Bomoa Bomoa ya TANROADS Morogoro Road Dar Es Salaam

Bomoa Bomoa ya TANROADS Morogoro Road Dar Es Salaam

Kwanza tuna wabunge wapumbavu sana. Tunahitaji mita 120 za nini? Hasara tunayowapa wananchi ni kubwa mara mia kuliko kujenga ring roads.tujenge ring roads.
 
Umeongea vizuri ulichoharibu ni kutumia neno inasekana
 
Lakini nakumbuka wote waliojenga barabara ya Morogoro road walilipwa miaka mingi iliyopita fidia yao.

Hao wanaodai sasa wamejenga baada ya malipo kufanyika na ramani ipo mamlaka husika kwa ushahidi.

Uwezekano wa kulipwa fidia unaweza kuwa mdogo sana kwa wenye nyumba unless otherwise
Je ni lini malipo haya yalifanywa? ni watu wangapi walilipwa? je walipaswa kuhamia wapi? je kuna orodha ya waliolipwa na uthibitisho wa malipo hayo?

Je walifanyiwa fidia walikuwa wamejenga upande gani wa barabara ya Morogoro? kabla ya kufika ubungo au baada ya kupita ubungo?

Mchakato, mkakati na mpango wa kujenga/kupanua barabara ya Morogoro ulianza lini na unapangwa umalizike lini?
 
Umeongea vizuri ulichoharibu ni kutumia neno inasekana
Mwandishi makini huweza kutumia neno inasemekana kwa jambo ambalo halina uthibitisho kamili na ushahidi wa kutosha. Nimetumia inasemekana katika vipengele viwilii au vitatu ili kuruhusu wenye uhakika wa kilichosemwa wakilete kama ushahidi na isiwe ni habari isiyo rasmi na ya mtaani.

Rejea kanuni za uandishi.
 
Juzi jamaa yangu nyumba zake zilibomolewa hapo hapo Kibamba. Alikuwa amepata NSSF yake akaamua awe mjasiriamali kwa kuanzisha biashara. Zote zilifyekwa.

WaTanzania tuna asili ya ku-ignore sheria especially pale ambapo hazitekelezwi (nakumbuka jamaa yangu nilimwambia kabisa..Mkuu hebu angalia sheria inasemaje kuweka hela yako ya maana sehemu kama hii-it might be road reserve. Alichonijibu ni kwamba..mipango ya serikali ni ya mda mrefu kwa hiyo barabara watajenga ila siyo leo wala kesho). The rest is history.

Mfano DSM watu wenye hela zao na influence..wamejenga almost baharini kabisa. na vibali (vingi vya figisu) wanavyo. Lakini sheria za kimataifa na za Tanzania ziko wazi. Ufukwe wa Bahari mpaka sehemu ya ujenzi/maendeleo ni mita 60! Sasa kama wengi tunavyojua wanaoishi baharini ni wenye nazo. Lakini kesho Magufuli au mwingine akiamka akasema wote walio ndani ya mita 60 wabomoe nyumba zao..utaona vilio na kudai fidia. Lakini hiyo sheria iko kwenye vitabu miaka na miaka. Ni mambo mengi ambayo tunafanya bila kuzingatia sheria. Refer: Mama Lwakatare kujenga baharini Mbezi beach , Matias Manga wa Arusha kujenga Hotel ya Kimataifa barabarani nk sehemu ambazo haziruhusiwi. Lakini kwa vile tunaweza kuwahonga wanaotoa vibali we do it knowing kwamba hatutasumbuliwa.

Serikali ina mapungufu yake na sometimes inatumia ubabe. Lakini lazima tujue DSM ya leo siyo dsm ya miaka 50 au 100 ijayo. Lazima tupange mipango tukifikiria vizazi na vizazi vijavyo. Imagine mtu aliye-plan mita 60 miaka hiyo DSM haina hata wakazi laki tano! But they did that with an eye on the future. waliopanga leo hawapo. na wala hata huo uwezo wa kujenga barabara hawakuwa nao kipindi hicho.

In all: Katika nchi yoyote ukitaka kuishi vizuri na salama, jifunze kuheshimu na kufuata sheria. Utafanikiwa. WaTanzania wengi hatuheshimu sheria ndo maana mambo yetu yanakwenda hovyo hovyo. Kila kitu tunaweka siasa au kutaka huruma za hiyo hiyo sheria!
 
Lakini nakumbuka wote waliojenga barabara ya Morogoro road walilipwa miaka mingi iliyopita fidia yao.

Hao wanaodai sasa wamejenga baada ya malipo kufanyika na ramani ipo mamlaka husika kwa ushahidi.

Uwezekano wa kulipwa fidia unaweza kuwa mdogo sana kwa wenye nyumba unless otherwise
Walijenga serikali ikiwa wapi?
 
sheria ipo wazi na hata kwenye hiyo kesi serikari ilishinda ,hata rufaa iliyo katwa ,serikali ilishinda.Ila kuna watu wamewauzia wajinga barabarani.na waowakanunua.

Msidanganywealama za roadi reserve ziko morogoro road tangu enzi za mkoloni,alama zikp,ilikuwa miti na becon ziko morogororad yote .Ila watu wamezizarau na kujenga ndani yake.
Nasisitiza alama ziko mimi nimeziona miti na becon watu wamevamia makusudi.
 
Walijenga serikali ikiwa wapi?

Mkuu hapa ndo tunakosea. Sheria ipo ifuatwe.

Serikali haina wajibu wa kukukataza wewe kujenga au kutojenga. Ni jukumu lako kujiridhisha kama sheria husika imefuatwa. Huwezi ukajenga ..halafu kesho unauliza eti serikali ilikuwa wapi kipindi najenga. It is your fault. Na nimeona wengi wakiumia kwa approach hii.

Kawa wasemavyo wanasheria. Ignorance of the law is no defence.
 
Juzi jamaa yangu nyumba zake zilibomolewa hapo hapo Kibamba. Alikuwa amepata NSSF yake akaamua awe mjasiriamali kwa kuanzisha biashara. Zote zilifyekwa.

WaTanzania tuna asili ya ku-ignore sheria especially pale ambapo hazitekelezwi (nakumbuka jamaa yangu nilimwambia kabisa..Mkuu hebu angalia sheria inasemaje kuweka hela yako ya maana sehemu kama hii-it might be road reserve. Alichonijibu ni kwamba..mipango ya serikali ni ya mda mrefu kwa hiyo barabara watajenga ila siyo leo wala kesho). The rest is history.

Mfano DSM watu wenye hela zao na influence..wamejenga almost baharini kabisa. na vibali (vingi vya figisu) wanavyo. Lakini sheria za kimataifa na za Tanzania ziko wazi. Ufukwe wa Bahari mpaka sehemu ya ujenzi/maendeleo ni mita 60! Sasa kama wengi tunavyojua wanaoishi baharini ni wenye nazo. Lakini kesho Magufuli au mwingine akiamka akasema wote walio ndani ya mita 60 wabomoe nyumba zao..utaona vilio na kudai fidia. Lakini hiyo sheria iko kwenye vitabu miaka na miaka. Ni mambo mengi ambayo tunafanya bila kuzingatia sheria. Refer: Mama Lwakatare kujenga baharini Mbezi beach , Matias Manga wa Arusha kujenga Hotel ya Kimataifa barabarani nk sehemu ambazo haziruhusiwi. Lakini kwa vile tunaweza kuwahonga wanaotoa vibali we do it knowing kwamba hatutasumbuliwa.

Serikali ina mapungufu yake na sometimes inatumia ubabe. Lakini lazima tujue DSM ya leo siyo dsm ya miaka 50 au 100 ijayo. Lazima tupange mipango tukifikiria vizazi na vizazi vijavyo. Imagine mtu aliye-plan mita 60 miaka hiyo DSM haina hata wakazi laki tano! But they did that with an eye on the future. waliopanga leo hawapo. na wala hata huo uwezo wa kujenga barabara hawakuwa nao kipindi hicho.

In all: Katika nchi yoyote ukitaka kuishi vizuri na salama, jifunze kuheshimu na kufuata sheria. Utafanikiwa. WaTanzania wengi hatuheshimu sheria ndo maana mambo yetu yanakwenda hovyo hovyo. Kila kitu tunaweka siasa au kutaka huruma za hiyo hiyo sheria!

Ngosha,

Naafiki kuna waliomo na wasiokuwemo. Hapa lazima Serikali itumie haki,busara na utu kufanya uamuzi wake ili kila mtu apate haki yake anayostahili.

Wale ambao walilipwa fidia wakazinywa na wakabakia watambuliwe na iwe ni shauri yao kupata fidia. Wapewe muda muafaka wenye utu kuhama.

Wale ambao hawakulipwa fidia, lakini mali zao zisizohamishika ziko kwenye maeneo yaliyopimwa na wizara ya ardhi katika ramani zake za mipango miji, wapewe haki yao ya fidia pamoja na kupewa maeneo mapya ya kuhama,nao wapewe muda muafaka wa kuhama.

Wale ambao walivamia maeneo,hawana hati walaaina yeyote ya utambulisho kuwa walipewa ardhi na ikasajiliwa na kijiji, wizara, nao wapewe muda muafaka kuhakikisha wanahama.

Muda muafaka kwa makundi yote haya matatu uwe walau miezi 18-24, ili watu waweze kupata mahali papya pa kuweka makazi mapya.
 
Ila tu niseme kwamba kuna roho za uharibifu zimetajwa mpaka kwenye misahafu, hili ni pepo baya sana ....daima halitengenezi bali linaharibu na likitengeneza kitu hakitakosa kuwa na walakini mkubwa.... Hiyo ndio roho ya uharibifu ilivyo
Tunahitaji kuwa na barabara pana eneo husika Lakini hekima na utu vitawale watu walipwe fidia waondoke kwa amani ubabe hautatufikisha popote

Mtu avunje Sheria mwenyewe halafu alipwe fidia? Kwa nini hiyo Misaafu yenu sijui Biblia unayoinukuu inasema mhalifu akatwe mkono mmoja akirudia akatwe na wa pili? Kwa nini Msaafu wako haujasema alipwe fidia?

Haya mambo ya huo mnaouita utu wa kinafiki ndiyo yaliyotufikisha hapa, hakuna jamii ya kijinga na kipuuzi kama yetu, Sheria ziko wazi mna upuuzia hlf mkishikwa mnaleta sijui mambo ya utu, kama mnajifanya mna huo utu sana kwa nini msitii Sheria zetu?
 
Mkuu nakubaliana na wewe ila umekuwa mkali sana.....hahahaha
 
Na ya Tabata Relini hadi Kinyerezi ijengwe kama ilivyo kwenye Master Plan twende kwa pamoja!
Wabomowe tu.mji umekuwa mkubwa.nilikwenda mbezi ya kimara asubuhi.hyo foleni sasaaa.bora bagamoyo road kuna 2 way mpaka tegeta.kule 1 way.hatari
 
Sheria bila utu ni unyapara!

Gamba,

Umezungumzia kitu kikubwa sana ambacho ni dhahiri ni kigumu ama kwa makusudi au upeo na uelewa finyu katika jamii yetu ambapo Utu na Haki vinaonekana kuwa ni vya watawala pekee.

Ukipima ukali wa kauli, mchemko na hata ueleko wa hasira na kubeza "bomoa, wacha wapigwe" unajiuliza je tunapojisifia kuwa ni nchi yenye amani, utulivu na mshikamano ni kweli au imebakia kuwa kauli isiyo na maana?

Wengi hawajui na hawataki hata kukubali na kuthamini kuwa hata mkiukaji wa sheria ana haki zake na utu wake uko pale pale.

Labda ukweli wa dhamiri zetu unaonekana pale yoe la "mwizi" linapopigwa na watu kuhamaki bila kujali thamani ya uhai au fursa ya kujitetea na kuponda mtu mawe ama kumchoma moto kisa mtu kapiga yoe "mwizi"

Wasio na busara wala hekima kamwe hawataelewa ulichosema kuwa "Sheria bila Utu ni unyapara" kwao hukumu yao imejaa ukatili na wala si haki ya kuhitimisha shauri kwa amani na maelewano.
 
Bomoa Bomoa ya makazi, nyumba, majengo na mali Morogoro Road Kuanzia Ubungo mpaka Kiluvia.

Leo mbunge wa Kibamba John Mnyika alikuwa na mkutano na wananchi wa jimbo lake kuhusiana na barua zilizosambazwa hivi siku 10 zilizopita kwa wakazi wa maeneo kutoka Kimara Mjini mpaka Kiluvia na TanRoads na alama za kutaka nyumba, majengo na mali kubomolewa kwa kuwa zinasemekana ziko kwenye hfadhi ya barabara ya Taifa.

Barua hizi zimetolewa na TanRoads MKoa wa Dar Es Salaam na mazungumzo ya watu yamechukua mkondo usio makini na kulifanya hili ni jambo la kisiasa.

Wengi wanaongea bila kujua undani wa jambi hili na zaidi ni ushabiki usio na mantiki.

1. Miaka ya 70,80,90 Serikali iligawa maeneo along Barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo a kuendelea hadi Kiluvia kutokana na wananchi waliopoteza makazi maeneo kadhaa ya jiji na hata kusaidia kupanuka kwa jiji.

2. Asilima kubwa 75% ya waliojenga nyumba, majengo ni halali na hata kwenye ramani za mipango miji za wizara ya ardhi, hizo nyumba na maeneo hayako kwenye Road Reserve.

3. Kwa mujibu wa wizara ya ardhi, eneo qualifying kuwa road reserve ni kati ya mita 30 hadi 60 kutoka katikati ya barabara. hii pia iko katika sheria zilizotumika na kuendelea kutumika kuhusu maeneo.

4. TanRoads (iliyoanzishwa 2000s) inadai kuwa road reserves ni mita 120 kutoka katikati ya barabara ambayo nikutokana nasheria ya barabara ya mwaka 1926/27.

5. Marekebisho kadhaa ya sheria ya barabara yameshafanyika tangu tupate uhuru na ndio maana Wizara ya ardhi, manispaa wanatumia sheria mpya na kuhusisha maeneo katika mipango miji.

6. Barabara ya Morogoro,eneo la Ubungo mpaka KImara mjini, TanRoads imetumia upana wa mita 30 na wakati wa kujenga mwendo kasi ikapanua mpaka mita 45 kutoka katikati ya barabara. Maeneo kutoka KIbaha kuelekea Chalinze, Tanroads inatumia sheria ya sasa ya mita 30 kutoka katikati ya barabara kila upande.

7. Bomoabomoa inayozungumziwa leo ni kutoka KImara Mjini/StopOver mpaka Kiluvia na TanRoads wanadai eneo la mita 120 kutoka katikati ya barabara (pande zote mita 120!)

8. Shauri hili lilishapelekwa mahakamani miaka iliyopita na TanRoads ilishindwa kesi. Hata wakati Waziri wa Ujenzi kati ya mwaka 2000 -2015 alipojaribu kung'ang'ania sheria ya mwaka 1927, si mahakama pekee, bali hata sheria za barabara na baraza la Mawaziri liliafiki kuwa ukubwa wa mwisho ni mita 60 kutoka katikati ya barabara kwa pande zote (jumla upana mzima mita 120). Hili linahitaji uchambuzi wa zaidi pamoja na kumbukumbu husika kuthibitisha hivyo.

9. Inasemekana kuwa miaka ya mwisho ya 90, kwenye mpango wa upanuzi wa barabara hii, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (WB/IMF) waliipa Serikali fedha za fidia kwa watakaolazimika kuhama maeneo yatakayo bomolewa kwa kufanya tathmini ya nyumba, majengo na mali zilizoko kwenye eneo litakaloathirika. Mpaka sasa hakuna mkazi ambaye imethibitika alipatiwa kiwanja kipya cha kuhama na kupewa fidia mali yake kubomolewa na hakuna kumbukumbiu kuonyesha malipo haya yalifanyika vipi.

10. Bomoabomoa ya sasa inafanywa na TanRoads mkoa wa Dar. Inasemekana ngazi zote zilizoulizwa(mawaziri Tamisemi,Ardhi,Ujenzi,TanRoads na hata Waziri Mkuu)kila mmoja inarusha mpira kwa mwenzake na vidole vinaelekezwa mamlaka ya juu ya Mkoa na Nchi.

11. Serikali kutokana na kauli inayosemekana ni ya Rais, inasema haitatoa fidia wala kutoa maeneo mapya kwa waathirika(inabidi kuthibitishwa kama ni kweli).

12. Barabara kuu ya kuingia Dar, imebadilishwa katika mipango ya barabara kuu na kuhamia upande wa Daraja la Kigamboni na highway kuu mpya imeshaanza kukwanguliwa miaka kadhaa iliyopita na itapita pembeni ya mji mpaka Ruvu au Chalinze kwenye maeneo ambayo yako wazi na hayana watu na gharama ni nafuu ukizingatia hakutakuwa na haja ya kubomoa au kutoa fidia kwa watu watakaoathirika kwa kiwango cha kutoka Ubungo pale Sam Nujoma na Morogoro road zinapokutana mpaka Ruvu.

13. Inasemekana mpango wa kupanua barabara hii kutoka Ubungo uko hati hati kutokanana kukosekana kwa fedha na kipaumbele kupelekwa maeneo mengine ya nchi yananayohitaji upanuzi wa barabara, fedha na kipaumbele kuwekwa barabara ya kutoka daraja la kigamboni, fly over za Tazara na Ubungo, Daraja jipya kutoka Aga Khan mpaka Coco Beach, Bandari ya Bagamoyo, Reli mpya na miradi mingine ya miundo mbinu nchini. Mradi unasemekana umesimama kwa kati ya miaka mitano hadi saba na hivyo kuweza kutoa fursa njema kwa mipango inayoeleweka kufanyika ikiwa na kuwapa wakazi watakaoathirika maeneo mapya ya kuhamia na fidia.

Kwa kutazamo hayo mambo 13 niliyataja hapo juu, ni wazi kuna ulazima wa jambo hili kufanywa kwa umakini, haki na kuthamini utu na si kufanyiwa upambe na ushabiki wa kisiasa.

Tafakari ni waathirika wangapi na kiasi gani kitatumika kutoa fidia au hata kufanya zoezi la ubomoaji.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi,
Na zidumu Fikra sahihi za Mwenyekiti wa Chama na ambae ni Rais
By the way Long time No See kaka, ulikua wapi??
Nimemkumbuka na rafiki yangu rev Massanilo
 
Back
Top Bottom