Bomoabomoa Yaikumba Nyumba Ya Shilingi bilioni 1

Bomoabomoa Yaikumba Nyumba Ya Shilingi bilioni 1

Ama kweli nyani halioni.... Wewe mbona uwa unasapoti kila takataka ya ccm hapa..

Sasa shida yako nini haswa... eti nasapoti kila nini!!!! Endelea kunisoma utayaona... na chama chenu utakiitake kama unaita chama chao hivyo.. si hata neno utalikosa au? Eeeeeh hiyo methali inawahusu kabisaaaaa bila mpindo
 
Mita 120 ni sawa na zaidi ya urefu wa uwanja wa mpira, kama ni suala la sheria nafikiri majengo yote mkabala na barabara hayastahili kuwepo hapa DSM, hata majengo yale ya serikali katikati ya jiji. Kutolipa watu fidia ni uvunjifu wa haki za binadamu uliopitiliza. Unyakuaji ardhi bila fidia sasa umehamia kwa watawala badala ya matajiri kwa kisingizio cha kutucheleweshea maendeleo.
 
TLS + Lissu+ Wapinzani haya ndio mambo ya kushikia bango kuwatetea watu kama sheria ya 120M badala ya 60M ilitungwa wakati nyumba hizi zikiwa zimeshajengwa tayari na zipo nje ya 60M za hifadhi ya barabara.
Kama ni haki kuvunjwa sheria haijakiukwa basi wapeni elimu wananchi waitambue sheria. Pia muilazimishe serikali kuwazuia watu mapema wasijenge mahali pasiporuhusiwa ili kuepusha kadhaia kama hii yenye kutia watu umasikini mkubwa.

Tusiwekeze nguvu kubwa ktk kutetea wawekezaji toka nje kama ACCACIA na wawekezaji wengine wa viwanda walivyoshindwa kuviendeleza.
CC: Petro E. Mselewa
Pascal Mayalla
Umenipa nakala kama Mwanasheria,mpinzani au mtetezi wa ACACIA? Umenisikitisha sana mkuu kunijumuisha katika fikra zako.
 
Umenipa nakala kama Mwanasheria,mpinzani au mtetezi wa ACACIA? Umenisikitisha sana mkuu kunijumuisha katika fikra zako.
...kwani ulipowashauri CUF uliwashauri kama Mwanasheria,mpinzani au mtetezi wa Maalim Seif?
..usijifanye hujaiona TLS hapo kwenye hoja yake.,
.ama haikuhusu
 
So sad to these people.
But I believe God will be with you all the time,
Never give up any thing happen and go away that life is.
 
Sijaona hapo nyumba ya shs billion moja au usanii plus kiki kwa pikipiki ili siku akija raisi mwingine jamaa wa kiki walipwe fidia ya billion moja
 
Kwakweli ili la mita 120 kila upande ni jambo la kuwaumiz watu maana ilikuwa 60
Wakikurupuka wanaweka sheria mpya bila kuangalia kuwa wananchi wataumizwa na kuzoroteshwa uchumi.

Walitii sheria na kuacha mita 60 leo wanavunjiwa utadhani wamevunja sheria... so sad
 
Una roho ya kichawi sana wewe mchumia tumbo
Naona hukumuelewa....
Nilivyomuelewa mimi ni kuwa sheria ambayo ilikuwepo ni mita 60... kama wanaona haifai walitakiwa warejeshe bungeni ili ibadilishwe
 
Umenipa nakala kama Mwanasheria,mpinzani au mtetezi wa ACACIA? Umenisikitisha sana mkuu kunijumuisha katika fikra zako.
Mkuu nakala kama mwanasheria tu na si vinginevyo, kama umenielewa vibaya naomba tusameheane mkuu. Lengo hasa unifafanulie sheria hiyo ya umbali wa 120M ni ya lini? Nimesikitishwa sana na sakata hili la bomoa bomoa Morogoro road.
 
Usijali. Nitarudi hivi karibuni na elimu juu ya jambo hilo.
 
Back
Top Bottom