Hivi kweli vitendo kama hivi ni muhimu? Kwanini wasiwape muda wa kuhamisha vitu vyao?
some times ubabe kama huu unahitajika. Watu tumekuwa na tabia ya kuijaribu nguvu ya serikari. wewe umeshalipwa na umeambiwa uondoke kupisha maendeleo halafu unang'ang'ania kubaki unategemea nini? kwanza nyumba zenyewe zilijengwa kienyeji bila kuzingatia ramani za mipango miji, jamani hamuoni miji ya wenzetu inavyopendeza? cheap things are always expensive bwana.
Hivi kweli vitendo kama hivi ni muhimu? Kwanini wasiwape muda wa kuhamisha vitu vyao?
Labda kama watu wamekaidi amri ya mahakama, vinginevyo kwa nchi maskini kama za kwetu, hatutakiwi kabisa kuharibu mali za wananchi kwa njia kama hizi.
Tinga tinga lipo kazini ,Mpaka saizi bomoa bomoa imepamba moto.
View attachment 1974
Tatizo hao watu wa mipango miji, hiyo miji hivi waliipanga llini? baada ya watu kujenga kiholela au? Je hao watu walipokuwa wakiuziana viwanja na kujenga kuna yeyote (hata balozi nyumba kumi..) aliyewaambia hili ni eneo la bandari?,...kama hakuna sasa inakuwaje wanabomolewa bila kulipwa kikamilifu?
tatizo kubwa zaidi ni kwamba ujenzi holela bado unaendelea kama kawa, next 5 years tutasikia wengine tena wamebomolewa ili kupitisha mabomba ya maji!
Hivi kweli vitendo kama hivi ni muhimu? Kwanini wasiwape muda wa kuhamisha vitu vyao?
Labda kama watu wamekaidi amri ya mahakama, vinginevyo kwa nchi maskini kama za kwetu, hatutakiwi kabisa kuharibu mali za wananchi kwa njia kama hizi.
..mswahili habembelezeki na hana ustaarabu huo unaoutegemea.
..ingekuwa hivyo tungefika mbali sana.
..ni kweli hawabebeki..kama wale waliosaidiwa na rais akawaapa milionmi 20 kila mmoja pale tabata dampi..sasa wanagoma kufuta kesi waliyoahidi baada ya kulipwa ..SAASA WANATAKA WAPEWE TENA MILIONI 30 KILA MMOJA
Nadhani Watanzania we are learning the hard way. Inawezekana ndiyo njia pekee.....Si waombei haya, lakini panapokosekana mshikamano katika mambo makubwa ndiyo yanayotokea. Tunahitaji kujiuliza kama hakuna njia za kistaarabu zaidi? Kama vyombo vyote husika vilitimiza majukumu yao? Kama hakuna mipangilio katika mambo yote ndiyo inavyotokea. Wenzetu mlioko nje ni vema mkatupa pia uzoefu kwa wenzetu haya mambo yanafanyikaje mbona hatusikii vya hivi? Ni ngozi nyeusi ina matatizo zaidi au nini? Lakini pia kwanini kuna Estate developers kwa wenzetu? kwanini kuna credit facilities zikiwemo za nyumba kwa wenzetu? Hivi ukilipwa 12 huna ardhi utajenga wapi? labda tu apply hadithi ya Abunuwas....Nadhani Wanaharakati Tunahitaji uchambuzi wa kina. Haiwezekani kila kona ya nchi yatokee haya na daima wananchi wawe wakosaji tu..... Tunajitaji kuchambua na kutibu once for all. Wasio husika hasa wanawake na watoto, na wapangaji wasio hata na taarifa ya kinachoendelea wanaumia sana.Tinga tinga lipo kazini ,Mpaka saizi bomoa bomoa imepamba moto.
View attachment 1974