Bodi ya Ligi muwe makini na wakaguzi wenu wa viwanja; kuna harufu ya rushwa

Majok majok

JF-Expert Member
Aug 3, 2023
609
1,563
Najiuliza maswali mengi juu ya wakaguzi wa viwanja vinavyatumika kwenye michezo ya LIGI kuu, sielewi uwa wanatumia vigezo Gani kuruhusu matumzi ya viwanja husika

Mfano mdogo ni kuruhusiwa kutumika kwa uwanja wa CCM kambarage mjini shinyanga baada ya kukaguliwa na hao wakaguzi na kuwaruhusu jkt Tanzania kuutumia kwamba umekidhi vigezo

Lakini Cha ajabu umefungiwa Tena Leo baada ya mechi 2 tu kwa maelezo kuwa aujakidhi vigezo na pitch yake ni mbovu

Maswali ninayojiuliza ni kivipi kamati ya ukaguzi uliruhusu utumike na wakati ni mbovu?

Pitch ya uwanja wa kambarage ni ya ovyo Ina maana wakati wameenda kuukagua wao waliona Ile ni kapeti?

Wamekwenda kule kuukagua ama walikwenda kupiga posho tu na kurudi walipotoka?

Uwanja unakaguliwa na unaruhusiwa na kabla azijaisha ata wiki 2 unafungiwa Tena huu ni mzaha.

TAKUKURU wawe wanaingia na uku kwenye michezo Kuna blunders nyingi sana
 
Back
Top Bottom