Bombardier Q400 yapata hitilafu Mwanza

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
FB_IMG_1485953051967.jpg


Zaidi ya abiria 70 wa ndege ya Bombadier Q dash 400,waliokuwa wakisafiri kutoka jijini Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam jana majira ya saa moja usiku,wameshindwa kusafiri kwa kutumia ndege hiyo kutokana na kupata hitilafu kwenye moja ya injini zake.

Kaimu Meneja wa uwanja wa ndege Mwanza David Matovolwa amesema kutokana na ndege hiyo yenye namba za usajili 5H TCB, kupata hitilafu ikiwa inataka kunyanyuka kwenye barabara ya kutulia na kurukia ndege ( runway ), ilibidi abiria kubadilishiwa ndege iliyotoka Dar es salaam ambapo waliweza kuondoka majira ya saa saba kasorobo usiku huo huo.

Akithibitisha ndege hiyo kupata hitilafu, Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la ndege Tanzania ( ATCL ), Mhandisi Emmanuel Koroso ameiambia ITV kwa njia ya simu kwamba ndege hiyo imeondoka uwanja hapo hii leo majira ya saa 4.30 asubuhi kuelekea jijini Dar es salaam ikiwa haina abiria baada ya mafundi kuifanyia matengenezo ya awali.

Shirika la ndege Tanzania lilizindua rasmi safari za ndege zake aina ya Bombadier Q dashi 400 kati ya Dar es Salaam na Mwanza Oktoba mwaka jana, ambapo ndege hiyo iliwasili mwanza kwa mara ya kwanza saa 10.45 jioni ikiwa Katibu mkuu wa Wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Leonard Chamriho na kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.


Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom