Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

Bodi ya MCC yainyima Tanzania fedha za msaada

Salas la nchi ki vipi? . Kwamba Tz inayojinasibu ni ya kidemocrasi kumbe Changa la macho ?

Mi niwaulize pro ccm (utawala) kwenu mambo ya ndani na kidemocrasi ni kuifavor ccm??. Hata kama ni kuvunja sharia ?

Kujitegemea ni jambo la lazima na haliepukiki ukizingatia ni watawala (viongozi) haohao wanaotuingiza mikataba ya kishenzi na hao jamaa

Kabla hujachangia hii topic unalazimika kuwa na kibari harari cha kuishi na kujiusisha na mambo ya ndani ya Tz. Kachangie kwenu Kenya.
 
Ni kweli mkuu!

Hatua ya kwanza tuwashukuru wazungu kutunyima pesa yao.

Pia tumshukuru Mungu kutupatia raisi asiye chekea wakwepa kodi na wala rushwa na wazembe.

Tukatae roho ya utegemezi na kutokujiamini. Tunaweza x 1,000,000,000 kujitegemea na kuendelea kama taifa bila kutegemea wazungu!

Hakuna Mtanzania anayepinga suala la kujitegemea,heshima ya kwanza ya mwanadamu ni uwezo wa kumudu kuendesha maisha yake bila kuwa tegemezi.

Mwananchi wa kawaida linapokuja suala la kujitegemea analielewa zaidi kuliko Viongozi wetu.Mwananchi wa kawaida ambaye anavuja jasho na damu kila siku ili apate walau kibaba alishe familia yake wala hatishwi na Tamko la MCC.

Wanaoweza kuathiriwa na MCC ni walio katika Utekelezaji wa Sera ya mpango wa Maendeleo ya Taifa,hao ndiyo wanaoelewa Maana ya misaada na Ruzuku za mashirika ya Kimataifa.Kukuza uchumi na ustawi wa Taifa si jambo dogo kama unavyolichukulia,pamoja na Juhudi zetu za ndani za kukuza uchumi na kupambana na umaskini,bado kama Taifa tunahitaji misaada ya kimaendeleo ili tufikie lengo la kulifanya Taifa letu liwe la kipato cha kati ifikapo 2025.

Lengo na mfuko wa MCC na mingine ya aina hiyo,ni kuziwezesha Serikali zetu kupiga hatua kwa kasi kuelekea Maendeleo.Kukosekana au kucheleweshwa kwa fedha hizo toka kwa wahisani wetu,kutapelekea baadhi ya miladi muhimu ya kuchochea Ingini ya Maendeleo kukwama.

Tumeona hapo nyuma tuliponyimwa misaada,serikali ya awamu ya 4 ilirudi kuwa mkopaji katika Taasisi za ndani na kusababisha madhara makubwa kwa waliokuwa wanategemea Taasisi hizo.Mfano: kwa muda mrefu sasa serikali imekuwa ikiendeshwa na kutekeleza miradi mbalimbali kwa kutegemea fedha toka mifuko ya hifadhi ya jamii.Miradi yote ambayo serikali inajinasibu kuwa imetekelezwa kwa fedha za ndani,kinachoitwa "fedha za ndani" ni fedha kutoka katika mifuko yetu ya hifadhi ya jamii.

Miradi mingi ya barabara,Chuo cha Dodoma,daraja la Kigamboni na mingine mingi,imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa kwa fedha za mifuko ya hifadhi ya jamii.Matokeo ya Serikali kujiendesha kwa kutumia mifuko ya hifadhi ya jamii,yamesababisha wastaafu kukosa mafao yao kwa wakati.

Takribani miaka mitatu sasa,mifuko ya hifadhi ya jamii imekumbwa na ukata mkubwa kiasi cha kushindwa kulipa wanachama wao mafao yao mara wanapostaafu.Mama yangu amestaafu mwezi May 2013,hadi leo hajalipwa hata senti pamoja na kalitumikia Taifa hili kwa uaminifu mkubwa.Hivi sasa anaishi maisha ya dhiki wakati alikatwa pensheni ktk kipindi chote cha uhai wa ajira yake.

Hivyo basi,kutokana na nakisi ya bajeti yetu,tusijifanye vipofu wa kutoona umuhimu wa michango ya Maendeleo toka kwa marafiki wetu wa Maendeleo.Pamoja na Juhudi zetu za kukusanya kodi,tusiibeze michango ya marafiki zetu,walio kwenye vyombo vya Utekelezaji wanalielewa hili kuliko Mimi na Wewe.Ni Mara ngapi fedha zinaidhinishwa katika halmashauri zetu,lakini kutokana na ukata wa serikali hazifiki kwa wakati na wakati mwingine hazifiki Kabisa?Ni uwendawazimu tu na mlevi wa kiitikadi anayeweza kubeza mchango wa marafiki wa Maendeleo kwa nchi zetu masikini.
 
Chukua muda kutafakari,siku tukiingia machafukoni kisa mambo ya ubakwaji demokrasia tutawaangukia wao kusaidia kuirejesha amani!Angalia burundi hali ilivyo

Ni kweli mkuu tukivurugana hapa kwa sababu tu ya uroho wa madaraka walionayo CCM tutaanza kulia na kuwataka haohao waingilie kati. Watoe pesa ya kuendesha mazungumzo nk.

Tuna nafasi ya kujitafakari tusiwaone Marekani kama wachawi wetu. Tukitaka hayo maendeleo na democrasi twende na vyote vinavyotuwezesha kufikia malengo
 
tukusanye wenyewe, kwani hiyo ingine si walikuwa wanakula wajanja tu....??
 
Nadhani wafadhiri wetu wako right maana ma ccm kama Nkurunzinza siyo ya kuchekea
 
Bora kuwa na umaskini wa mawazo kuliko kuwa na mawazo ya umaskini. Utegemezi siku zote ni mbaya, na yeyote ambaye ni tegemezi kwa mawazo na raslimali hana tofauti na mtumwa. Hivi ni kweli TZ bila misaada maisha hayawezi kwenda?
 
Habari ilopo ni kwamba Tanzania wamenyimwa msaada wa MCC kwa sababu ya suala la Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na cyber crime legislation.
kwa hiyo wewe unachekelea. ni vizuri kupata hizo hela ila sio kwa kuingiliwa uhuru wetu wa kitaifa.
 
Ni kweli mkuu!

Hatua ya kwanza tuwashukuru wazungu kutunyima pesa yao.

Pia tumshukuru Mungu kutupatia raisi asiye chekea wakwepa kodi na wala rushwa na wazembe.

Tukatae roho ya utegemezi na kutokujiamini. Tunaweza x 1,000,000,000 kujitegemea na kuendelea kama taifa bila kutegemea wazungu!

Easy said than done bro! Mungu kaumba dunia hii ni kutegemeana. Wakitupa na sisi tunawapa. Give and take. Two ways traffic. OK? Marekani wenyewe wanakopa mabenki ya uchina. Magufuli anahitaji hizo pesa wakati akiikwamua nchi kutoka shimo lililotokana na makosa makubwa ya kiuongozi ya zaidi ya miaka 50.
 
Chukua muda kutafakari,siku tukiingia machafukoni kisa mambo ya ubakwaji demokrasia tutawaangukia wao kusaidia kuirejesha amani!Angalia burundi hali ilivyo

Ni kweli mkuu tukivurugana hapa kwa sababu tu ya uroho wa madaraka walionayo CCM tutaanza kulia na kuwataka haohao waingilie kati. Watoe pesa ya kuendesha mazungumzo nk.

Tuna nafasi ya kujitafakari tusiwaone Marekani kama wachawi wetu. Tukitaka hayo maendeleo na democrasi twende na vyote vinavyotuwezesha kufikia malengo
 
Kabla hujachangia hii topic unalazimika kuwa na kibari harari cha kuishi na kujiusisha na mambo ya ndani ya Tz. Kachangie kwenu Kenya.

Rweye unakwepa point na unaonekana mbaguzi gebwe we. Ipeleke Rorya yote kenya kama JPM atakuelewa !!!??? Swala ni kuwa wakweli na si WANAFKI
 
Mi naona hawa huwa wana sababu zao za kutotoa msaada. Siwezi amini eti hiyo ndo sababu. Kwani wao sera zao za mambo ya nje zina hata chembe ya demokrasia?


Ingia kwenye website yao MCC utaona jinsi wanavyofanya kazi na pia nchi ngapi wanazifadhiri.

Moja ya maelezo yao ni:-

What is distinctive about MCC?

MCC is a prime example of smart U.S. Government assistance in action, benefiting both developing countries and U.S. taxpayers through:

Competitive selection: Before a country can become eligible to receive assistance, MCC?s Board examines its performance on independent and transparent policy indicators and selects compact-eligible countries based on policy performance.
Country-led solutions: MCC requires selected countries to identify their priorities for achieving sustainable economic growth and poverty reduction. Countries develop their MCC proposals in broad consultation within their society. MCC teams then work in close partnership to help countries refine a program.
Country-led implementation: MCC administers the Millennium Challenge Account (MCA). When a country is awarded a compact, it sets up its own local MCA accountable entity to manage and oversee all aspects of implementation. Monitoring of funds is rigorous and transparent, often through independent fiscal agents.
MCC forms partnerships with some of the world?s poorest countries, but only those committed to:

good governance,
economic freedom,
and investments in their citizens.
MCC provides these well-performing countries with large-scale grants to fund country-led solutions for reducing poverty through sustainable economic growth. MCC grants complement other U.S. and international development programs. There are two primary types of MCC grants: compacts and threshold programs.

Compacts are large, five-year grants for countries that pass MCC?s eligibility criteria.
Threshold Programs are smaller grants awarded to countries that come close to passing these criteria and are firmly committed to improving their policy performance.



Hivyo tuache kujidanganya kuwa Tanzania tunaweza kujitegemea, bado ni hatua kubwa sana ipo mbele yetu, huenda kizazi chetu kitapita na watotot wetu kizazi chao kitapita. Tusitegemee karne hii hizo ndoto wanazoota watu humu JF ambao wamemezwa na mambo ya kiitikadi kuwa tunaweza.
 
Mimi naona tz wafute tuu cyber crime

Ili iweje? Kusalim amri? Ili kina yericko waendelee kupotosha nchi? Ili vijana wa IT waendelee kuchezea na kuingilia wasikoruhusiwa? Ili Shariff aingie kuwa rais kupitia mlango wa nyuma?
HAPANA.
 
watanzania tuache umbumbu na ushabiki wa kijinga.
Hizo sababu nyingine ni zipi...!!
Tatizo la Zanzibar mnaliona kuwa ni la mzaha?
Ukweli waheshimiwa Lowassa na Mbowe na UKAWA kwa ujumla waliona mbali...ELIMU....ELIMU...ELIMU!
VIVA LOWASSA.....VIVA UKAWA!
 
Salaaam kwa wamarekani. Watatunyanyasa sana, watatupangia sana lakini kama nchi huru tutapambana kwa ajiri ya nchi yetu. Wamenyimwa gesi walitaka tuingie vitani wakati wa uchaguzi sasa roho imewauma, na wataendelea kuelewa tu. Pesa zao wakae nazo ama wapeleke Libya waliko haribu.

Mmarekani hajanyimwa gas mkuu, kaja kwa mgongo wa nyuma. Fuatilia makampuni yanayofanya utafiti wa gas hapa nchini halafu unambie ni wapi Mmarekani hana mkono mfano Exxon Mobil, Chevron, Shellys na zingine zote zilizopo. Hawa jamaa wana mkono mrefu sana kaka na tunalijua hilo fika kwamba hatutakaa tuwe nje ya mikono yao sababu wanamiliki mitaji na technolojia na rasilimali watu.

Msaada umeahirishwa tuu kwa muda na wanachimba mkwara tuu sababu wanajua wanatuhitaji sana sanaa tuu na siye tunawahitaji sana sana tuu. Kwa sasa wanajihubiria kwamba Africa is the Future sasa hawawezi timiliza hayo kwa kuwa mbali na nchi kama Tanzania yenye resources za kutosha amabazo 80% tayari zipo mikononi mwao moja kwa moja ama kwa kupitia mgongo wa nyuma.

Hebu angalia kidogo tuu Symbion kwa undani then utanambia nini wanafanya hawa jamaaa. Na sasa wapo kwenye renewable energy huko sasa usitie mguu kabisaaa. Hali bado tete sana, ila huwa najiuliza kwanini Mrussia katulia sana na hana habari na Africa, sababu yeye ndo the largest distributor wa gas Dunian kwa kampuni yap ya GAZPROM, je haitaki hii gas iliyopo Africa?
 
Hii ndiyo statement ya The Millennium Challenge Corporation (MCC) Board of Directors!

For Immediate Release
December 17, 2015

Renee Kelly
202-521-3880

The Millennium Challenge Corporation (MCC) Board of Directors held its quarterly meeting on Dec. 16, 2015. The Board approved three countries as eligible for compacts and two countries as eligible for threshold programs. Three of the five countries are new partners for MCC and all have worked hard to improve their performance on MCC?s scorecard, which measures countries? commitment to ruling justly, economic freedom, and investing in their people.

The Board selected Cote d?Ivoire, Kosovo and Senegal as newly eligible for compacts. Cote d?Ivoire, which was selected in December 2014 for a threshold program, will now transition into the compact program after showing continued improvement on its scorecard and achieving greater political stability. Kosovo, which passed MCC?s scorecard for the first time after making progress on democratic rights, is a new partner for MCC. Senegal successfully completed its first MCC compact in September and demonstrated improved scorecard performance over the life of the partnership.

In both Senegal and Cote d?Ivoire, the Board recommended that MCC explore potential investments that address regional obstacles to economic growth, in addition to domestic investments, while recognizing the need for statutory authority to optimize regional impact.

The Board also selected Togo and Sri Lanka to develop MCC threshold programs. Togo has shown a clear upward trajectory on overall scorecard performance over the past few years. Sri Lanka has embarked on a remarkable effort over the past year to reinvigorate its democratic institutions, improve governance, and restore protection of human rights.

Nepal, Niger and the Philippines were reselected by the Board to continue developing their compacts. The Board reselects all countries in compact development as part of the annual selection process. The Board deferred a vote on the reselection of Tanzania and Lesotho for compact eligibility until relevant governance concerns in both countries have been addressed.

Finally, the Board reaffirmed its commitment to developing a compact with Mongolia and its support for a strategic partnership with India to advance economic growth and poverty reduction in South Asia.


Kaaaaaazi kweli kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!​
 
Hawa wazungu bwana, wanatuibia halafu pesa yetu hiyo hiyo wanarudisha kama msaada tena kwa masharti, sasa ni bora tupunguze mianya ya wao kutuibia, ili tuishi kwa kuheshimiana.
 
Back
Top Bottom