system aliyokuwa ameijenga lakini alifanikiwa kutoa Ajira kwa watanzania kila mwaka,kupandishwa madaraja kwa wafanyakazi kila mwaka,kupeleka wafanyakazi kusoma kila mwaka na mengine mengi.

Tanzania watu wanaingia kwenye soko Ajira kwa mwaka ni 800,000- 1000,000 .

1: Kila mwaka Kikwete alitengeneza Ajira rasmi serikalini kwa wastani wa 40,000 za Walimu Madactari,halimashauri na Wizarani.

2: Kila mwaka idadi ya watu walioajiriwa iliongezeka kwa mfano wakati anaingia mwaka 2005 serikali ilikuwa ikiajiri wastani wa wafanyakazi elfu 9,000- 12,000 kwa mwaka...

Lakini ameondoka serikali ina uwezo wa kuajiri wafanyakazi 40,000 kwa mwaka..

Sasa hivi mwaka unapita hata kupanda madaraja kwa wafanyakazi imeshindikana kisa uhakiki hivi uhakiki kwanini haufanyiki wa wakuu wa mikoa ,Wilaya na wakurugenzi na wakuu wa idala serikalini?..

Kichekesho na mshangao ni wakati serikali wapo kimya kwenye swala la Ajira

Serikali iko na upungufu wa walimu wa sayansi 25,000, madactari wa kawaida 7,000, madactari bingwa 1200 wauguzi 20,000 ..

Wakati huo kiwango cha wanafunzi wanaojiunga primary schools kikiongezeka kwa 84% na wanajiunga sekondari kwa 25%.

Lakini kikubwa zaidi sector binafsi Ajira zilikuwa nyingi lakini ndio hivyo tena Sera mbovu za uchumi zinaua hata Ajira zilizokuwepo...

Sector ya usafirishaji pekee Mfano mwaka ulioisha pekee maroli 15,000 yalipaki ambayo yalisababisha Ajira kati ya 30,000- 40,000 kupotea na vijana hawa kuingia mtaani..

Mwaka huu huu ulioisha tumeondoa wafanyakazi 19,000 kwenye payroll ya serikali na kuokoa pesa ambazo zingefanya tuajiri watu zaidi ya 20,000 kwa mpigo lakini mpaka sasa kimya.

Na wakati huo wastani wa makusanyo kutoka TRA ni kiasi cha 1.2 trions kwa mwezi.

Sasa unashindwaje kutoa Ajira kwa vijana wakati unakusanya trions 1.2 kwa mwezi kwa nini?

Hakuna serikali yeyote duniani inayo ajiri watu wote lakini hakuna serikali duniani ambayo haitoi Ajira kwa watu wote.

Kumbuka watanzania wanaishi kwenye poverty line ni 12,000,000 hawa utegemea ndugu zao walioajiriwa ili kujikwamua .

Sasa kama Ajira hakuna,Madaraja upandishi, wenye Ajira zao sector binafsi unaziua...

Unategemea nini hawa vijana wakizagaa mtaani? Magufuli Bomu unalotengeneza litakulipua.


Dahh hila hii hali ni mbayaa, Rais wetu awe makini na hili...Vijana wengi, uhalifu utaongezeka, Wizi...
Hali ni mbaya mitaani...Sio kila aliyemaliza chuo wanamaisha mazuri katk familia yao wengine wanategemewa
 
Dahh hila hii hali ni mbayaa, Rais wetu awe makini na hili...Vijana wengi, uhalifu utaongezeka, Wizi...
Hali ni mbaya mitaani...Sio kila aliyemaliza chuo wanamaisha mazuri katk familia yao wengine wanategemewa
Yes nawaonea huruma sana vijana
 
Hili bomu mbona tokea wakat wa kikwete tunaambiwa litaripuka? Suala la ajira ni gumu sio tanzania tu bali dunia nzima hata kwenye kampeni za urais marekani lilitajwa sana tu
Fatlia hata BBC SWAHILI basi....
 
Wanaojua kinachofanyika barabara ya ddm-babati, itigi, tabora-kigoma, hatua za kuanza std gauge Dar- mza, kigoma na miradi mingine mikubwa ya miundombinu hawajisumbui kuuliza makusanyo ya tra yanakwenda wapi..tembea uone hata kwa miguu itakusaidia vitu vya kuuliza.
We ufuatilii nani kakuambia ujenzi wa reli ni fedha za ndani? Nimkopo toka bank za china
Rais Jakaya Kikwete Pamoja na mapungufu yake mengi ya corrupt system aliyokuwa ameijenga lakini alifanikiwa kutoa Ajira kwa watanzania kila mwaka,kupandishwa madaraja kwa wafanyakazi kila mwaka,kupeleka wafanyakazi kusoma kila mwaka na mengine mengi...
 
Binafsi huwa nazifurahia articles zake kwani yupo very dynamic. Sio sawa na hawa wapiga siasa za kusibiri teuzi zisizoishi humu. Najua anawaacha mbali wale buku Saba wa mtaa uleee!
Keep doing technicality! Unawapa za USO baai tu nyuso zao ni za puto hazitoi manundu!
 
Tangua uingie madarakani walimu wa masomo ya arts umewapiga pini wanarandaranda mtaani miaka mitatu sasa na kila mwaka wanagraduate. Madaktari umetelekeza ambao ndo ilikuwa kimbilio la waroto maskini.

Hata walimu wa sayansi ambao enzi za jk walikuwa hot cake sasa hivi wanazulula tu mtaani lakini shule hazina walimu kabisa na ni miaka mitatu.

Zamani mtu akisomea ualimu au udaktari basi ajira hahangaiki kabisa na ilikuwa ndo mkombozi wa watoto maskini achilia mbali taaluma zingine kama uhasibu na engineer ambapo hata zenyewe ajira zilikuwepo japo za kuomba lakini zilikuwepo na fursa nyingi pia
Zamani enzi za jk hata kwenda upolisi au uanajeahi ilikuwa simple sana kwa hiyo vijana walikuwa na wigo mpana sana lakini sasa hivi kila kitu ni majanga hata biashara nazo imekuwa tatizo.

Usione vijana wnamshabikia sana tundu lisu wamekuchoka na wamesubili mtu wa kupuliza filimbi tu waki ready hata kuingia msituni.
Yaani wanaona afadhari hata hao mnaowaita mabeberu kuliko wanavyokufa na njaa ilihari wana mavyeti kibao.

Huo ni ushauri tu la sivyo venezuela inakuja tanzania soon.
 
Wanabodi,

Kama nchi tunapitia kwenye changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira. Ni bahati mbaya kuwa wengi tumejikita kwenye kulaumu badala ya kushauri.

Baya halijawahi kuhalalisha baya lingine Ila tuu Ni muhimu kujua kuwa tatizo la ukosefu wa ajira ni tatizo la kiulimwengu, tofauti ipo kwenye kiwango cha ukosefu wa ajira.

Nini kilipaswa kufanywa (ambacho hakijafanywa au hakifanywi ipasavyo) na;
1. Serikali
2. Jamiii
3. Watafuta ajira hasa vijana
4. Wazazi

Je, tatizo hili liko sawa kwa makundi na tabaka zote?

1. Vijana
2. Watu wa makamo
3. Watu wazima
4. Watanzania weusi
5. Watanzania wenye asili ya Asia
6. Watanzania wenye asili ya mabara mengine ukiacha bara la Asia
7. Watanzania wenye elimu ya msingi
8. Watanzania wenye elimu ya sekondari
9. Watanzania wenye elimu ya ngazi ya ashahada na astashahada
10. Watanzania wenye elimu ya shahada ya kwanza
11. Watanzania wenye elimu ya shahada ya uzamili na kuendelea

Kama kuna tofauti, je, unadhani tofauti hizo zinaletwa na nini?

Karibu sana.

Amani Msumari
Tanga
 
Mamvi mbona hajapanda jukwaani kumsaidia huyu jiwe?
 
Back
Top Bottom