Bodaboda mnawahi wapi?

Kalamu Nzito

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
318
662
Leo kwa mara ya kwanza nimeshuhudia mtu anakata roho.

Ajali ya bodaboda na gari ndogo imetokea maeneo ya Kange kituoni mkoani Tanga majira ya saa tisa alasiri.

Bodaboda ame-overtake upande wa kushoto wakati gari ndogo ilikua inakunja kutoka barabara kuu kuelekea barabara ya vumbi huku dereva wa gari dogo akiwa amechukua tahadhari zote ikiwemo kuwasha indicator.

Bodaboda katoka na speed zote upande wa kushoto bila kujua kuna gari tayari inakunja kona mbele yake. Kijana akalivaa gari ubavuni upande wa mbele, akatupwa mbali na boda yake na kutua mzimamzima pembezoni mwa barabara.

Kwakua niilikua nyuma ya gari hilo dogo wakati ajali inatokea eneo, nilisogea mbele na kupaki pembeni kisha nikashuka kwenda kumtazama muhanga wa ajali ile. Damu zilikua zinamtoka kwa nyingi sana puani, mdomoni na masikioni.

Alikua katika mwendo wa kasi mno (takribani 80-100km/her) na mbaya zaidi hakua na helmet kichwani.

Shukrani zimuendee msamalia mwema mwenye gari zenye namba T*** EBN ambaye alijitolea kumkimbiza hospitali. Lakini kwa hali ilivyokua ni wazi kijana alikua amekwishakata roho.

Chondechonde vijana wa Bodaboda kuweni makini tafadhali.
 
Mungu atunusuru.. kwanza ukiona boda anahatarisha usalama wako abiria mkanye.

Juzi kati hapo niko Dar, nimepanda boda.. Dar maroli si ndo nyumbani kwao, kushoto roli, kulia roli plus mafoleni boda anapita katikati.

Nilikuwa naogopa, mwisho uoga ukanizidi nikamuomba tu apite service road.
 
Boda yupo Mbezi anawaza abiria kijiweni kwake Njia4, anawaza wenzake wanampiga bao kwa kubeba abiria wengi, so akili yake haipo Mbezi, ipo kijiweni...

Ndio maana mda wote wapo high!
 
Leo kwa mara ya kwanza nimeshuhudia mtu anakata roho.

Ajali ya bodaboda na gari ndogo imetokea maeneo ya Kange kituoni mkoani Tanga majira ya saa tisa alasiri.

Bodaboda ame-overtake upande wa kushoto wakati gari ndogo ilikua inakunja kutoka barabara kuu kuelekea barabara ya vumbi huku dereva wa gari dogo akiwa amechukua tahadhari zote ikiwemo kuwasha indicator.

Bodaboda katoka na speed zote upande wa kushoto bila kujua kuna gari tayari inakunja kona mbele yake. Kijana akalivaa gari ubavuni upande wa mbele, akatupwa mbali na boda yake na kutua mzimamzima pembezoni mwa barabara.

Kwakua niilikua nyuma ya gari hilo dogo wakati ajali inatokea eneo, nilisogea mbele na kupaki pembeni kisha nikashuka kwenda kumtazama muhanga wa ajali ile. Damu zilikua zinamtoka kwa nyingi sana puani, mdomoni na masikioni.

Alikua katika mwendo wa kasi mno (takribani 80-100km/her) na mbaya zaidi hakua na helmet kichwani.

Shukrani zimuendee msamalia mwema mwenye gari zenye namba T*** EBN ambaye alijitolea kumkimbiza hospitali. Lakini kwa hali ilivyokua ni wazi kijana alikua amekwishakata roho.

Chondechonde vijana wa Bodaboda kuweni makini tafadhali.
Aisee hiyo ajali nimeikuta hapo kange, kijana alikua anatokwa na damu nyingi Sana maeneo ya kichwani, na gari ilomchukua nadhani Ni vitz ilokua imepaki hapo pembeni njia ya kwenda nyuma ya kiwanda Cha kuchambulia mkonge
 
Back
Top Bottom