Bomoabomoa Dar! Kwa jicho la kishirikina

Bomoabomoa Dar! Kwa jicho la kishirikina

wakati yanabomolewa ilitolewa hadi kwenye Tv njia ya iringa ukiipita utaiona hayo makaburi na jinsi umeme ulivyo chepuka

Mchepuko ulishaondolewa lile kaburi limehamishwa baada ya TANROADS kuwapa wanafamilia fedha za kupiga makafara.
 
Ipo moja pale oysterbaby police Karibu na ubalozi wa marekani, nyumba ya ghorofa moja zamani ilikuwa na rangi nyeupe siku hizi imekarabatiwa! Ile nyumba imeua wamiliki watatu na mmiliki wa sasa baada ya kufanya makafara sana yeye kapona ila halali kwenye ile nyumba
Mkuu Mshana naomba ukienda Moshi uende pale Rau mbele kidogo ya Chuo cha Ushirika Moshi mkono wa kushoto upate dondoo za Ghorofa fulani hivi kubwa halilali mtu wala kukaa mtu ni full majanga.
 
kwanza mie siaongelea kuhusu Tingatinga mie nimeongelea kuhusu maeneo ambapo kuna paranomal activities nashangaa umetoka ulikotoka kubisha na kuniambia niache fix

sidhani wewe ni mtoto wa mjini kwa maana mtoto uliyezaliwa na kukulia kariakoo, upanga, magomeni kama ungekuwa umezaliwa na kukulia huku usingesumbua na maneno yako kwani watu wamekutana nalo sana jini la fire tena ni mwanamke na huwa anavaa hijab...


wakongwe mtanisaidia nakumbula enzi za 90s mwanamke ukivaa hijab ukapita fire saa saba usiku hautapigwa ngwala na vibaka wala nini coz ya urban legend hiyo

au uliza madereva taxi wa kariakoo wale wakongwe wa enzi na enzi watakupa story nyinyi mliokuja dar baada ya kuingia chuo kikuu mnatusumbua sana
Mkuu umenikumbusha miaka ya 80s na 90s eneo la Chang'ombe Polisi kwenda Mataa ya Chang'ombe/Kibasila Secondary enzi hizo panaitwa machinjioni kuelekea Keko lile eneo ikifika mida ya saa12 jioni mpaka saa moja asubuhi kulikuwa na vituko sana pale. Unaweza ukawa unapita ukasikia sauti ya skuna zikilia nyuma yako ukigeuka huoni kitu,pia unaweza kumuona Mwanamke mzuri mbele yako kavaa baibui ukicheki chini ana kwato mara ghafla kayeyuka.
 
mshana jr, kweli kabisa ushirikina katika mambo haya unahusika sana.... NA wenyewe wanajinasibu Kwa mambo hayo....
 
Watu walichukizwa na hii bomoabomoa wamefanya yao! Hizi ndio habari motomoto mitaani uswazi na kwenye radio mbao! Kwamba eti msimamizi mkuu wa hii operation alipigwa kipapai akaanguka na kuzirai ofisini kwake lakini hakufa! Na hata alipopelekwa hospital hakuonekana na tatizo lolote! Lakini likaja na hili pia kwamba yule Dereva wa kile kijiko (greda/tingatinga) la ubomoaji yuko hoi hospitali... Huku uswazi ni full shangwe watu wanafanya sherehe eti wamewaweza..! Hili laweza kuwa kweli lakini tusibebwe na mass hallucination kwa sababu zifuatazo

Kwanza kuanguka kwa yule msimamizi hakuna mahusiano ya moja kwa moja na ushirikina, na hata huyo dereva pia... Maelezo yanayoweza kuwa sahihi zaidi ni uchovu na tension ya zoezi zima na kule kuhukumiwa na roho kwa kile wanachofanya huku wakishuhudia kina mama watu wazima watoto wasiojiweza wagonjwa na wazee wakitoa machozi ya uchungu kwa kubomolewa nyumba zao. Inahitaji roho ngumu mno kuweza kuhimili hiyo hali
LAKINI Kama kweli Uchawi unahusika kwenye hali zao zilizowapata basi ni kutokana na kubomoa nyumba zenye mazindiko na makafara, yaani wameingia pasipo ingilika... Kiukweli ni kwamba kuna nyumba sizo kabisa zimebebeshwa vitu vya ajabu na vya kutisha mno! Wanaopanga uswazi ni mashuhuda kwenye hili
Kuna nyumba ni gateway ya kuzimu kuna nyumba ni vilinge vya wachawi kuna nyumba zimeshafanyiwa mambo ya ajabu mno na kuharibiwa kabisa kutokana na mirathi dhuluma nknk, kwahiyo ukiingia kwenye anga zake huko lazima likupate la kukupata
Operation bomoabomoa ina wahusika wengi Kama kweli ni kipapai kingeanza kupukutisha mamlaka za juu mpaka chini na isingekuwa watu wahusika wawili tu tena ambao yaliyowapata hayana ithibati za moja kwa moja na ushirikina
 

Attachments

  • 1452488525503.jpg
    1452488525503.jpg
    8.2 KB · Views: 48
Mengine sio ya kupuuzia!
 

Attachments

  • 1452488612880.jpg
    1452488612880.jpg
    8.2 KB · Views: 48
Hayo makubwa tena ndumba zimeaza hata zoez halijakamilika.,mmmh heh.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Maph huwezi kumwelewa mshana jr. Yawezekana ni mtafiti wa mambo ya ushirikinA au amekulia mazingira hayo
 
makaburi ya kiyeyeu nguzo za umeme zili divert kwani walikuwa wakiweka umeme juu yake umeme haupiti na ni ule gridi ya taifa wakaona isiwe tabu waka divert ila juzi juzi makaburi hayo yamehamishwa
Yamehamishwa baada ya kuwaita ndugu na ukoo wa chief aliezikwa na kukubaliana na ndugu kuridhia kuamishwa
 
Mkuu umenikumbusha miaka ya 80s na 90s eneo la Chang'ombe Polisi kwenda Mataa ya Chang'ombe/Kibasila Secondary enzi hizo panaitwa machinjioni kuelekea Keko lile eneo ikifika mida ya saa12 jioni mpaka saa moja asubuhi kulikuwa na vituko sana pale. Unaweza ukawa unapita ukasikia sauti ya skuna zikilia nyuma yako ukigeuka huoni kitu,pia unaweza kumuona Mwanamke mzuri mbele yako kavaa baibui ukicheki chini ana kwato mara ghafla kayeyuka.
pia nilisika story kuwa kulikuwa na nyoka mkubwa maeneo yale.ya mataa huwa anakatiza kuelekea kule makaburini
 
Watu walichukizwa na hii bomoabomoa wamefanya yao! Hizi ndio habari motomoto mitaani uswazi na kwenye radio mbao! Kwamba eti msimamizi mkuu wa hii operation alipigwa kipapai akaanguka na kuzirai ofisini kwake lakini hakufa! Na hata alipopelekwa hospital hakuonekana na tatizo lolote!

Lakini likaja na hili pia kwamba yule Dereva wa kile kijiko (greda/tingatinga) la ubomoaji yuko hoi hospitali... Huku uswazi ni full shangwe watu wanafanya sherehe eti wamewaweza..! Hili laweza kuwa kweli lakini tusibebwe na mass hallucination kwa sababu zifuatazo

Kwanza kuanguka kwa yule msimamizi hakuna mahusiano ya moja kwa moja na ushirikina, na hata huyo dereva pia... Maelezo yanayoweza kuwa sahihi zaidi ni uchovu na tension ya zoezi zima na kule kuhukumiwa na roho kwa kile wanachofanya huku wakishuhudia kina mama watu wazima watoto wasiojiweza wagonjwa na wazee wakitoa machozi ya uchungu kwa kubomolewa nyumba zao. Inahitaji roho ngumu mno kuweza kuhimili hiyo hali.

LAKINI Kama kweli Uchawi unahusika kwenye hali zao zilizowapata basi ni kutokana na kubomoa nyumba zenye mazindiko na makafara, yaani wameingia pasipo ingilika... Kiukweli ni kwamba kuna nyumba sizo kabisa zimebebeshwa vitu vya ajabu na vya kutisha mno! Wanaopanga uswazi ni mashuhuda kwenye hili.

Kuna nyumba ni gateway ya kuzimu kuna nyumba ni vilinge vya wachawi kuna nyumba zimeshafanyiwa mambo ya ajabu mno na kuharibiwa kabisa kutokana na mirathi dhuluma nknk, kwahiyo ukiingia kwenye anga zake huko lazima likupate la kukupata.

Operation bomoabomoa ina wahusika wengi Kama kweli ni kipapai kingeanza kupukutisha mamlaka za juu mpaka chini na isingekuwa watu wahusika wawili tu tena ambao yaliyowapata hayana ithibati za moja kwa moja na ushirikina.
Mkuu unaingia unatoka.....yote ni sababu ya wenye shingo ngumu ila wajuvi tumekupata vema
 
Huwa nashangaa sana mtu haamini kua uchawi upo lakini anaamini Mungu yupo. Hehehe kwanza uchawi una proof inayoonekana zaidi kuliko hata proof ya uwepo wa Mungu.
 
Back
Top Bottom