Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

tukusanye wenyewe, kwani hiyo ingine si walikuwa wanakula wajanja tu....??

Hii tunayokusanya pamoja na hizo za wahisani ndizo zitakazoleta MABADILIKO tunayohitaji Tanzania.

Ni mapema mno kujitgemea.
 
watanzania tuache umbumbu na ushabiki wa kijinga.
Hizo sababu nyingine ni zipi...!!
Tatizo la Zanzibar mnaliona kuwa ni la mzaha?
Ukweli waheshimiwa Lowassa na Mbowe na UKAWA kwa ujumla waliona mbali...ELIMU....ELIMU...ELIMU!
VIVA LOWASSA.....VIVA UKAWA!
Kwani umeambiwa hamna kinachofanyika? Kwamba rais na watu wake wamepotezea tu ishu ya Zenji? Au wewe unataka hata kama kuna serious irregularities waendelee nayo tu? Tuliza mpira!
 
Kwa hiyo!!!!!!!!!?????? Wewe umefurahi si ndiyo??????

Mimi nimefurahi sana na nasema tunyimwe Tu tena sana.
Hela zimejaa hapa kila kona msaada wa nini?

Sisi siyo matonya bana
 
Mi naona hawa huwa wana sababu zao za kutotoa msaada. Siwezi amini eti hiyo ndo sababu. Kwani wao sera zao za mambo ya nje zina hata chembe ya demokrasia?

Inawezekana sana mkuu wangu Paradigm kwa maana hili swala si geni hata kidogo maskioni mwangu. Walishatupaga taarifa ila viongozi wetu wakajitetea bila kuchukua tahadhari stahiki, yaani viongozi walituaminisha watanzania kwamba suala la Zanzibar litashughulikiwa kabla ya hicho kikao cha jana na pia masuala ya wale jamaa wa ukawa waliokamatwawakati wa kampeni. MCC hawakuwa na kigezo kingine cha kutunyima huo msaada ila ni hayo tu mkuu. BORA KUZIBA UFA KULIKO KUJENGA UKUTA. Huu msaada ungemsaidia sana JPM na ahadi zake.
 
Hakika wazungu hawa watatudhalilisha sana. Nyerere alisema kweli kwamba mnaweza kuachana na Ujamaa lakini hamtaweza kuachana na Kujitegemea. Nikigombea urais mwaka 2025 kauli mbiu angu itakuwa "Hapa Kujitegemea Tu"
Aya zito kabwe tumekusikia 2025 unayo kura angu
 
Kabla hujachangia hii topic unalazimika kuwa na kibari harari cha kuishi na kujiusisha na mambo ya ndani ya Tz. Kachangie kwenu Kenya.

'Kibari harari' mtaji wa CCM ni Ujinga kama huu.

Mkiambiwa ukweli hamtaki eti rudi Kenya ila msaada unataka kutoka Marekani.
 
Hawa wazungu bwana, wanatuibia halafu pesa yetu hiyo hiyo wanarudisha kama msaada tena kwa masharti, sasa ni bora tupunguze mianya ya wao kutuibia, ili tuishi kwa kuheshimiana.

Hili ndo wazo mbadal Mkuu, suala linakuja namna ya kujinusuru naye, nchi yetu haina uwezo kamwe wa kupambana na Mmarekani mkuu kwa kila kitu, hawa jamaa washakita mizizi sana na wanajua yote tunayoyafanya, kila hatua tunayopiga wapo nyuma tuu.

Nchi kama China na Russia wanajaribu kujinusuru naye kwa miaka mingi sana lakini bado wanaye tuu kiunoni, Ni matumaini yangu unajua yanayotokea kule North Korea, wale wanampaka viwanda vyao lakini bado ni tatizo tuu, Je itakuwa siye tusiokuwa hata na uwezo wa kutengeneza tooth pick.

Wazo lako la kujinusuru nao ni mipango ya muda mrefu sana tena sana, na hapo inabidi tujivike uendawazimu haswaaa tufanye kazi zaidi na zaidi.
 
Hii ndiyo statement ya The Millennium Challenge Corporation (MCC) Board of Directors!

For Immediate Release
December 17, 2015

Renee Kelly
202-521-3880

The Millennium Challenge Corporation (MCC) Board of Directors held its quarterly meeting on Dec. 16, 2015. The Board approved three countries as eligible for compacts and two countries as eligible for threshold programs. Three of the five countries are new partners for MCC and all have worked hard to improve their performance on MCC?s scorecard, which measures countries? commitment to ruling justly, economic freedom, and investing in their people.



Nepal, Niger and the Philippines were reselected by the Board to continue developing their compacts. The Board reselects all countries in compact development as part of the annual selection process. The Board deferred a vote on the reselection of Tanzania and Lesotho for compact eligibility until relevant governance concerns in both countries have been addressed.


Kwa kinachoendelea Zanzibar na kilichotoeka wakati wa Uchaguzi kwa kamata kamata ya vijana wa CDM wa kituo cha kujumlishia matokeo hili linatustahili kutoka kwa mabwana zetu wa Uchumi.Na hii itawalinda hao watoa pesa kuwa nao siyo wale wale !
 
Kweli Jecha katuweza duh! Kwaheri umeme vijijini, miradi ya barabara na miradi mingineyo ya maendeleo.!
 
Washabikie tu iko siku watakwambia ili upate hiyo hela yako ukubali watu wafanye ngono na mbwa uoe mwanamme na ndoa za waume kwa wake marufuku usipokubal hawakupi misaada ndo unajua yesu yu mlangon

Kwa upande mmoja ni sawa maana kumbuka walishakuja Kenya , Tz tunakumbuka wakichojibiwa na JK, na pia kubwa lao ni yale majibu ya mzee wa Zambia kuhusu hiyo ndoa ya jinsia moko. Cha muhimu tuzungushe zaidi bakuli letu la kodo ila nasi siku moja tuweze kujikwamua kwenye hii hali ya ombaomba jappo kwa sasa bado wachanga kimtindo.
 
Hawa wazungu bwana, wanatuibia halafu pesa yetu hiyo hiyo wanarudisha kama msaada tena kwa masharti, sasa ni bora tupunguze mianya ya wao kutuibia, ili tuishi kwa kuheshimiana.

Mtahangaika na vijimaneno jf.
Mzungu atakutawala milele
 
Habari ilopo ni kwamba Tanzania wamenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya suala la Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na cyber crime legislation.

Nadhani siyo misaada ya Bure kabisa!.Pengine msaada wenye masharti nafuu!



Section 2.4

Interest

. The Government shall pay to the MCC any interest and other earnings that accrue on MCC Funding in accordance with the Program Implementation Agreement(whether by directing such payments to thebank account outside Tanzania designated by the MCC or otherwise)
 
Inasikitisha kweli kwa maana HATUKUTEGEMEA hasa kwa kile kiaminisho toka kwa viongozi wetu wa ngazi za juu kuhusu ukamilisho wa muStakabali wa Zanzibar na suala la vijana wataalam wa IT wa upande wa UKAWA, HIVI VIWILI NDO VIKWAZO VIKUBWA vilivyosababisha kukosa kwetu huo msaada. Japo tunapenda kua maskini jeuri ila baaaado labda JPM akae vipindi vinne na apewe ushirikiano wa hali ya juu sana na pande zote mbili. Naamini tunaweza kufika tunakotaka , tena mapeeema sana ila kama tu hawa MAPAPA WAKUBWA wanaojulikana ila wanaogopwa wakishughulikiwa mapema na kunyamazishwa kabisa, naam tutaweza at least kujiita maskini jeuri. ila kwa sasa BAAADO.
 
WB iliwanyima Ethiopia ela ya kujenga dam baada ya wana harakati wa mazingira kuleta figisufigisu....Ethiopia wakasema tunatumia ela ya ndani...mradi umeshakamilika
Tujifunze kujitegemea...
Si rahisi lakini inawezekana tukijifunga mikanda

You're very right. Ethiopia kirasilimali ni masikini kuliko sisi. Lakini wanafanya makubwa. Tena dalili zinaonyesha wanatupita kimyakimya kimaendeleo. Huwezi kukuta wageni au wafadhili wanaleta jeuri kule kama hapa. Tukiweza kufuta "uswahili" basi itawezekana kabisa kujitegemea kwa ukubwa wa rasilimali tulizo nazo. Vinginevyo, leo hii hatuna jeuri ya kuwasemea ovyo wafadhili.
 
Nchi lazima ianze kujitegemea
Tusijidanganye hawa wakubwa wakiamua wanaweza kuziwekea vikwazo bidhaa za Tanzania. Sasa tukishindwa kuuza bidhaa chache tulizonazo nje sijui dola za kuagiza mafuta na bidhaa nyingine muhimu tutapata wapi! Hatutaki nchi yetu iwe kama Zimbabwe kisa watu wachache wanang'ang'ania madarakani.
 
Salas la nchi ki vipi? . Kwamba Tz inayojinasibu ni ya kidemocrasi kumbe Changa la macho ?

Mi niwaulize pro ccm (utawala) kwenu mambo ya ndani na kidemocrasi ni kuifavor ccm??. Hata kama ni kuvunja sharia ?

Kujitegemea ni jambo la lazima na haliepukiki ukizingatia ni watawala (viongozi) haohao wanaotuingiza mikataba ya kishenzi na hao jamaa

Ni kweli wametuingiza mikataba ya kishenzi sana. Ona mikataba ya Richmond jamaa wamepiga hela afu leo wanajinasibu kwamba ni wasafi wanagombea hadi urais eti kisa demokrasia inawaruhusu wafanye hayo. Democracy my foot. Rais wetu JPM we piga kazi tuko nyuma yako. Nchi itajiendesha kwa mapato yetu ya ndani na si vinginevyo. Wamarekani watasubiri sana na watashindwa
 
Back
Top Bottom