Bomba la mafuta Tanga - Hoima EACOP ni salama kwa mazingira

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Samwel Gwamaka amesema tayari ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kati ya Hoima Uganda na Chongoleani Tanga umeanza kwa hatua za awali kwa maeneo ya kipaumbele na NEMC inafuatilia kwa karibu mradi huo na imeridhishwa na mwenendo wa mradi husika kimazingira. Hakuna athari zozote za mazingira zilizoainishwa katika tathmini ya mazingira kwenye mradi wa ujenzi huo.


Novemba 29 mradi wa Bomba la mafuta ghafi ulipatiwa cheti cha mazingira na Waziri aliyekuwa na dhamana ya mazingira kipindi hicho hivyo mradi umefuata sheria na kanuni zote zinazohusu mazingira katika uwekezaji na ndiyo maana ukaruhusiwa kujengwa. Mradi huu ulisajiliwa Machi 2017 na NEMC na waliofanya usajili ni Total Energy na baraza lilihakiki andiko la tathmini na kujiridhisha nalo na tathmini hiyo ilihusisha wadau wote wakiwemo wananchi na taasisi linakopita bomba la mafuta ghafi.

1652709820070.png
 
Back
Top Bottom