Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,639
- 4,387
Kutokana na changamoto za waendesha Pikipiki, nimeona niwakumbushe tena kwani wengi hufanya mzaha barabarani bila kujua kuwa Mwili wao ndio bodi ya pikipiki!
1. Usikae ubavuni mwa gari, kwa kuwa hutajua maamuzi dereva wa gari anayotaka kufanya. Gari inaweza kupinda kushoto au Kulia bila wewe kufaham - Utagongwa!
2. Usiendeshe katikati ya Barabara kwa kuwa magari yanakimbia sana hivyo unayazuia kuovertake - utagongwa
3. Usiovertake gari na kukaa mbele yake huku ukipunguza mwendo; utagongwa. Ukiovertake gari, ongeza mwendo au sogea kushoto kabisa mwa barabara
4. Usiendeshe bila vioo vya pembeni (side mirror mjini) kwani hutaona gari linalokuja nyuma- utagongwa!
5. Usiendeshe kwa kupanga msitari (moja nyuma ya nyingine) katikati ya Barabara. Mnaweza kuendesha hivyo ila iwe kushoto kabisa mwa barabara.
6. Usichomekee gari ukitegemea lisimame/lipunguze mwendo, sio magari yote yenye break za karibu kama pikipiki. Majuzi hapa mmoja kafa pale Msamvu/Moro kwa ujinga wake
7. Ukiona gari limesimama, usipite kabla ya kujua kwa nini limesimama; unaweza kuta limesimama kupisha gari jingine liingie barabarani...utagongwa!
8. Usibebe mzigo unaopita sana pembeni mwa pikipiki (mbao, mabati, bomba nk) ukiguswa tu kidogo, utasokotwa kama pia, ukipona shukuru Mungu.
Muhimu:
1. Endeshea kushoto (pembeni kabisa mwa Barabara) muda wote, kumbuka magari yanakimbia sana kuliko Pikipiki hivyo ukiwa kushoto/pembeni, yataweza kukupita/kukukwepa bila shida.
2. Narudia tena - endeshea kushoto kabisa mwa Barabara... Pikipiki inaweza tu kuyapita magari kwenye msongamano, au Barabara mbovu za vumbi ila sio highway (Barabara kuu)