Bollen Ngetti: Wana CCM wenzangu hebu tujitenge na unafiki na uoga wa kijinga...

Sijui niwape jina gani, nisijeitwa na kamati kuhojiwa.

Tuna wawakilishi na watumishi hopeless ktk chi hii.

Umesikia dhamira ya AG kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu juu ya MaDED kuwa wasimamizi?? Je AG anafanya hivyo kwa maslahi ya nani au ni aibu ya kugalagazwa akiwa ndiye mshtakiwa( mlalamikiwa) kwenye kesi ile?? Anaona abu AG kushindwa hoja??

Huyo ni kada pia anaogopa ccm ikishindwa maslai yake yatakuwa shakani
 
Mleta mada sio CCM ungekuwa CCM ungekuwa na uelewa mkubwa .Huelewi katiba ya nchi inasenaje.Katiba ya nchi inasema kila mtu anastahili heshima na kuthaminiwa utu wake.Kumwita mtu taahira,msukule nk ni kumvunjia mtu heshima na utu wake .Haikubaliki na haivumiliki na Ni uvunjaji katiba na kosa kisheria

Kama sio tahira unawashwa nn
 
Kumita lofa je? au kilaza yenyewe iko sawa?
 
kuwa mbunge kupitia CCM hakumfanyi mbunge akose msimamo.
Shida ni kwamba wabunge wanatokana na vyama ambapo ili uteuliwe na chama kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM ni lazima ushinde kwenye kura za maoni katika chama na hapo ndipo kwenye shida, kama utakuwa ni mbunge unayepinga na kuikosoa sana serikali basi Chama kinakuwa na hatima yako kwa msingi kwamba serikali inaongozwa na chama husika na Raisi (mkuu wa serikali) ndiye mwenyekiti wa chama.

Hapo ndipo shida inapotokea na ndiyo maana Wabunge wengi wa CCM ni "misukule" kwani hawajitambui, ni Wabunge wachache sana wa CCM wanaojitambua na wao pia huchukua tahadhari kubwa katika kuikosoa serikali.
 
kuwa mbunge kupitia CCM hakumfanyi mbunge akose msimamo.

Mkuu ndivyo ilivyo kwamba mbunge halisi hapaswi kutokuwa na msimamo na hii ni kulingana na wajibu wake kama mbunge, lakini kumbuka mbunge ni binadamu naye anazo hisia, matamanio, maslahi,mahitaji nk, sasa inapotokea / anapoona hayo mahitaji yanaweza kuhatarishwa kwa njia yoyote hapo ndipo wajibu wa ubunge unapokoma na anakosa MSIMAMO.
 
Back
Top Bottom