Bobomoa ya kiama kushuka Kimara nyumba ya Ngeleja ndani, Maige ndani ni malisho ya Tanganyka Packers

Mnaangalia tu hao wawili, hamuoni athari watakayopata majority ya wananchi wa kawaida?

Rejao umenena vema, kama Ngeleja na Maige watalia basi watalia kwa jicho moja moja, tena machozi yao ni ya kitambo lakini hao walala hoi ambao walijenga kutumia mafao ya kiinua mgongo machozi yao hayataisha bali yatatirurika kama kijito wakati wa masika.
Kwani wahusika walikuwa wapi wakati watu wanajenga?
 
Wameacha kuwakamata walio filisi kiwanda cha Tanganyika packers wao wanahangaika na wakazi.
 
Katika swala zima la wavamizi haramu wa ardhi huenda Tamu na Chungu kushukia wakazi wa kimara safari hii, ni baada ya Serikali kuamua kuwakabili wa hamiaji haramu wa makazi na safari hii ni wavamizi wa eneo la Tanganyika packers baada ya wale walalahoi wa madale kubomolewa zaidi ya Nyumba mia mbili, Muda wowote kushukiwa na greda la mji.

Source:
Ramani ya Malisho Tanganyika Packers Jiji wanayo:
Hukumu ya kesi Mahakamani.
Taarifa ya mmiliki mpya wa Tanganyika packers.

Acheni uchangiaji wa kishabiki,bila tafakuri ya kina...hivi hii tanganyika packers mpaka sasa ni mali ya nani?.

Je? Nini manufaa yake kwa umma mpaka sasa maana hata ile nyama ya kopo zamani ikijulikaana kama zao la yanganyika packers corned beef,iliadimika tangia miaka ya 1980,je hii si mbinu ya mafisadi kupora ardhi ya wengi kwa manufaa ya wachache?

Hivi hao idara ya ardhi walikuwa wapi wakati huo wote haya yakitendeka?

Je wananchi wakiishtaki serikali mahakamani kwa kutowajibika ipaswavyo na kuwasabishia hasara na usumbufu itakuwaje?

Naomba wachangiaji tuwe makini na kutomia jukwaa hili kwa kuhabarishana na kuelimishana bila visasi na vinyongo,kati yenu ebu fikirieni kama huko kimara kungekuwa ndio makazi ya mababa na mama zenu mngejisikiaje?

Nadhani kuna haja ya kufuta mtaala wa mass com ili tuwe na wasomi wa kweli

Alamsiki ndugu zangu...punguzeni hasira
 
Back
Top Bottom