Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,666
- 729,805
Watu walichukizwa na hii bomoabomoa wamefanya yao! Hizi ndio habari motomoto mitaani uswazi na kwenye radio mbao! Kwamba eti msimamizi mkuu wa hii operation alipigwa kipapai akaanguka na kuzirai ofisini kwake lakini hakufa! Na hata alipopelekwa hospital hakuonekana na tatizo lolote!
Lakini likaja na hili pia kwamba yule Dereva wa kile kijiko (greda/tingatinga) la ubomoaji yuko hoi hospitali... Huku uswazi ni full shangwe watu wanafanya sherehe eti wamewaweza..! Hili laweza kuwa kweli lakini tusibebwe na mass hallucination kwa sababu zifuatazo
Kwanza kuanguka kwa yule msimamizi hakuna mahusiano ya moja kwa moja na ushirikina, na hata huyo dereva pia... Maelezo yanayoweza kuwa sahihi zaidi ni uchovu na tension ya zoezi zima na kule kuhukumiwa na roho kwa kile wanachofanya huku wakishuhudia kina mama watu wazima watoto wasiojiweza wagonjwa na wazee wakitoa machozi ya uchungu kwa kubomolewa nyumba zao. Inahitaji roho ngumu mno kuweza kuhimili hiyo hali.
LAKINI Kama kweli Uchawi unahusika kwenye hali zao zilizowapata basi ni kutokana na kubomoa nyumba zenye mazindiko na makafara, yaani wameingia pasipo ingilika... Kiukweli ni kwamba kuna nyumba sizo kabisa zimebebeshwa vitu vya ajabu na vya kutisha mno! Wanaopanga uswazi ni mashuhuda kwenye hili.
Kuna nyumba ni gateway ya kuzimu kuna nyumba ni vilinge vya wachawi kuna nyumba zimeshafanyiwa mambo ya ajabu mno na kuharibiwa kabisa kutokana na mirathi dhuluma nknk, kwahiyo ukiingia kwenye anga zake huko lazima likupate la kukupata.
Operation bomoabomoa ina wahusika wengi Kama kweli ni kipapai kingeanza kupukutisha mamlaka za juu mpaka chini na isingekuwa watu wahusika wawili tu tena ambao yaliyowapata hayana ithibati za moja kwa moja na ushirikina.

Last edited by a moderator: