Kabla ya kuanza ushabiki me nadhani tujifikirie sote kwa kina, ni kwanini hiyo misaada imezuiliwa na impact yake katika nchi yetu kwa huu wakati tuliopo. Je hizo sababu zao zina mashiko?
Tusiwalaumu hao jamaa walioshika makali, kiukweli nchi yetu inahitaji huo msaada sana ili kumsaidia Rais kutimiza ahadi zake alizotoa kipindi cha kampeni, kwa sasa makusanyo ya ndani hayawezi tutosheleza kwa kila kitu, miradi mingi itakwama na ukizingatia kwa sasa tunasuala la elimu bure na juzi Rais kasema zinatakiwa zaidi ya billion 300 ili kutimiliza hayo.
Bado maeneo mengine ya hadi hayajaguswa hata kidogo, sasa haya mapato yetu ya ndani hayatoshi kamwe na kwa sasa yanaweza pungua zaidi sababu hela haipo kwenye mzunguke, the government is not spending, 90% of daily consumables we are importing, sasa ina maana tunahitaji dollar zaidi. Na project kubwakubwa zote zinazoendelea kwa sasa na zitazoendelea wakandandarasi wote ni makampuni ya kigeni, inamaana tena sio hao hao tunawasaidia to export dollars na uchumi mzuri kwenye nchi wanazotokea hao wakandarasi.
Nadhani hao jamaa wa MCC wamewahi sana kufanya maamuzi, wangelimpa muda Mh Rais angetimiliza tuu yote yanayotakikana kupata huo msaada.