Abtali mwerevu
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 652
- 488
UKATILI,HUZUNI,UZANDIKI, KICHEKO
Nilipita Mkwajuni na Jangwani, nikaona familia zilizobomolewa nyumba zao zikiishi nje ya vifusi, pembezoni mwa maji machafu na chini ya vipande vya mabati na miti. (UKATILI).
Wananchi hawa wote wanamlaani Magufuli kwa kumuombea kila aina ya dua mbaya, aliahidi kuwatoa katika dimbwi la umasikini, lakini sasa amesha watumbukiza katika shimo refu la ufukara. (HUZUNI).
Magufuli anahujumiwa na NEMC. chombo kilichobeba nyundo kubomoa kila aina ya nyumba ya mnyonge! Magufuli aliyekulia katika familia ya "changa tushibe" ambaye amewahi hata kuuza furu (dagaa) ili kupata kipato cha kusukuma siku hawezi kuwanyang'anya wananchi wake hitaji muhimu (basic need) ya makazi. (UZANDIKI).
Nyumba 16,000 zinatakiwa kubomolewa, zaidi ya watu 400,000 watakosa makazi. "Elimu bure kulala nje" (KICHEKO).