Bomoabomoa Yaikumba Nyumba Ya Shilingi bilioni 1

Bomoabomoa Yaikumba Nyumba Ya Shilingi bilioni 1

Mmhh usiombe yakukute, usiombe kabisa nyumba uliyoijenga kwa mkopo iliyoijenga kwa kujibana umeamua kutokuvaa vizuri ili angalau ujenge MTU unavaa kiatu kimechoka kimepinda unajikaza angalau na wewe uwe na kwako wàtoto wako mda mwingine wanakula vyakula ambavyo hata wewe mzazi havikuridhishi................

Alafu Leo hii linakuja agizo na unajua kwamba nyumba yako pia itakua kenye mkumbo Wa kubomolewa inauma hujui utaenda wapii mmmhh inauma Mimi binafsi naomba Mungu yasinikute omba Mungu yasikukute na hao yaliyowakute Mungu awatie nguvu yakutokukata tamaa Luna maisha baada ya hapo
 
Ni vizuri hekima itumike ili kila upande ujiridhishe....

Sio kutumia maguvu na mikwara mingi eti unanyoosha nchi...

Mfalme Suleimani aliomba Hekima na Busara mengine Mwenyezi Mungu alimuongezea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ni msumeno...kama mnaona sheria mlizozitunga hazifai zirejesheni bungeni basi.

Huko hata mkitaka nyumba zijengwe katikati ya barabara ni juu yenu.

Kwa sasa acha sheria iliyopo ifuate mkondo.
Sheria ni msumemo pale ambapo hazijawagusa wakubwa tu
 
Hawa waandishi sijui walisomea wapi kazi eanazofanya.. mtu analeta habari ya upande wa wenye nyumba.. yaani wamekosa ujuzi kwenda wizara ya ardhi kupata habari kamili.. na kuacha haya ya wananchi kutokupata ukweli na wengine kujua na kujipanga katika maisha yao kueasaidia na haya ya barabara.. ni bure kabisa hawa waandishi wa nchi yetu.. yaani bure kabisa

Mwakyembe fanya ulilotaka kucheki juu yao
 
Mimi sielewi kwa nini kubomolewa nyumba ya 1b imekuwa ishu hapa. Huyu kama ameweza kujenga nyumba ya thamani hiyo hawezi kukosa mahala pa kuishi. Kwangu mimi zile nyumba ambazo zimechakaa na wananchi wake hawana uwezo wa kuzikarabati na wanaishia kubomolewa ndio ishu. Wanachi hawa wataishia kulala nje hivyo kuwakosesha hitaji muhimu la binadamu kulingana na azimio la arusha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ni msumeno...kama mnaona sheria mlizozitunga hazifai zirejesheni bungeni basi.

Huko hata mkitaka nyumba zijengwe katikati ya barabara ni juu yenu.

Kwa sasa acha sheria iliyopo ifuate mkondo.
Hayo yasikie tu kwa mwenzio. Siku yakikukuta ndio utajua uchungu wanaoupata.
 
Hilo jimbo kwakweli ccm wasiegemee kulipata kwa hali jinsi ilivyo
 
Anyway, tusubirie ya Mahakamani! Kama Fidia haijalipwa basi huo ni Ukatili dhidi ya Binadamu! Pia ni dharau kwa Mahakama ambayo ilishatoa Amri ya Kuzuia zoezi Hilo! Tunaposema huyu ni DU haya ndiyo yanayofanya aitwe hivyo! Haheshimu Utawala wa Sheria, AG nae yupo tu, how comes Sheria zina act retrospectively katika utawala huu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwezekeza kwenye hifadhi ya barabara kwa kutegemea huruma ya serikali ni sawa na kuhifadhi maji kwenye gunia.
Tumia akili kidogo tu na usome maelezo ya huyo mama vizuri! Wakati wanajenga Sheria iliyokuwepo iliwataka kujenga mita 60 baada ya Barabara! Kuna Sheria nyingine iliyokuja mpya inayotaka watu wajenge mita 120 baada ya Barabara! Hii mpya imekuta watu wameshajenga, hivyo kuitekeleza kunahitaji Serikali kutoa fidia kuwahamisha hao watu ndani ya hizi mita,kwa sababu sii kosa lao,ni Kosa la short sighted people from the govt waliokuwa na maono mafupi kwa kutunga Sheria ya mita 60! Naamini nitakuwa nimekusaidia!

Swala linabaki palepale, kujenga kwenye hifadhi ya barabara ni sawa kuteka maji kwa kutumia gunia. Kwa sababu kama unajua sheria zinabadilika mara kwa mara kutokana na mahitaji yaliyopo kwa nini usiwekeze sehemu unayojua haiwezi kuathirika na hizo sheria hata zikibadilika? Unajenga kwenye highway eti unaishia kwenye 60 zilizowekwa na sheria si upuuzi huo. Kwa nini na wewe usiongeze mita zako chache ili kujihakikishia usalama zaidi?
 
Sheria ni msumeno...kama mnaona sheria mlizozitunga hazifai zirejesheni bungeni basi.

Huko hata mkitaka nyumba zijengwe katikati ya barabara ni juu yenu.

Kwa sasa acha sheria iliyopo ifuate mkondo.
We una hata kibanda cha tembe kweli?
 
Nani wakulaumiwa ikiwa serikali ilizitazama hizo project tangu mwanzo mpaka mwisho! Hasara hii atailipa nani sasa!
 
Swala linabaki palepale, kujenga kwenye hifadhi ya barabara ni sawa kuteka maji kwa kutumia gunia. Kwa sababu kama unajua sheria zinabadilika mara kwa mara kutokana na mahitaji yaliyopo kwa nini usiwekeze sehemu unayojua haiwezi kuathirika na hizo sheria hata zikibadilika? Unajenga kwenye highway eti unaishia kwenye 60 zilizowekwa na sheria si upuuzi huo. Kwa nini na wewe usiongeze mita zako chache ili kujihakikishia usalama zaidi?
Nilidhani nimekusaidia kumbe husaidiki! Najua unalenga kuyahalalisha haya ya Ubomoaji! Ni mtu mpuuzi tu anaeweza kuja na argument kama hii! Kinachofanya jambo Fulani kuwa Kosa ni Sheria ya kipindi hicho, sio Speculations! Serikali ndiyo iliyopewa jukumu na walioiweka madarakani kufikiri na kutenda kwa niaba yao, not otherwise!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom