Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,890
- 939
BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI (EACOP)
✍🏻 Huu ni mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani mkoani Tanga nchini Tanzania. Mradi huu una urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo nchini Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.
Bomba linapita katika mikoa nane ya Tanzania Bara ambayo ni;
1.Kagera (Bukoba Vijijini, Muleba na Biharamulo);
2.Geita (Chato, Geita, Bukombe na Mbogwe);
3.Shinyanga (Kahama Mjini);
4.Tabora (Nzega Vijijini, Nzega Mjini na Igunga);
5.Singida (Iramba, Mkalama na Singida Mjini);
6.Dodoma (Kondoa na Chemba);
7.Manyara (Hanang na Kiteto) na
8.Tanga (Kilindi, Handeni Mji, Handeni Vijijini, Korogwe, Muheza na Tanga Mji).
✍🏻 Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.
✍🏻 Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili litajengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
✍🏻 Mradi umetoa ajira 200 kwa watanzania katika kazi za awali. Vilevile kampuni 100 za kitanzania zimepata kazi katika kipindi hiki. Watanzania wame elimishwa kuhusu mradi huu na manufaa yake. Zaidi ya wafanyabiashara 2000 wamepitishwa kwenye fursa zilizopo kwenye mradi. Watanzania wanaozunguka eneo la mradi kutoka wilaya nane (8) wamehamasishwa pamoja na serikali za mitaa.
#AlipoMamaVijanaTupo
#KaziIendelee