Bodi ya mikopo mambo yameiva muda wowote kuanzia siku ya leo mambo yatakuwa hadharani

Vijana ingawa hii ni serikali ya Magamba,bado naamini kuwa watajitahidi kutoa mikopo kwa watu wote ambao kwa kweli ni wahitaji wa mikopo, msijali si unajua sisi ndio wapiga kura mwaka 2015 hawawezi kufanya upuuzi wa kutubania mikopo sie wakina kayumba hata kama tumechaguliwa non priority coarses

Mjomba mkopo ni kwa wale waloandikiwa PRIORTY 2,kwa mujibu wa HESLB.
 
Wana ndugu nimepata taarifa sasa hivi kupitia mwana dodoso mwenzangu aliye ndani ya HESLB na amenihakikishia ya kwamba taratibu zote za ku-upload majina ya wanafunzi waliopata mikopo ya elimu ya juu umefikia tamati hivyo muda wowote kuanzia sasa tuelekeze macho yetu ndani ya Welcome to HESLB tukajionee wenyewe mambo ya bodi. Kwa mliotembelea website ya HESLB sasa hivi mtaona baadhi ya mabadiliko katika website hiyo kwani hata kale ka alama ka-new hakaonikani tena. Mjumbe hafungwi. asanteni nimefikisha.

Asante kwa taarifa
 
oya wazeiya ni kweli mi mwenyewe nimeambiwa hivyo hivyo. Source 0713122995 mcheki huyu jamaa ana uhusiano wa karibu na heslb.
 
wanatoa sangapi wadau?? maana tulishasikia maneno kama haya muda tu msiwe mnatuzengua bwana
 
kwa sasa watu wengi wanasubiri mikopo kwa hamu kubwa,wengi wao wana umri mkubwa kuliko wewe sasa sio vyema kuwadanganya na kuwarusha roho kiasi hicho.siku zote taarifa zako zimekua hazina tija kabisa.muungwana asipokua na la kusema huwa ananyamaza tu na kusikiliza wengine,sio lazima kuandike wewe tu kila siku
 
Nyie mnaobishana humu ndio mnaoweza kujisomesha bila loan. Wahitaji wenyewe wapo huko vijijini wanasubri waletewe taarifa kwa simu. Ha ha ha
 
Back
Top Bottom