Bodi ya Mikopo inawaibia Watanzania

Bodi ya Mikopo inawaibia Watanzania

Hayo maesabu unajipangia wewe unapeleka laki 4. Kama unaenda kulipia Kodi ya nyumba. Ndio maaana wamewatageti watu wanaopata mshahara wanakata kwa asilimia. Na mikopo waliopata ni watu wa degree ambao mshahara wao unaanzia 750,000 na kuendelea na kama ni asilimia 15 wanakata kwa mshahara ujue ni 1,350,000/- kwa mwaka apo na ujue mshahara kila baada ya miaka 2 mshahara unapanda ivi vitu vinahesabika, sema watu wengi wanaingiza kwy mkopo Mambo ambayo ukuwa nayo wakati wa mkopo. Mfano umu vyuoni wakati unapata mkopo unajiingiza kwy matumizi yasiyoendana na mkopo uliosainiwa kama kusomesha wadogo zako, kwenda kutafutia mademu, kuolea na kuongea mpaka unamaliza chuo unajikuta una mke na watoto 2 unaanza kazi tayari una wategemezi kitu ambacho mkataba wa mkopo hautambui wategemezi hao, mkopo unakutambua wewe na mzazi aliyekuwa referees wako. Tujifunze kuishi kwa bajeti sio kulalamika tuuuu.
Soma kwanza ujue mada inahusu, na ujaribu kuficha upumbavu wako, kusomesha kwa pesa ya bodi wewe inakuhusu nini?
 
HIvi unatetea nini wewe mjinga? Tena haujui kuwa ni mjinga - ukaamua kuweka msisitizo wa ujinga wako katika maandishi mazito meusi (bold)! Hivi umesoma michango hii ambao umezaa coment yangu (Tilburg1 na Molembe)?
tilburg1 said:
Kweli ni post nzuri, ila nina wasiwasi na alivyo kokotoa hiyo nyongeza ya 6% ya mkopo kila mwaka wa fedha, sababu nilivyo ona huo utoaji wa hiyo mikopo ya masomo ya juu nikama wame copy na ku paste toka nchi za hapa Ulaya, ila wao wamezidisha sana asilimia za marejesho. hiyo 6% huwa ina kokotolewa kutokana na deni unalo anzanalo katika mwaka ule wa fedha na sio deni Original, kwa hiyo kama mwaka ulio pita ulidaiwa milioni 30 umelipa milioni tufanye 2, kwa hiyo mwaka huu unaanza na deni la milioni 28 kitakacho ongezeka ni 6%*28 millioni nikama nyongeza ya 1.6millioni, kwa hiyo kadili unavyo lipa deni ndivyo nyongeza inavyo pungua. Lengo ni kuwasukuma watu walipe madeni yao, yule ambaye halipi deni lake ndio linaongezeka zaidi.
Ila ushauri wangu mimi nikuwa mwanafunzi anaye soma mpaka kumaliza masomo yake vizuri basi serikali imsaidie 40% ya malipo au hata zaidi kwa kadiri watakavyo ona, bali yule anayeishia njia bila sababu muhimu kama matatizo ya kiafya namengineyo basi alipe mwenyewe pesa yote aliyo kopa na nyongeza.
Na huu hapa wa Molembe:
Kwahiyo ukichukua mil 28 +1.6m=29.6 tofauti ya laki nne tu, sasa hapo unakuwa unalipa deni au una maktaimu?
Hayo maesabu unajipangia wewe unapeleka laki 4. Kama unaenda kulipia Kodi ya nyumba. Ndio maaana wamewatageti watu wanaopata mshahara wanakata kwa asilimia. Na mikopo waliopata ni watu wa degree ambao mshahara wao unaanzia 750,000 na kuendelea na kama ni asilimia 15 wanakata kwa mshahara ujue ni 1,350,000/- kwa mwaka apo na ujue mshahara kila baada ya miaka 2 mshahara unapanda ivi vitu vinahesabika, sema watu wengi wanaingiza kwy mkopo Mambo ambayo ukuwa nayo wakati wa mkopo. Mfano umu vyuoni wakati unapata mkopo unajiingiza kwy matumizi yasiyoendana na mkopo uliosainiwa kama kusomesha wadogo zako, kwenda kutafutia mademu, kuolea na kuongea mpaka unamaliza chuo unajikuta una mke na watoto 2 unaanza kazi tayari una wategemezi kitu ambacho mkataba wa mkopo hautambui wategemezi hao, mkopo unakutambua wewe na mzazi aliyekuwa referees wako. Tujifunze kuishi kwa bajeti sio kulalamika tuuuu.
 
HiHivi rais wa wanyonge anasomaga uzi mzuri kama huu,bodi ya mikopo ni kirusi kinachowatafunna watoto wa maskin,na mbaya zaid hali si shwali kwa waliosoma sayansi,ukiangalia salary slip zao utasikitika,utakuta mtu anadaiwa mpaka milion 30,ikute una penalty hadi milion 40,na makato hayako fixed.
Huu ndo tunasema wizi na unyanyasaji kwa vijana maskini wa nchi hii, tafakari huyu kijana aanze maisha na deni la milioni 40 na hapo hajapata kazi, na unaambiwa kasoma chuo kikuu cha umma
 
Haya mambo magufuli ndio kayaleta angeacha ile asilimia 8 iliyokua inatumika.utaratibu wa mwanzo ulikua mzuri kaja yy kavuruga kila kitu
 
Mkuu hizi habari za kusema utulie kwanza sjui ukae vizuri unazitoa wapi?? Huu uzi hauna cha kusubiri mwagika kila kitu hapa tunataka mambo yote yawekwe adharani kuhusu upupu wa hawa jamaa

Kiongozi,ni maelezo marefu kidogo ambayo nataka niambatanishe na vielelezo husika kabisa vya Salary slip zangu pamoja na notice za HELSB, sitaki masihara kabisaaa!!
 
Haya mambo magufuli ndio kayaleta angeacha ile asilimia 8 iliyokua inatumika.utaratibu wa mwanzo ulikua mzuri kaja yy kavuruga kila kitu

Mkuu kwa sharia kandamizi iliyopo,ingebakia 8% ndo ilikua mbaya kabisaaaa

Maana deni ndo lisingeisha mpaka tunaozea kaburini
 
. Bodi ya mikopo ijipange .. Isiumize wachache ambao wamejitolea kulipa kufikia malengo ya 80% ambao bodi imeshindwa kuwafikia

Hawa ambao hawalipi asilimia kubwa hawajapata ajira, wanalipaje? Bado shida ni kubwa, wazazi wao ndio hawa wanaojikongoja familia iweze kujikimu, na wengine pia wapate elimu.
Kulipa kweli zilipwe lakini sio kwa style hiyo ya komoa
 
Hesabu za kuzidisha na kutoa inaonesha hiyo asilimia 6 ya kila mwaka kwa kipindi chote cha marejesho miaka 10 inafika asilimia 26 ya kiasi cha deni uliloanza nalo kama utakatwa mfululizo.
Wataalamu wa benki mtusaidie hii asilimia 26 kwa mkopo wa miaka 10 ni fair?
 
Kiongozi,ni maelezo marefu kidogo ambayo nataka niambatanishe na vielelezo husika kabisa vya Salary slip zangu pamoja na notice za HELSB, sitaki masihara kabisaaa!!
Sasa ndo tupambane mpaka tone la mwisho kuhakikisha haki inapatikana siyo tena ukate tamaa kama jina lako linavyosomeka hapo kwenye id
 
Tusisahau rais wa wanyonge ndio alisaini 15%. mimi naona wote wauaji.watumishi chamoto hakitaisha hapa
 
. Kwako *Dr.John Pombe Magufuli*

Bodi ya Mikopo imewanufaisha watanzania wengi sana ikiwa ni pamoja na kuwajengea watanzania misingi ya kielimu kwa ajili ya future katika maisha yao . Aidha, Asilimia 80 ya wanufaika wa mikopo ya bodi ni wale kina KAYUMBA Yaani watoto wa maskini.
Sheria ya mwaka 2016 ya bodi ya mikopo iliyofanyiwa marekebisho ni sheria *ANGAMIZI* kwa watoto maskini.
*Sheria imeweka wazi ( Watz wengi hawana tabia ya kujisomea) kuwa marejesho ya mkopo yatakuwa ni kwa 15%, na deni hilo litakuwa linaongezeka kila mwaka wa fedha kwa asilimia 6% ya deni halisi la mwanzo.*
Kwa mfano.
*Daktari ambae amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30.*
Basic salary yake ni 1.5 Mil
Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo
Helsb 225, 000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension. 80, 000
Total deduction 642, 510 TSH
take home yake ni 857,590 TSH —ana watoto na anasomesha!
-----------------------------
Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil ( 225,000X12)
Hivyo katika deni lake la 30Mil , atakuwa amepunguza deni lake hadi 27, 300,000TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.
Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27, 300, 000 TSH.
Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil
Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000+ 1.8 Mil sawa na 29, 100, 000 TSH.
Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.
Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambaye ni 1.8
Hivyo 26,400,000+ 1.8 mil
Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on.
Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.
Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa.
Yaani, Ikiwa una pension ya 15 Mil , na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria.
Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi,maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.
I just can't figure it out , ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu.
Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni , ni deni la maisha hasa waliosoma makozi ya sayansi kama udaktari, Nesi, famasi , na injinia na wale waliosoma nje ya nchi.hawa wote madeni yao si chini ya 25Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair.
Mapendekezo
1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wheri anakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno.
2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika na hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.
3. Bodi ya Mikopo itoe elimu maredioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato WaTZ wengi haijui kitu kuhusu mambo ya sheria.
4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu itolewe kwa Sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.
Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli ? Doh tutapata laana katika nchi.
USHAURI.
1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho, hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil.
2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake, you need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akuelewesheni ni hatari sana fuatilieni haya mambo.
Rais JPM tunaomba ufanyie kazi hayo mapendekezo kwa heshima na taadhima .

*Wako Raia Mwema.*
[Heri nimeacha kazi na kwenda kufuga nguruwe na sungura kwa mwezi napiga m12 bila cammisina kujua ]
 
Heri nimeacha kazi na kwenda kufuga nguruwe na sungura kwe mwezi napiga m12 bila kamishina kujua
 
Heri nimeacha kazi na kwenda kufuga nguruwe na sungura kwe mwezi napiga m12 bila kamishina kujua

Watakukamata tu siku za usoni huko huko uliko. Kuna wenzako miaka hiyo nilipokua nakatwa, nikawashauri wajisalimishe wenyewe; wakapuuza! Leo hii wanalia na kusaga meno! 15% ya basic salary si mchezo! Hawaangalii salary slip ina take home ya shilingi ngapi.
 
Back
Top Bottom