Kupanda Ligi Kuu kwa timu ya KenGold inadhihirisha kwamba Mbeya ni mkoa wa soka na Vipaji. Kwanini Serikali haijengi uwanja wa kisasa Mbeya?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
47,902
55,816
Timu ya KenGold kutoka Mbeya imekuwa timu ya kwanza kupanda Ligi kuu ya NBC premiership.

KenGold yenye Makao yake Chunya Mbeya imefikisha pointi ambazo haziwezi kupigwa na timu shindani hivyo kutawazwa kuwa timu ya kwanza kutinga Ligi kuu huku mechi za mwisho zikisubiriwa kuamua watakoungana na KenGold na kuchukua ubingwa.

Chini yake Kuna timu nyingine kutoka Mbeya ya Mbeya kwanza ambayo inatumia uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara ambayo nayo inaweza kupanda Ligi kuu Kwa kutegemea matokea ya Pamba na Play Off.

On top of that Mbeya ilikuwa na timu ya Ihefu ambayo imenunuliwa na kuhamia Singida Aidha Mbeya City imemaliza nafasi ya 6 hivyo inajipanga Kwa Ajili ya kupambana na kuhakikisha inarejea Ligi kuu msimu ujao.

View: https://www.instagram.com/p/C6CIES8t4pi/?igsh=YW52MXd2bjRwdjJk

Hoja Chokonozi.
Inakuaje Serikali inautenga Mkoa huu wa Mbeya Kwa Kushindwa kujenga miundombinu rafiki Kwa michezo hasa uwanja wa Kisasa wa mpira ikizingatiwa huu ni Mkoa wa vipaji?

Watu wa Mbeya Wana stahili na ni Haki Yao ukilinganisha na huko kwingine ambako Serikali inapendelea.Ni aibu kuwa na uwanja mbovu kama Sokoine ndani ya Jiji.

images (5).jpeg
images (4) (1).jpeg
 
Kimsingi Mbeya inastahili kwa vigezo vyote kuwa na uwanja wenye hadhi hapa nchini. Sababu kubwa ni kwamba kwa miaka kama 40 sasa Mbeya haijawahi kukosa timu ya Daraja la 1 kuanzia enzi za Tukuyu Stars, na Mecco kwenye 1980- 1990s. Kwenye miaka ya 2000 tumeiona Prisons na Mbeya City na hatimaye ujio wa Ihefu.

Hata mimi naamini kwa population iliyopo, income per capita ya wakazi basi Mbeya ilistahili hata uwanja wa AFCON 2027 kama walivyopata Arusha, Dodoma na Mwanza na Dar.

Shida ya pekee ya Mbeya ni ukosefu wa hoteli zenye hadhi. Tukubaliane tu kuwa Mbeya kuna Guest Houses tu. Kama kuna 3 Star hotel sijui ni ipi kwa Mbeya, forget about 4 & 5 Star
 
Kimsingi Mbeya inastahili kwa vigezo vyote kuwa na uwanja wenye hadhi hapa nchini. Sababu kubwa ni kwamba kwa miaka kama 40 sasa Mbeya haijawahi kukosa timu ya Daraja la 1 kuanzia enzi za Tukuyu Stars, na Mecco kwenye 1980- 1990s. Kwenye miaka ya 2000 tumeiona Prisons na Mbeya City na hatimaye ujio wa Ihefu.

Hata mimi naamini kwa pop[ulation iliyopo, income per capita ya wakazi basi Mbeye ilistahili hata uwanja wa AFCON 2027 kama walivyopata Arusha, Dodoma na Mwanza na Dar.

Shoda ya pekee ya Mbeya ni ukosefu wa hoteli zenye hadhi. Tukubaliane tu kuwa Mbeya kuna Guest Houses tu. Kama kuna 3 Star hotel sijui ni ipi kwa Mbeya, forget about 4 & 5 Star
🙏🙏
 
Pia tunaitaka pamba wana tp lindanda warudi kwenye ligi kuu, mwanza ilipoa sana kisoka, uwanja wa kirumba uchangamke tena. Kuna arusha na moshi zimepotea sana kisoka muda mrefu tangu zama za afc na ushirika nazo ziibuke tena
 
Timu ya KenGold kutoka Mbeya imekuwa timu ya kwanza kupanda Ligi kuu ya NBC premiership.

KenGold yenye Makao yake Chunya Mbeya imefikisha pointi ambazo haziwezi kupigwa na timu shindani hivyo kutawazwa kuwa timu ya kwanza kutinga Ligi kuu huku mechi za mwisho zikisubiriwa kuamua watakoungana na KenGold na kuchukua ubingwa.

Chini yake Kuna timu nyingine kutoka Mbeya ya Mbeya kwanza ambayo inatumia uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara ambayo nayo inaweza kupanda Ligi kuu Kwa kutegemea matokea ya Pamba na Play Off.

On top of that Mbeya ilikuwa na timu ya Ihefu ambayo imenunuliwa na kuhamia Singida Aidha Mbeya City imemaliza nafasi ya 6 hivyo inajipanga Kwa Ajili ya kupambana na kuhakikisha inarejea Ligi kuu msimu ujao.

View: https://www.instagram.com/p/C6CIES8t4pi/?igsh=YW52MXd2bjRwdjJk

Hoja Chokonozi.
Inakuaje Serikali inautenga Mkoa huu wa Mbeya Kwa Kushindwa kujenga miundombinu rafiki Kwa michezo hasa uwanja wa Kisasa wa mpira ikizingatiwa huu ni Mkoa wa vipaji?

Watu wa Mbeya Wana stahili na ni Haki Yao ukilinganisha na huko kwingine ambako Serikali inapendelea.Ni aibu kuwa na uwanja mbovu kama Sokoine ndani ya Jiji.

View attachment 2970835View attachment 2970836

View: https://www.instagram.com/p/C6CBd-3rwXK/?igsh=bGd1OHpsZTM0eWZx
 
Back
Top Bottom