Bombardier Q400 yapata hitilafu Mwanza

Bombardier Q400 yapata hitilafu Mwanza

Zinazidiwa na magari mpya yanakaa muda bila kuharibika
 
Dah,,,, watu wengine wa ajabu sana,,,, hivi hizi ndege si zimenunuliwa kwa hela za walipa kodi wa Tanzania? Sasa kinachokufanya ushabikie hitilafu ni nini? Badala ya kisikitika kuwa kodi zetu zinaenda kutumika kufanyia marekebisho,,, wewe unafurahia eti,, tulijua tu,,,,, mmmh! Mungu iponye Tanzanaia

Mbona unajushtukia? Wapi kafurahia?
 
Mkuu ni pesa zetu lazima iwe nongwa au ww hauna machungu?Kwanza imenunuliwa sh,ngapi hatujui kitu kipya mizinguo kila uchao siku itakapowafanya kitu mbaya wapendwa wetu ndo mtazibuka maskio!
 
View attachment 466077

Zaidi ya abiria 70 wa ndege ya Bombadier Q dash 400,waliokuwa wakisafiri kutoka jijini Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam jana majira ya saa moja usiku,wameshindwa kusafiri kwa kutumia ndege hiyo kutokana na kupata hitilafu kwenye moja ya injini zake.

Kaimu Meneja wa uwanja wa ndege Mwanza David Matovolwa amesema kutokana na ndege hiyo yenye namba za usajili 5H TCB, kupata hitilafu ikiwa inataka kunyanyuka kwenye barabara ya kutulia na kurukia ndege ( runway ), ilibidi abiria kubadilishiwa ndege iliyotoka Dar es salaam ambapo waliweza kuondoka majira ya saa saba kasorobo usiku huo huo.

Akithibitisha ndege hiyo kupata hitilafu, Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la ndege Tanzania ( ATCL ), Mhandisi Emmanuel Koroso ameiambia ITV kwa njia ya simu kwamba ndege hiyo imeondoka uwanja hapo hii leo majira ya saa 4.30 asubuhi kuelekea jijini Dar es salaam ikiwa haina abiria baada ya mafundi kuifanyia matengenezo ya awali.

Shirika la ndege Tanzania lilizindua rasmi safari za ndege zake aina ya Bombadier Q dashi 400 kati ya Dar es Salaam na Mwanza Oktoba mwaka jana, ambapo ndege hiyo iliwasili mwanza kwa mara ya kwanza saa 10.45 jioni ikiwa Katibu mkuu wa Wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Leonard Chamriho na kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.


Chanzo: ITV
Au Yale maji wakati zinaingia itakuwa yalijaa ndani ya engen,Maana umwagiliaji sijauelewaelewa.
 
Wabadilishe yule Twiga na Wamuweke Faru John.

Twiga ameonekana kushindwa kwenye kila Shirika.

Tanesco, Twiga Cement n.k

Hata kwenye pesa yetu ndio maana Uchumi haukui.

Sio mnyama wa maendeleo na bahati.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] you made my day comrade!
 
Baadhi ya Watz mnasikitisha sana. Suala la ndege kupata matatizo ya kiufundi ni kitu cha kawaida haijalishi ni pangaboi au jet. Fastjet leo ni siku ya tatu ndo safari zake za kuja Mwanza kwa ndege yao ya usiku ndo zmerudi kwenye ratiba zake za kawaida. Kabla ya hizi siku ndege zao zilipata hitilafu kwa kupokezana ndani ya siku moja. Labda kwakuwa mlio wengi humu mnapita airports wakati wa safari tu. Kwahiyo siku unapopita ukakuta ndege imepata hitilafu kwa siku hiyo,basi mnapiga kelele ndege mbovu eti za ATCL tu !!! Kwanini isiwe Fastjet au Precision Air ambazo nazo zimekuwa zikiharibika tena mara nyingi zaidi kuliko hata ATCL. Naona hizi ni chuki juu ya Magufuri baada ya kuziba na kuvuruga mitandao ya wizi wa pesa za serikali. Tuwe waungwana hata jambo zuri akilitenda adui yako,lipokee kwa mtazamo chanya. Upinzani sio kupinga kila linalotendwa na mpinzani wako,bali ni kujenga hoja. Mnapaswa kumpongeza mh rais kwan baada ya kuja ATCL unyanyasaji uliokuwa unafanywa na Fastjet walau umepungua kidogo japo bado upo,lkn kuna usafiri mbadala walau mtu anaweza kubadilisha ndege kuliko ilivyokuwa awali. Tuwe wazalendo kwa kuvipenda na kuvithamini vyetu ili kuvipa uwezo wa kutia huduma bora zaidi. Nilikuwa napita tuu maana nimewasikia baadhi mmekariri ule ubeti wa viongozi wenu kuwa Rais kanunua ndege mbovu,kitu ambacho ni tungo za wanasiasa wetu tuu.
 
Dah,kazi ipo awamu hii,au itakuwa wafanyakazi wamecheleweshewa mishahara yao,kwani kila hitilafu huwaga ni mwishoni mwa mwezi tu
 
siku hii ndege ikipotea angani au kuanguka kuna wajinga watachinja kuku na kupika pilau...
Huenda ila kuna haja ya kuzichunguzabkwa ukaribu isijekuwa kuna hujuma ama hazifanyiwi periodic maintanance si unajua kibongobongo?[emoji4] [emoji4]
 
Umesahau tz hakuna kisichowezekana, hapa utakutana watu wanaojua kubadilisha matumizi ya kitu lengo lao litimie.
That is not my concern..the key issue here is why are we not ready to accept the truth that Bombardier Q400 ni kimeo? Hizi ni ndege zinazotengenezwa special for irrigation purpose and not kubeba abiria.
 
Kama nawaona Bawacha na Ukawa wanavyo fanya sherehe.
Wakati hitilafu kwenye vyombo vya moto ni kawaida...ingeanguka wangechinja ng'ombe wale, wanywe, wafurahi walivyo na roho mbaya zenye kutu na kinyongo
 
Msidharau vyenu jamani. Hitilafu ya ndege ni kitu cha kawaida kabisa. Tatizo hizi zetu watu wamezikamia utadhani ni miraa. Mbona mataifa mengine walianza nazo na leo wapo mbali?? Sema, asingenunua aina moja zoote kwa mara moja. Angeleta pole pole yaani moja moja tukizoelea
 
Kama nawaona Bawacha na Ukawa wanavyo fanya sherehe.
Sijawahi kusikia kuwa fastjet imepata hitilafu ,yaani vyombo vya habari kama ITV ikitokea tatizo kwenye Atcl lazima walipot sijui Huwa Wana lengo Gani ,any way hii ndio nchi yetu watu hawapendivyetu.
 
Kila siku yenyewe ni hitilafu tuuuu bora nitembee kwa miguu tu
Unafikiri kwanin mbowe asipo lipa Kodi inakuwa big story ??? hata hao wengine hawalipi lkn ,vyombo vya habari vipo kimya ...
 
Back
Top Bottom