Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

Kumbe msaada bado upo . Mi nilidhani tumenyimwa kabisaaaa. Wanachotaka wao ni sisi kurekebisha kasoro fulani fulani kisha watautoa. Nadhani wataweka bank kifaida kwa muda kwa ajili yetu hadi tumalize hizo kasoro. Kwa hiyo wanaopata msaada huo sasa itakula kwao. Sisi fungu letu litawekwa bank kifaida hadi hapo tutakapomaliza hizo kasoro. Siunajua tena kinachokaa bank kwa muda huzalisha. Siku wakaianza kutukumbukatutapata na faidha yake toka bank. Patamu hapo! Ndiyo maana waswahili husemaharaka haraka ya kupata misaada sasa haina baraka. Wanaopata sasa itakua kwao.

Acha kupotosha sio watautoa no! Watalipitia tena faili letu lisipokidhi vigezo tunapigwa chini tu..
 
TUJIANDAE PIA KUCONSUME MALIGHAFI ZETU ZOTE IKIWEMO DHAHABU, KAHAWA, PAMBA, MWANI, ALMASI ZETU TUNAZOZALISHA KWANI SOKO LIKO KWAO, RAHA SANA MIDHAHABU NA MIALMASI TUTACONSUME WENYEWE, TUACHANAE NA MASOKO YA ULAYA, O/w BekaNurdin UMETIKISA MASIKIO, HUJUI ULISEMALO, MATAIFA IFA MAKUBWA NI KAMA MAJI USIPO YANYWA UTAYAOGA
Soko kubwa la dhahabu liko wapi????!!!!
 
Halafu hizi ni hela kidogo sana. Mazoea tu ya kuhongwa!
Sio kwamba nakataa sababu walizozitoa, ni kweli vitu hivyo viwili vishughulikiwe haraka.
 
Habari ilopo ni kwamba Tanzania wamenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya suala la Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na cyber crime legislation.

Hawa jamaa wameshatugeuza mazuzu,leo wanasema ,uchaguz zanzbar na cyber crime kesho wanakuja na hoja ya USHOGA.
 
Halafu hizi ni hela kidogo sana. Mazoea tu ya kuhongwa!
Sio kwamba nakataa sababu walizozitoa, ni kweli vitu hivyo viwili vishughulikiwe haraka.


Ndugu yangu!!!!!!!!!!!!!!

Hivi unaelewa maana ya Tsh. Billions 992.80 !!!!!!!!!!!
 
Siku nchi hii itakapovunjika amani kama Burundi sababu ya masuala ya uchaguzi,tukaanza kuuana ndio mtajua kwanin wanatunyima msaada!Wakiendelea kutupa misaada huku demokrasia ikiendelea kubakwa siku yakitokea yakutokea tutaanza kuulizana walikuwa wapi kufumbia m?cho viashiria vya uvunjifu wa amani ambapo kwa wingi Africa imeonekana kuwa ni ubakaji wa demokrasia!
Hakika tusipojirekebisha,ipo siku tutawakumbuka kwa kutuonya mara kwa mara!

Kwan Uganda walipokata Misaada walikwambia ni Ubakaji wa Demokrasia,we pinga USHOGA kama uwaone
 
Kwanza ni aibu ya kufa mtu.Mnapewe hela ya burw ya meandeleo kwenye nchi maskini kama hii halafu mnasglhindwa sababu ya Shein na CCM mfu.Ni Upuuzi uliopindukia
 
Yaani wewe unafikiria demokrasia ya Burundi halafu unalinganisha na Tanzania?

Ni sawa sawa na kusema usimcheke huyo mtoto kwa sababu kuna siku unaweza ukawa kama mtoto wakati kwa sasa nina miaka ya ujana.

Tanzania tumeishavuka hiyo demokrasia ya Burundi na haitatokea tena kurudi nyuma kwa kiwango hicho.

By the way, watanzania wengi wana haiba ya kutopenda vurugu katika maisha yao.

Bahati mbaya kuna watanzania wachache wanaotumia tabia hii ya watanzania wengi kutopenda vurugu kuwavuruga hao wengi kwa kuwatishia vurugu nyakati za uchaguzi.
 
Nchi zote duniani huheshimiana mipaka na kutoingiliana mambo ya ndani.Nchi zote duniani huwa na mahusiano katika mambo kadhaa wanayokubaliana.Nje ya yale wasiyokubaliana huwa hakuna mahusiano.

Tanzania bara na Zanzibar tuna mahusiano kati baadhi ya mambo ambayo yako katika katiba.Katika mambo hayo ya uhusiano swala la uchaguzio wa Zanzibar si la muungano na halimhusu raisi wa muungano sababu raisi wa muungano kazi yake ni kushughulikia mambo yale tu ya muungano na si yale yasiyo ya kimuungano.

Raisi wa Tanzania haiwezi ingilia mambo ya nchi yoyote ile iwe marekani au Zanzibar.

Bill Gate na MCC na wafadhili wote na watoa misaada hilo walielewe na wasichanganye mambo na kutupa masharti ya eti raisi atatue matatizo ya uchaguzi zanzibar si sahihi.Zanzibar ni nchi huru kama marekani.Hivi bunge la marekani laweza sema hatupitishi bajeti ya marekani hadi marekani itatue tatizo la zanzibar?

Mambo ya Zanzibar ni kama ya burundi nk ambapo kinachotakiwa ni kuomba ikiwezekana Raisi wa Muungano au hata wa burundi asaidie kumaliza mgogoro zanzibar.

Hili la kushinikizana si haki.Na wamarekani na jumuiya ya kimataifa ni vizuri wakawajua CUF vizuri kama hawawajui shauri yao.Kitendo cha MCC kutishia kutoipa misaada Tanzania Sijakipenda nadhani wana mshauri mbaya sana tena sana asiyesoma katiba ya Tanzania wala kujua uhusiano uliopo kati ya Raisi wa Muungano wa Tanzania Na Zanzibar.

Zanzibar ni nchi huru kama ambavyo akina Seif Sharif Hamad wanavyobwata Sasa zigo hilo linalowahusu nchi yao walimalize wenyewe kwa nini waitumbukize kwa Raisi wa Jamhuri ya muungano ambaye halimhusu na kufitini kwa wafadhili nchi ikose misaada?

Tunaomba wafadhili na watoa misaada msituonee kama ambavyo sisi hatuwaonei wawekezaji wenu toka nchi zenu.
 
Hii ni rasmi tumenyimwa! Angalia hapa chini;
----------------------------------------------

MCC Board Selects Five Countries for MCC Partnerships


New Compacts with Cote d?Ivoire, Kosovo and Senegal, and New Threshold Programs with Sri Lanka and Togo

For Immediate Release
December 17, 2015
Renee Kelly
202-521-3880

WASHINGTON, D.C., Dec. 17 ? The Millennium Challenge Corporation (MCC) Board of Directors held its quarterly meeting on Dec. 16, 2015. The Board approved three countries as eligible for compacts and two countries as eligible for threshold programs. Three of the five countries are new partners for MCC and all have worked hard to improve their performance on MCC?s scorecard, which measures countries? commitment to ruling justly, economic freedom, and investing in their people.
The Board selected Cote d?Ivoire, Kosovo and Senegal as newly eligible for compacts. Cote d?Ivoire, which was selected in December 2014 for a threshold program, will now transition into the compact program after showing continued improvement on its scorecard and achieving greater political stability. Kosovo, which passed MCC?s scorecard for the first time after making progress on democratic rights, is a new partner for MCC. Senegal successfully completed its first MCC compact in September and demonstrated improved scorecard performance over the life of the partnership.
In both Senegal and Cote d?Ivoire, the Board recommended that MCC explore potential investments that address regional obstacles to economic growth, in addition to domestic investments, while recognizing the need for statutory authority to optimize regional impact.
The Board also selected Togo and Sri Lanka to develop MCC threshold programs. Togo has shown a clear upward trajectory on overall scorecard performance over the past few years. Sri Lanka has embarked on a remarkable effort over the past year to reinvigorate its democratic institutions, improve governance, and restore protection of human rights.
Nepal, Niger and the Philippines were reselected by the Board to continue developing their compacts. The Board reselects all countries in compact development as part of the annual selection process. The Board deferred a vote on the reselection of Tanzania and Lesotho for compact eligibility until relevant governance concerns in both countries have been addressed.
Finally, the Board reaffirmed its commitment to developing a compact with Mongolia and its support for a strategic partnership with India to advance economic growth and poverty reduction in South Asia.


The Millennium Challenge Corporation is an innovative and independent U.S. Government agency working to reduce global poverty through economic growth. Created by the U.S. Congress in January 2004, with strong bipartisan support, MCC provides time-limited grants and assistance to countries that demonstrate a commitment to good governance, investments in people and economic freedom. Learn more about MCC at www.mcc.gov.

Kama board ya MCC imedefer a vote-ina maanisha Tz imepewa muda zaidi kurekebisha mambo-meaning kuna maelezo MCC wamepelekewa na wameona na wameridhika waipe TZ muda zaidi irekebishe mambo. Serikali inazihitaji hizo pesa ndio maana wamesema watanzania wasiwe na wasi wasi zitatolewa. Jnaelekea nyuma ya pazia kunakinachoendelea au sivyo panga lingeshuka.

Kama kweli hili limetukera basi tujipange lakini jazba haitatusaidia. Mashariti ya msaada lazima
tuyatimize
vinginevyo tujipange sio kukurukupa.
 
Ukipitia michango yote ya hii mada utagundua kuna ujinga umejikita kwenye itikadi za siasa. Hoja iliyopo ni MSAADA wa MCC. Lakini watu wanakwenda mbali kujadiri kujitegemea kukusanya mapato ya ndani mikataba Lowasa. Kukosa ufahamu wa masuala ya msingi kama uchumi na maendeleo na kushabikia itikadi mufilisi ambazo miaka 54 zimeshindwa kutujengea uchumi na kutuletea maendeleo ni mapungu makubwa sana kwenye uelewa wetu.

Tuna nafasi ya kujitegemea na kupokea misaada kwa ajili ya maendeleo yetu. Hatuna nafasi ya kubaka demokrasia siku zote na haya ndiyo matokeo yake. Na kwa wasiofahamu uamuzi wa MCC utashawishi wadau WOTE wa maendeleo kutuwekea ngumu
 
Kwani mgombea uraisi znz kupitia ccm mwenyekiti wa chama chake yuko wapi? Hivi anaenyimwa msaada sio rais wa znz? Unazani huyo jpm hajachaguliwa na rais wa znz?
 
Shirika la millennium challenge la Marekani hatimae wamekataa kuipa Tanzania fedha za kujikimu kimaendelea.
Zaid fuatilia katika website yao

Eligible Countries

The Board met on December 16, 2015, to select countries that will be eligible for assistance under section 607 of the Act (22 U.S.C. 7706) for FY 2016. The Board selected the following countries as eligible for such assistance for FY 2016: Cote d?Ivoire, Kosovo, and Senegal. The Board also reselected the following countries as eligible for FY 2016 compact assistance: Niger, Nepal, and the Philippines. The Board did not vote on the re-selection of Tanzania and Lesotho. The Board also reaffirmed its support for Mongolia?s continued effort to develop its compact proposal that will access funds appropriated to MCC when Mongolia was a candidate country.
 
Kama kawaida yako huna uwezo unawadindia wenye uwezo kwa elimu ya Lumumba. Unajipinga mwenyewe kwenye hoja zako.

Endeleeni na ubabe wa kisiasa (za CCM) hata ushirikiano wa maendeleo wa humu ndani mtausikia ukibuma.
 
kweli mkuki kwa nguruwe mtamu ila kwa binadamu mchungu . hiv mmesahau mliyowafanyia cuf kwa kuwabania ikulu wakati ushahidi unaonesha maalim alishinda ? acha mzuiliwe hiyo misaada mjifunze kuheshimu katiba
 
Hakuna msaada usiokuwa na masharti. Hata ule msaada anaekupa mzee wako aliokuzaa anawekeza kuwa siku moja utakuja kulipa fadhila. Sasa unakuwa na kiburi kwa pesa za watu, kodi za watu. Mmebebwa halafu aliekubebeni mnamkojolea mgongoni. Azidi kubebeni si mtamtia kinyesi mgongoni mkono wa kutoa uko ju na wa kupokea uko chini
 
Back
Top Bottom