Unaweza kuweka huo mgawanyo wa ajira na ujira alkadhalika manufaa baada ya ujenzi kukamilika??
Je, wanaopisha maeneo ya mradi wamekuwa equally/fairly compensated??
Victims walishalipwa kitambo .....mgawanyo kwa sasa vigumu ila pata picha kila stations 120 along the way to 100km apart ....kuna camp vibarua wote wata move 50km hadi wanakutana kazi kuwapikia maji huduma zote jammii na kulala hapo kambini magari drivers walinzi mafundi ...etc service providers wengine watakuwepo pia ....waendesha mitambo na full Wi-Fi solutions zitakuwepo na watajenga nyumba za wasimamizi na walinzi bomba......mafundi ujenzi etc.....
 
Unauhakika hao victims wamelipwa?? Una uhakika hao "vibarua" walipwa?

Alafu mradi huo huoni kuwa una madhara mengi zaidi ya faida... Climatr change... price of crude oil, etc
 
BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI (EACOP)

✍🏻 Huu ni mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani mkoani Tanga nchini Tanzania. Mradi huu una urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo nchini Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.

Bomba linapita katika mikoa nane ya Tanzania Bara ambayo ni;

1.Kagera (Bukoba Vijijini, Muleba na Biharamulo);
2.Geita (Chato, Geita, Bukombe na Mbogwe);
3.Shinyanga (Kahama Mjini);
4.Tabora (Nzega Vijijini, Nzega Mjini na Igunga);
5.Singida (Iramba, Mkalama na Singida Mjini);
6.Dodoma (Kondoa na Chemba);
7.Manyara (Hanang na Kiteto) na
8.Tanga (Kilindi, Handeni Mji, Handeni Vijijini, Korogwe, Muheza na Tanga Mji).

✍🏻 Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.

✍🏻 Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili litajengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

✍🏻 Mradi umetoa ajira 200 kwa watanzania katika kazi za awali. Vilevile kampuni 100 za kitanzania zimepata kazi katika kipindi hiki. Watanzania wame elimishwa kuhusu mradi huu na manufaa yake. Zaidi ya wafanyabiashara 2000 wamepitishwa kwenye fursa zilizopo kwenye mradi. Watanzania wanaozunguka eneo la mradi kutoka wilaya nane (8) wamehamasishwa pamoja na serikali za mitaa.

#AlipoMamaVijanaTupo
#KaziIendelee

View attachment 2118527

View attachment 2118528

View attachment 2118529

View attachment 2118530

View attachment 2118531

View attachment 2118532
Hivi uvccm wanahusikaje hapo?Mradi wa Waganda huo na sisi Watanzania kazi yetu kwa hii project ni kukubali lipite kwenye ardhi yetu.Haijalishi rais wetu ni nani,Waganda wakijenga bomba sawa na wasipojenga hatuna tunachokosa.
Mwambieni Mama Samia aruhusu Katiba mpya,miradi iliyopo inatosha kwa sasa.Hilo tu ndiyo linaloweza kumpa Legacy na siyo kukimbizana na miradi ya kampeni za waliopita.
 
Victims walishalipwa kitambo .....mgawanyo kwa sasa vigumu ila pata picha kila stations 120 along the way to 100km apart ....kuna camp vibarua wote wata move 50km hadi wanakutana kazi kuwapikia maji huduma zote jammii na kulala hapo kambini magari drivers walinzi mafundi ...etc service providers wengine watakuwepo pia ....waendesha mitambo na full Wi-Fi solutions zitakuwepo na watajenga nyumba za wasimamizi na walinzi bomba......mafundi ujenzi etc.....
Ujenzi ushaanza mkuu?
 
Unauhakika hao victims wamelipwa?? Una uhakika hao "vibarua" walipwa?

Alafu mradi huo huoni kuwa una madhara mengi zaidi ya faida... Climatr change... price of crude oil, etc
Ooohhh basi uzuie mkuu lisijengwe
 
Tuchangamkie fursa
IMG-20220315-WA0011.jpg
 
Wananchi walionufaika wako wapi au unasema watakaonufaika?? Niko kandokando mwa mradisijaona kitu.
Ubabaishaji mwingi EACOP wanahubiri mradi kunufaisha waguswa wakati miradi na tender zikidakwa juu kwa juu na wajanja wa Dar hakuna cha local content wala nini, kuhusu local content inabidi EACOP na TPDC mjitafakari, mnachojaribu kufanya sicho, kuweni wazalendo hii nchi ni yetu sote.
 
Ishu siyo mimi kuuzuia... Najaribu tu kukuonesha ujue athari endelevu za huo mradi
Kwa maendeleo nchi zetu changa .....kodi itatusukuma athari ndogo ndogo si mbaya sana....kumbuka lipo la Zambia zaidi 30yrs ....sio la kwanza hili
 
BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI (EACOP)

✍🏻 Huu ni mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani mkoani Tanga nchini Tanzania. Mradi huu una urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo nchini Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.

Bomba linapita katika mikoa nane ya Tanzania Bara ambayo ni;

1.Kagera (Bukoba Vijijini, Muleba na Biharamulo);
2.Geita (Chato, Geita, Bukombe na Mbogwe);
3.Shinyanga (Kahama Mjini);
4.Tabora (Nzega Vijijini, Nzega Mjini na Igunga);
5.Singida (Iramba, Mkalama na Singida Mjini);
6.Dodoma (Kondoa na Chemba);
7.Manyara (Hanang na Kiteto) na
8.Tanga (Kilindi, Handeni Mji, Handeni Vijijini, Korogwe, Muheza na Tanga Mji).

✍🏻 Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.

✍🏻 Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili litajengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

✍🏻 Mradi umetoa ajira 200 kwa watanzania katika kazi za awali. Vilevile kampuni 100 za kitanzania zimepata kazi katika kipindi hiki. Watanzania wame elimishwa kuhusu mradi huu na manufaa yake. Zaidi ya wafanyabiashara 2000 wamepitishwa kwenye fursa zilizopo kwenye mradi. Watanzania wanaozunguka eneo la mradi kutoka wilaya nane (8) wamehamasishwa pamoja na serikali za mitaa.

#AlipoMamaVijanaTupo
#KaziIendelee

View attachment 2118527

View attachment 2118528

View attachment 2118529

View attachment 2118530

View attachment 2118531

View attachment 2118532
We Mataga/Chawa kwani hujui kuwa tunabomba la mafuta linaitwa TAZAMA? au unajitoa akili ? Waulize wananchi waliopitiwa na Hilo bomba la TAZAMA Hali zao za kiuchumi zikoje?
Sisi ni watu wazima danganya watoto wenzio.

20211006_082859.jpg
 
Back
Top Bottom