Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

Punguza kiwango cha upumbavu kwenye akili yako!Jifunze na jifikirishe kidogo!Tunachoshuhudia Burundi Leo ni matokeo ya ubakwaji demokrasia!Siku yakitokea Tz tutaelewa tu

Haitakaa itokee Tz, acha uoga na ulofa, ni muda wa kujitegemea
 
Habari ilopo ni kwamba Tanzania wamenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya suala la Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na cyber crime legislation.

Anaekunyima msaada anakupa akili ya kutafuta za kwako.wakae nazo tu,naamini tutafika kwa kodi zetu
 
Nchi lazima ianze kujitegemea

Ukiangalia kwa umakini hakuna anayepinga tusijitegemee, tatizo ni basis and basics za kujitegemea hatukuwa nazo tangia enzi za Mwinyi, Nyerere alijitahidi kuweka misingi mizuri sana ambayo ilikosa watu makini kuiendeleza. Na kama unakumbuka vizuri ilifikia hatua hawa watawala wa sasa kwa kukosa ubunifu walifikia hatua ya kututangazia kabisaa kwenye media kwamba nchi yetu bila misaada haiwezi kusonga mbele. Sasa kama unaviongozi wenye maono kama hayo unategemea tutapiga hatua ipi?

Hali hii inayotokoa sasa inapaswa iwe chachu ya kutufanya tuandae strategies za kujitegemea, hatuwezi jitegemea ghafla tuu inahitaji process na kuwa na team ambayo ni commited haswaaa, vile vile hali ya uchumi irejeshwe kwa wazawa na uwezeshaji uwe wa kiwangu cha kuridhisha. Wazawa tunapaswa tuumiliki uchumi wetu tofauti na sasa, kiufupi uchumi wetu upo katika hali mbaya mnoo. Tunahitaji muda mpAka kufikia hatua ya kukataa misaada.

Nadhani tujipange kwa pamoja tutafika tuu pale tunapopataka.
 
Ni kweli pesa zinahitajika sana kwa maendeleo!

MCC hawajainyima pesa Tanzania bali faili la Tanzania limewekwa kando kwanza mpaka vidokezo ambavyo walivitoa vikamilike.

Statement yao inasema,

Neno muhimu katika statement yao ni DEFERRED

Kwa akili ya kawaida lazima tungefahamu wasingeweza kutoa maamuzi kuhusu Tanzania wakati Uchaguzi wa Zanzibar bado haujamalizika.

Ninakubaliana na uamuzi wao kwa sababu utazileta pamoja pande zit mbili huko Zanzibar ili zifikie kwenye makubaliano haraka.

Kama wangetoa hizo pesa, kulikuwa na hatari ya kumeguka kwa Zanzibar kwa sababu upande mmoja ungepata nguvu zaidi.

Wanadiplomasia husema, mazungumzo huwa yanafanikiwa kama pande zote zinazokinzana zinapokuwa katika hali ya usawa.

Yeah hili ndo linalopaswa liwe, nashukuru mkuu kwa kuleta hAbari kamili.

Wale jamaa wanatuhitaji sana tuu hata kama wana mikwara sana. Wanajua kabisaa AFRICA is the FUTURE, kwa hiyo hawawezi timiliza hiyo ndoto yao bila kutudanganyadanganya na misaada yao kutuweka karibu.
 
Punguza kiwango cha upumbavu kwenye akili yako!Jifunze na jifikirishe kidogo!Tunachoshuhudia Burundi Leo ni matokeo ya ubakwaji demokrasia!Siku yakitokea Tz tutaelewa tu
Yaani wewe unafikiria demokrasia ya Burundi halafu unalinganisha na Tanzania?

Ni sawa sawa na kusema usimcheke huyo mtoto kwa sababu kuna siku unaweza ukawa kama mtoto wakati kwa sasa nina miaka ya ujana.

Tanzania tumeishavuka hiyo demokrasia ya Burundi na haitatokea tena kurudi nyuma kwa kiwango hicho.

By the way, watanzania wengi wana haiba ya kutopenda vurugu katika maisha yao.
 
Hata George Bush alimshinda AlGore kimagumashi huko huko marekani....was that what we term as democracy??

Tutajitegemea...!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Una akili fupi sana hapa dunian
 
Manina zao, hatuhitaji msaada wao wenye kutupangia cha kufanya! Wakaboreshe ushoga na hiyo pesa nchini mwao.

Utatulia tu nchi haijiwezi kwa chochote halafu ndomo mkubwa muulize Nyerere nchi alivyo iwacha wazungu watu wabaya sana wakingangania ushoga tutapitisha sheria hiyo domo kubwa hats chupi hutengenezi unategemea nini kama so wazungu
 
WB iliwanyima Ethiopia ela ya kujenga dam baada ya wana harakati wa mazingira kuleta figisufigisu....Ethiopia wakasema tunatumia ela ya ndani...mradi umeshakamilika
Tujifunze kujitegemea...
Si rahisi lakini inawezekana tukijifunga mikanda
 
Yeah hili ndo linalopaswa liwe, nashukuru mkuu kwa kuleta hAbari kamili.

Wale jamaa wanatuhitaji sana tuu hata kama wana mikwara sana. Wanajua kabisaa AFRICA is the FUTURE, kwa hiyo hawawezi timiliza hiyo ndoto yao bila kutudanganyadanganya na misaada yao kutuweka karibu.

Offcourse!

Hizi nchi za Magharibi ni wanafiki sana.

Wao kama wanapata kile wanachokitaka huwezi kuwasikia wakipiga kelele.

Walitaka kuleta mdomo mrefu kuhusu Saudi Arabia eti SFO wanataka kufanya uchunguzi kuhusu deal la ununuzi wa vifaa vya kivita kwa sababu ilidaiwa kulikuwa na harufu ya rushwa.

Saudi Arabia ikawaambia mkifanya uchunguzi mtambue pia, huo utakuwa ndiyo mwisho wa kununua vifaa vyenu vya kivita. Walikaa kimya.

Kwenye masuala ya demokrasia huwezi kuwasikia wakipiga kelele kuhusu Saudi Arabia kwa sababu wanachokitaka Saudi Arabia huwa wanakipata (oil) lakini vile vile matajiri wa Saudi Arabia wameweka pesa zao kwenye mabenki na fixed assets katika nchi za Magharibi.
 
A blessing by disguise, tukusanye kodi zetu wenyewe ili nasi siku moja tuwe donner country.
Hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa; tokose misaada akili zichangamke na tuwekeze katika kupunguza, kama si kuondoa kabisa utegemezi. Kama sababu ni suala la Zanzibar basi linatusaidia kujipanga upya na kuacha utegemezi!

Mungu ibariki Tanzania
 
Hatutaki misaada yao kwa sasa, tunao uwezo wa kukusanya kodi yetu, ila na wao wafanye wafungashe vilivyo vyao hapa kwetu.
 
Habari ilopo ni kwamba Tanzania wamenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya suala la Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na cyber crime legislation.

Kwa hiyo!!!!!!!!!?????? Wewe umefurahi si ndiyo??????
 
Ni kweli mkuu!

Hatua ya kwanza tuwashukuru wazungu kutunyima pesa yao.

Pia tumshukuru Mungu kutupatia raisi asiye chekea wakwepa kodi na wala rushwa na wazembe.

Tukatae roho ya utegemezi na kutokujiamini. Tunaweza x 1,000,000,000 kujitegemea na kuendelea kama taifa bila kutegemea wazungu!
Nimipenda kauli hii. Kumbe wzalendo bado wako wengi
 
Kama ilivyokua suala la Escrow ni sawa maana hapa hela ilikuwa inaliwa wakati wao wanatoa za kwao. Lakini hapa hili ni suala la nchi binafsi na halina uhusiano wowote na pesa zao.

Salas la nchi ki vipi? . Kwamba Tz inayojinasibu ni ya kidemocrasi kumbe Changa la macho ?

Mi niwaulize pro ccm (utawala) kwenu mambo ya ndani na kidemocrasi ni kuifavor ccm??. Hata kama ni kuvunja sharia ?

Kujitegemea ni jambo la lazima na haliepukiki ukizingatia ni watawala (viongozi) haohao wanaotuingiza mikataba ya kishenzi na hao jamaa
 
Ukiangalia kwa umakini hakuna anayepinga tusijitegemee, tatizo ni basis and basics za kujitegemea hatukuwa nazo tangia enzi za Mwinyi, Nyerere alijitahidi kuweka misingi mizuri sana ambayo ilikosa watu makini kuiendeleza. Na kama unakumbuka vizuri ilifikia hatua hawa watawala wa sasa kwa kukosa ubunifu walifikia hatua ya kututangazia kabisaa kwenye media kwamba nchi yetu bila misaada haiwezi kusonga mbele. Sasa kama unaviongozi wenye maono kama hayo unategemea tutapiga hatua ipi?

Hali hii inayotokoa sasa inapaswa iwe chachu ya kutufanya tuandae strategies za kujitegemea, hatuwezi jitegemea ghafla tuu inahitaji process na kuwa na team ambayo ni commited haswaaa, vile vile hali ya uchumi irejeshwe kwa wazawa na uwezeshaji uwe wa kiwangu cha kuridhisha. Wazawa tunapaswa tuumiliki uchumi wetu tofauti na sasa, kiufupi uchumi wetu upo katika hali mbaya mnoo. Tunahitaji muda mpAka kufikia hatua ya kukataa misaada.

Nadhani tujipange kwa pamoja tutafika tuu pale tunapopataka.

Sioni haja ya mchakato katika kujitegeme.
....Inabidi tupitie kipindi kigumu cha kujitoa mhanga ikibidi
 
Salaaam kwa wamarekani. Watatunyanyasa sana, watatupangia sana lakini kama nchi huru tutapambana kwa ajiri ya nchi yetu. Wamenyimwa gesi walitaka tuingie vitani wakati wa uchaguzi sasa roho imewauma, na wataendelea kuelewa tu. Pesa zao wakae nazo ama wapeleke Libya waliko haribu.
 
Back
Top Bottom