Body language

mafurikoyamoto

Senior Member
Joined
Sep 13, 2013
Posts
160
Reaction score
53
Wana Jamiiforum..

Napenda kuwajulisha kuwa tunapanga kutoa course fupi on body language.

Wewe kama ni mwalimu/lecturer, mwana muziki, mfanyabiashara, mwanasiasa, au mtu awae yote ni muhimu kujua na kutafsiri ishara za maumbile ya kibinadamu.

Kwa mfano i: unafundisha darasani mara ukaona baadhi ya wanafunzi wako wamekunja mikono vifuani....wewe kama mwalimu unapata picha gani kutoka kwa wanafunzi wako?...je uendelee na somo??



Mfano ii: wewe mfanyabiashara unapatana na mteja anaetakana kununua simu lakini anakuahidi atakuja kesho kununua hiyo simu na wakati huo huo anapekecha jicho au ameshikilia sikio...unapata picha gani? je atakuja kweli?

mfano iii:

Wewe ni mwanamme upo kwenye party fulani kuna mdada ungetamani akupe company ..... unajaribu kuwa karibu nae....umekaa opposite to her......cha ajabu unakuta kakunja mguu mmoja juu ya mwingine, viganja vya mikono yake vimelekea kwako na kifua kimeinamia mbele.....je unapata picha gani?....huyu kweli atakubali kukupa company?


Je unaweza kutusaidia kujibu swali moja kati hayo hapo juu?


We can now study subconscious mind which never lie




Now if u are interested u can join us!!
 
nataka kujua kuhusu mkuu wa kaya kwenda kwenye misiba huku akitabasamu? Inatoa jibu gani??
 
nataka kujua kuhusu mkuu wa kaya kwenda kwenye misiba huku akitabasamu? Inatoa jibu gani??


........tabasamu ni ishara ya furaha.....lkn kuna tabasamu fake pia........jee wakujua kutambua tabasamu fake??? we will cover this too...
 
je utafundisha na body language ya kutongoza????

je tutaweza jua body language ya mtu muongo wakati unaongea???

kwanni usiweke hapa hapa kwenye jukwaa tukafaidi wote???
 
Mfano ii: wewe mfanyabiashara unapatana na mteja anaetakana kununua simu lakini anakuahidi atakuja kesho kununua hiyo simu na wakati huo huo anapekecha jicho au ameshikilia sikio...unapata picha gani? je atakuja kweli?




Hakuna biashara hapo
 
je utafundisha na body language ya kutongoza????

je tutaweza jua body language ya mtu muongo wakati unaongea???

kwanni usiweke hapa hapa kwenye jukwaa tukafaidi wote???

jamiiforums inajitosheleza.. hebu jongea jamii intelligence ujifunze mengi zaidi..
 
unaongea na mpenzi wako, wewe unam-face lakini yeye ana-face upande(yaani ni kama anawaangalia waliopo nyuma yako), amekunja nne, mikono ameiweka juu ya mapaja huku amevifunga vidole na hakuangalii ukiwa unaongea.. inamaanisha nini hii?
 
Nakuongezea hii

Ukiona unaongea na mtu halafu wewe kila unapoongea mwenzio anarudisha kichwa nyuma - ujue kinywa chako kinatoa
 
kwanini usisubiri wakati mipango imekamilika ndio uje utuambie?
 
Ujasiriamali mwingine ni wizi mtupu.
Kuna sehemu nilikuta wanatoa kozi ya kujibu maswali ya kwenye interview.
Katika kufuatilia nkakuta nao wana-download yaleyale kwenye internet, afu wanakariri tu.
Hata wewe haya yote yapo kwenye net. Acha wizi.
 
Nakuongezea hii

Ukiona unaongea na mtu mazungumzo marefu halafu imefikia muda kila unachomuambia yeye anaitikia - kweli, kweli, kweli hata pale isipostahili jibu hilo

Ujue amechoka huyo
 
je utafundisha na body language ya kutongoza????

je tutaweza jua body language ya mtu muongo wakati unaongea???

kwanni usiweke hapa hapa kwenye jukwaa tukafaidi wote???

absolutely yes.......akidanganya utajua..... 3 wise monkeys which never see, hear or speak!!

yes........utafundishwa how to approach gal, mteja na kadhalika, pia utafundishwa namna ya kujua km he/she unae muapproach atakukubali au la ili usipoteze muda kwa mtu ambae is unlikely kukubali......

....about kuiweka mada nzima hapa jf inakuwa ngumu sana ni km cuz issue yenyewe inahitaji kupractice so is not that simple and u have to pay cash for it..
 
 
Kwa kweli kujiajiri kipaji, hongera kwa ubunifu.
 
Nakuongezea hii

Ukiona unaongea na mtu mazungumzo marefu halafu imefikia muda kila unachomuambia yeye anaitikia - kweli, kweli, kweli hata pale isipostahili jibu hilo

Ujue amechoka huyo

Mi nikichoka huwa napiga mihayo ya kufa mtu, hata sijui huwa inatokea wapi. Tukimaliza tu mazungumzo na mihayo inakwisha.....
 
Mi nikichoka huwa napiga mihayo ya kufa mtu, hata sijui huwa inatokea wapi. Tukimaliza tu mazungumzo na mihayo inakwisha.....
Ndivyo inavyokuwa mkuu, kuna watu wanachosha halafu hawana magutu/machale kusoma mchezo - yeye ataendelea na mazungumzo tu
 
mambo ya kizungu...mzungu ndo anatoa body language

waswahili tunatoa body insult:eyebrows::eyebrows:

mtu kakaa anawaza kodi ya pango ila anaitafakari akicheki boli la mani u...pembeni anashushia castle lite ..utamsoma kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…