Uchambuzi wa ovyo kabisa. Mimi nakumbuka nyumbani kwetu tulikumbwa na sakata la mita 60 toka ziwani, na na sheria hiyo ilitukuta na hakuna aliyebisha zaidi ya kuondoka. Kwa ufupi, waache wabomolewe, na wabomolewe kweli, maana wananchi wa Dar mnajifanya mna haki zaidi. Mfano, sisi kivuko cha feli busisi mwanza tunavusha gari (mfano Kluga) kwa shs 6500, ila nyie wa dar mnalalamika.Bomoa Bomoa ya makazi, nyumba, majengo na mali Morogoro Road Kuanzia Ubungo mpaka Kiluvia.
Leo mbunge wa Kibamba John Mnyika alikuwa na mkutano na wananchi wa jimbo lake kuhusiana na barua zilizosambazwa hivi siku 10 zilizopita kwa wakazi wa maeneo kutoka Kimara Mjini mpaka Kiluvia na TanRoads na alama za kutaka nyumba, majengo na mali kubomolewa kwa kuwa zinasemekana ziko kwenye hfadhi ya barabara ya Taifa.
Barua hizi zimetolewa na TanRoads MKoa wa Dar Es Salaam na mazungumzo ya watu yamechukua mkondo usio makini na kulifanya hili ni jambo la kisiasa.
Wengi wanaongea bila kujua undani wa jambi hili na zaidi ni ushabiki usio na mantiki.
1. Miaka ya 70,80,90 Serikali iligawa maeneo along Barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo a kuendelea hadi Kiluvia kutokana na wananchi waliopoteza makazi maeneo kadhaa ya jiji na hata kusaidia kupanuka kwa jiji.
2. Asilima kubwa 75% ya waliojenga nyumba, majengo ni halali na hata kwenye ramani za mipango miji za wizara ya ardhi, hizo nyumba na maeneo hayako kwenye Road Reserve.
3. Kwa mujibu wa wizara ya ardhi, eneo qualifying kuwa road reserve ni kati ya mita 30 hadi 60 kutoka katikati ya barabara. hii pia iko katika sheria zilizotumika na kuendelea kutumika kuhusu maeneo.
4. TanRoads (iliyoanzishwa 2000s) inadai kuwa road reserves ni mita 120 kutoka katikati ya barabara ambayo nikutokana nasheria ya barabara ya mwaka 1926/27.
5. Marekebisho kadhaa ya sheria ya barabara yameshafanyika tangu tupate uhuru na ndio maana Wizara ya ardhi, manispaa wanatumia sheria mpya na kuhusisha maeneo katika mipango miji.
6. Barabara ya Morogoro,eneo la Ubungo mpaka KImara mjini, TanRoads imetumia upana wa mita 30 na wakati wa kujenga mwendo kasi ikapanua mpaka mita 45 kutoka katikati ya barabara. Maeneo kutoka KIbaha kuelekea Chalinze, Tanroads inatumia sheria ya sasa ya mita 30 kutoka katikati ya barabara kila upande.
7. Bomoabomoa inayozungumziwa leo ni kutoka KImara Mjini/StopOver mpaka Kiluvia na TanRoads wanadai eneo la mita 120 kutoka katikati ya barabara (pande zote mita 120!)
8. Shauri hili lilishapelekwa mahakamani miaka iliyopita na TanRoads ilishindwa kesi. Hata wakati Waziri wa Ujenzi kati ya mwaka 2000 -2015 alipojaribu kung'ang'ania sheria ya mwaka 1927, si mahakama pekee, bali hata sheria za barabara na baraza la Mawaziri liliafiki kuwa ukubwa wa mwisho ni mita 60 kutoka katikati ya barabara kwa pande zote (jumla upana mzima mita 120). Hili linahitaji uchambuzi wa zaidi pamoja na kumbukumbu husika kuthibitisha hivyo.
9. Inasemekana kuwa miaka ya mwisho ya 90, kwenye mpango wa upanuzi wa barabara hii, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (WB/IMF) waliipa Serikali fedha za fidia kwa watakaolazimika kuhama maeneo yatakayo bomolewa kwa kufanya tathmini ya nyumba, majengo na mali zilizoko kwenye eneo litakaloathirika. Mpaka sasa hakuna mkazi ambaye imethibitika alipatiwa kiwanja kipya cha kuhama na kupewa fidia mali yake kubomolewa na hakuna kumbukumbiu kuonyesha malipo haya yalifanyika vipi.
10. Bomoabomoa ya sasa inafanywa na TanRoads mkoa wa Dar. Inasemekana ngazi zote zilizoulizwa(mawaziri Tamisemi, Ardhi, Ujenzi, TanRoads na hata Waziri Mkuu)kila mmoja inarusha mpira kwa mwenzake na vidole vinaelekezwa mamlaka ya juu ya Mkoa na Nchi.
11. Serikali kutokana na kauli inayosemekana ni ya Rais, inasema haitatoa fidia wala kutoa maeneo mapya kwa waathirika(inabidi kuthibitishwa kama ni kweli).
12. Barabara kuu ya kuingia Dar, imebadilishwa katika mipango ya barabara kuu na kuhamia upande wa Daraja la Kigamboni na highway kuu mpya imeshaanza kukwanguliwa miaka kadhaa iliyopita na itapita pembeni ya mji mpaka Ruvu au Chalinze kwenye maeneo ambayo yako wazi na hayana watu na gharama ni nafuu ukizingatia hakutakuwa na haja ya kubomoa au kutoa fidia kwa watu watakaoathirika kwa kiwango cha kutoka Ubungo pale Sam Nujoma na Morogoro road zinapokutana mpaka Ruvu.
13. Inasemekana mpango wa kupanua barabara hii kutoka Ubungo uko hati hati kutokanana kukosekana kwa fedha na kipaumbele kupelekwa maeneo mengine ya nchi yananayohitaji upanuzi wa barabara, fedha na kipaumbele kuwekwa barabara ya kutoka daraja la kigamboni, fly over za Tazara na Ubungo, Daraja jipya kutoka Aga Khan mpaka Coco Beach, Bandari ya Bagamoyo, Reli mpya na miradi mingine ya miundo mbinu nchini. Mradi unasemekana umesimama kwa kati ya miaka mitano hadi saba na hivyo kuweza kutoa fursa njema kwa mipango inayoeleweka kufanyika ikiwa na kuwapa wakazi watakaoathirika maeneo mapya ya kuhamia na fidia.
Kwa kutazamo hayo mambo 13 niliyataja hapo juu, ni wazi kuna ulazima wa jambo hili kufanywa kwa umakini, haki na kuthamini utu na si kufanyiwa upambe na ushabiki wa kisiasa.
Tafakari ni waathirika wangapi na kiasi gani kitatumika kutoa fidia au hata kufanya zoezi la ubomoaji.
Ndo utekelezaji wa ahadi ya waliokua wanaishi km malaika waishi km shetaniBadala ya kuondoa umaskini kwenye jamii serikali inakazana kutengeneza umaskini ok acha mungu ataamua
Yaani mtu amekuwa akikutapeli kwa muda wa miaka zaidi ya 20.,,.na baada ya kumgundua pia unatakiwa umlipe fidia....!!!!??Valiokutwa na vyeti feki wengine walikuwa wakilipwa mishahara kwa zaidi ya miaka 20, Sasa wameondolewa kazini na yet, serikali inaangalia uwezekano wa kuwalipa mafao yao. Kwa nini hawa wanaoishi kwenye road reserve waondolewe bila ya fidia hata kidogo
Very interesting perspective!Mtazamo wangu:
Hii nguvu kubwa ya kubomoa hizi nyumba inatokana na matajiri wanaotaka kujenga na kuendesha hii barabara kwa njia ya ushirikiano na serikali lakini kwa kutoza ushuru watumiaji wa hii barabara...
Ukiangalia gharama za ujenzi wa hii barabara kwa vyovyote vile wawekezaji hawatarudisha fedha zao kwa muda mfupi pia kwa kuzingatia sera nyingine za serikali kama ujenzi wa reli mpya na kituo cha magari makubwa nje ya jiji na pia serikali kuhamia dodoma...
Hii ardhi inayotafutwa bila fidia ndiyo mahali watakapopiga fedha...serikali ikisitisha ujenzi wa hii barabara kwa ubia utaona kabisa suala la kubomolea watu mita 121.5 kila upande litaisha
unaweza kutupatia link ya hii document?Ni vizuri ukajua kwamba ni kweli kila wakati mahitaji yanapokuwa ni lazima, basi Serikali hutwaa ardhi kukidhi matakwa hayo, na kwa ajili hii hulipa fidia. Sehemu inayozungumziwa imebadilishwa na Sheria ya 2007 na hasa kanuni chini ya sheria hio za 2009 na eneo la kama kilomita 20 tu ndio linahusu upana wa 120m. Kwa uhakika wananchi wale wanastahili fidia kwani barabara imewafuata.- Nukuu za Road Regulations za 2009 hizi hapa
View attachment 509598
unaweza kutupatia link ya hii document?
unaweza kutupatia link ya hii document?
Nimeweza kupata hiyosheria ya 2009 na kama sikukosea, kipande ulichonukuu cha 29 (2) kinaelezea specific kuhusu Morogoro road na kipengele 29 (1) kinabainisha upana na kipimo halisia cha barabara.Ni vizuri ukajua kwamba ni kweli kila wakati mahitaji yanapokuwa ni lazima, basi Serikali hutwaa ardhi kukidhi matakwa hayo, na kwa ajili hii hulipa fidia. Sehemu inayozungumziwa imebadilishwa na Sheria ya 2007 na hasa kanuni chini ya sheria hio za 2009 na eneo la kama kilomita 20 tu ndio linahusu upana wa 120m. Kwa uhakika wananchi wale wanastahili fidia kwani barabara imewafuata.- Nukuu za Road Regulations za 2009 hizi hapa
View attachment 509598
Mganga wa jF !Ila tu niseme kwamba kuna roho za uharibifu zimetajwa mpaka kwenye misahafu, hili ni pepo baya sana.
...daima halitengenezi bali linaharibu na likitengeneza kitu hakitakosa kuwa na walakini mkubwa....
Hiyo ndio roho ya uharibifu ilivyo
Tunahitaji kuwa na barabara pana eneo husika Lakini hekima na utu vitawale watu walipwe fidia waondoke kwa amani ubabe hautatufikisha popote
NI HATARI SANA MTU KUONGELEA KITU ASICHOKIJUA KIUSHABIKI. SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA CHINI YA MWALIMU NYERERE MWISHONI WA MIAKA 1960 ILILIPA FIDIA KWA MITA 22.85 TU TOKA KATIKATI YA BARABARA, PANDE ZOTE MBILI KATI YA MITA 121 ZILIZOTAMKWA KATIKA SHERIA YA BARABARA YA 1967. WAKATI WA UJENZI WA BARABARA HII YA SASA YA MOROGORO MWANZONI WA MIAKA YA 1970 WALIOLIPWA FIDIA YAANI MITA 22.85 NDIO TU WALIOTAKIWA KUPISHA UJENZI. NA KWA KUWA SERIKAKI ILIKUWA HAJALIPA FIDIA TOKA MITA 23 WALIRUHUSIWA KUREJESHA MAKAZI YAO BAADA YA MITA 23. MWAKA 1975 SERIKALI YA NYERERE IKIJUA KUWA HIFADHI YA BARABARA YA MOROGORO NI MITA 22.85 ILIZOLIPA FIDIA ILIWAHAMISHIA WATU KATIKA VIJIJI VYA KIMARA,MBEZI, KIBAMBA NA KILUVYA NA KUWAGAWIA ARDHI TOKA MITA 22.85 TOKA KATIKATI YA BARABARA. BAADHI YA WALIOGAWIA ARDHI HIZO ZILIPIMWA NA SERIKALI NA IKAWAPATIA HATI MILIKI AMBAZO WANAZILIPIA HADI LEO. HIVYO TUACHE USHABIKILakini nakumbuka wote waliojenga barabara ya Morogoro road walilipwa miaka mingi iliyopita fidia yao.
Hao wanaodai sasa wamejenga baada ya malipo kufanyika na ramani ipo mamlaka husika kwa ushahidi.
Uwezekano wa kulipwa fidia unaweza kuwa mdogo sana kwa wenye nyumba unless otherwise
Sasa ulichoandika wewe maneno mengiiii na nilichoandika Mimi Kuna tofauti gani!! Au kwavile umewatanya maraisi na miaka basi ndiyo unajua na sie wa gezaulole hatujui kitu.NI HATARI SANA MTU KUONGELEA KITU ASICHOKIJUA KIUSHABIKI. SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA CHINI YA MWALIMU NYERERE MWISHONI WA MIAKA 1960 ILILIPA FIDIA KWA MITA 22.85 TU TOKA KATIKATI YA BARABARA, PANDE ZOTE MBILI KATI YA MITA 121 ZILIZOTAMKWA KATIKA SHERIA YA BARABARA YA 1967. WAKATI WA UJENZI WA BARABARA HII YA SASA YA MOROGORO MWANZONI WA MIAKA YA 1970 WALIOLIPWA FIDIA YAANI MITA 22.85 NDIO TU WALIOTAKIWA KUPISHA UJENZI. NA KWA KUWA SERIKAKI ILIKUWA HAJALIPA FIDIA TOKA MITA 23 WALIRUHUSIWA KUREJESHA MAKAZI YAO BAADA YA MITA 23. MWAKA 1975 SERIKALI YA NYERERE IKIJUA KUWA HIFADHI YA BARABARA YA MOROGORO NI MITA 22.85 ILIZOLIPA FIDIA ILIWAHAMISHIA WATU KATIKA VIJIJI VYA KIMARA,MBEZI, KIBAMBA NA KILUVYA NA KUWAGAWIA ARDHI TOKA MITA 22.85 TOKA KATIKATI YA BARABARA. BAADHI YA WALIOGAWIA ARDHI HIZO ZILIPIMWA NA SERIKALI NA IKAWAPATIA HATI MILIKI AMBAZO WANAZILIPIA HADI LEO. HIVYO TUACHE USHABIKI
OK may be but I do doubt, kama Kuna malipo yatafanyika tena!! Sijui!!!Mkuu:
Fidia unayo zungumzia ni hadi mita 30 tu kutoka katikati ya Barabara kuu zaidi ya hapo hakuna fidia yeyote iliyo lipwa.