Bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam limepasuka Somanga

Barca

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,108
2,000
Habari ya muda hii. Bomba la gesi limepasuka maeneo ya somanga taharuki imetanda maeneo haya. Vyombo vya ulinzi na usalama kama kawaida hawatoi elimu kwa wananchi wapo tu wamezagaa hovyo. Tanzania hatujifunzi kabisa kuepuka majanga. Magari yote yanayotoka Dar es Salaam na kwenda Dar es Salaam hayapiti.

Inasemekana right moto ungeweka ungeweza unguza wilaya yote y kilwa. Nimeshangaa sana kwa kweli.

=====

UPDATES:

“TANESCO linawataarifu wateja wake kuwa saa 11:20 jioni leo imetokea hitilafu kwenye "valve" na kusababisha kuvuja kwa gesi kwenye kituo cha Somanga Rufiji Mkoani Pwani, hitilafu imetokea wakati Songas wakiendelea na matengenezo kinga kwenye bomba la gesi la Songosongo”- TANESCO.

Taarifa zaidi....

Mamia ya Wasafiri wamekwama kwa saa zaidi ya 3 karibu na eneo la kati ya Songas na Banduka, Wilaya ya Kilwa Lindi baada ya bomba la gesi kwenye mitambo ya umeme kudaiwa kupasuka, Polisi wamezuia magari na vyombo vingine vya moto kupita eneo hilo ili kuepusha madhara.

Gesi hiyo inavuja kwenye kituo hicho kinachomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivyo kuwashawishi walinzi wa kituo jirani cha kupokea gesi kutoka Madimba Mtwara na Songosongo kilicho chini ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kusaidia kuimarisha ulinzi.

“Ni kweli kuna hitilafu kidogo. Wataalamu wetu wanashughulikia hali hiyo ila hakuna moto wala madhara yoyote kwa binadamu,” amesema Nigel Whittaker mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Songas.
 
Usangu

JF-Expert Member
May 28, 2015
827
500
Maombo yenu ni Muhimu sana kwani Mpaka sasa tumekwama katikati ya Somanga na Tingi kwani kunamlipuko mkubwa wa Gasi itakayo Songosongo. Njia imefungwa mpaka sasa na hakuna uhakika wa kupita.
 
r2ga

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,233
2,000
Asee poleni sana..Mungu awaepushie hilo balaa.ukiweza uwe unatupatia updates.
 
m2me

Member
Jul 23, 2012
55
95
hali ikoje, taaruki? Mwonekano wa moto?
Maombo yenu ni Muhimu sana kwani Mpaka sasa tumekwama katikati ya Somanga na Tingi kwani kunamlipuko mkubwa wa Gasi itakayo Songosongo. Njia imefungwa mpaka sasa na hakuna uhakika wa kupita.
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,262
2,000
Halafu utasikia watu wanakwambia tuna uranium tujenge kiwanda cha kuzalisha umeme kutumia hizo minerals, sisi waafrika tuna utani mmbaya sana.

TPDC safety kwenye gas ya uhakika inawashinda tutaiweza ya nuclear plant, halafu wanataka kujenga kiwanda cha kuuza gas karibu na hospital watailipua Muhimbili yote.
 
Bookman Oldstyle

Senior Member
Nov 3, 2019
151
225
Maombo yenu ni Muhimu sana kwani Mpaka sasa tumekwama katikati ya Somanga na Tingi kwani kunamlipuko mkubwa wa Gasi itakayo Songosongo. Njia imefungwa mpaka sasa na hakuna uhakika wa kupita.
Labda Kwa sababu "NCHI ILIYOPATA MAENDELEO FEDHA HAINA SAMANI" jamaa anamkwanja Sana atakuwa anadharau report Kwa sababu ni story "FEDHA KUINGIA KWENYE MZUNGUKO"
 
wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
2,526
2,000
Halafu utasikia watu wanakwambia tuna uranium tujenge kiwanda cha kuzalisha umeme kutumia hizo minerals, sisi waafrika tuna utani mmbaya sana.

TPDC safety gas ya uhakika inawashinda tutaiweza ya nuclear plant, halafu wanataka kujenga kiwanda cha kuuza gas karibu na hospital watailupua Muhimbili yote.
TPDC wapo vizuri asee,ukipata nafasi watembelee ujue ni namna gani wamejipanga kujikinga na hizo ajari za moto. Majanga yapo tu,mwisho tunaangalia kuyazuia,ama kupunguza madhara.
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
3,262
2,000
TPDC wapo vizuri asee,ukipata nafasi watembelee ujue ni namna gani wamejipanga kujikinga na hizo ajari za moto. Majanga yapo tu,mwisho tunaangalia kuyazuia,ama kupunguza madhara.
Hakuna anaekataa accidents do happen na saa zingine uzembe pia unahusika.

Bila ya kutoa lawama ngoja tupewe habari kamili nini kimejili huko kwanza.

Hila kitendo cha kutaka kujenga kiwanda cha kuuza gas karibu na hospitali lazima tuulizane weledi wao wa risk assessment na kama kweli wako safi kama unavyo wauza kwenye precaution measures.
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
Halafu utasikia watu wanakwambia tuna uranium tujenge kiwanda cha kuzalisha umeme kutumia hizo minerals, sisi waafrika tuna utani mmbaya sana.

TPDC safety kwenye gas ya uhakika inawashinda tutaiweza ya nuclear plant, halafu wanataka kujenga kiwanda cha kuuza gas karibu na hospital watailipua Muhimbili yote.

Nigeria anachimba Uranium..

Unaweza kuishia kwenye kuichimba na sio kuirutubisha..
 
Blandes

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
305
250
Umakini uliyopo pale kisiwa cha songosongo bado inalipuka,mungu wasimamie
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom