Bob Marley vs Lucky Dube

Bob Marley vs Lucky Dube

Ivi lucky dube na bob marley nani alikua mkali na alitamba sana enzi za muziki wake, Binafsi Wakati nakua nilikua namsikiliza sana lucky dube, lakini walionitangulia wanasema hajawahi tokea kama bob marley.. Nini maoni yako nani mkali kati ya hawa jamaa wawili. Kwangu lucky dube ni bora sauti mashairi mpka ujumbe wa nyimbo zake.
Unaweza kumlinganisha bob marley kweli na dube?,unaweza kwenda ujerumani au ureno ukataja jina la luck dube wakakuuliza ni nani huyu?,bob marley kokote kule ukiulizia unaambiwa alikua ni nani
 
Kwenye "Sweet Reggae" kuna mtu anaitwa Beres Hammond huyu mzee ni balaa
Umemsahau na jah qure kwa upande wa sweet regger lakin THE LEGEND BOB MARLEY hakuna kama huyu kwa upande wa regger kwan alichokua anakiimba ni kitu ambacho kipo mpaka sasa na kinatokea ...mafano nailewa sana nyimbo yake ya "so much troble in the world" yani kama alikuwa aniona kesho...Respect to him
 
sikiliza 'don't cry' hapo ndo mtajua lucky dube ni nyoko
 
Tuseme hivi.

1. Nyakati.
Bob na Luck wameishi nyakati tofauti kimuziki hata jumbe zao zilikuwa tofauti kimuziki. Ingawa kwa kiasi kikubwa wote wameimba kuhusu unyanyasaji, unyonyaji(rat race/gun &roses) uhalifu(victims), mapeniz(stir up/got u babe). Bob ni muanzilishi ,luck ni waendelezaji. Tukumbule pia Bob Marley ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuibadili kutoka tradition music ya marastafari--Nyabingi na kuupeleka kwenye commercial music--Reggae.. kina lucky wameimodernise zaid reggae--by then--kama walikuwa kuwa kina Bunny Wailer aliyekua band moja na bob--the wailers--muziki wa bunny ulilaanishwa zaidi kuliko wa bob.

2. Coverage
Bob alikuwa ni world wide icon/luck alikuwa zaid afrika. Kuna nyimbo moja ya Morgan Heritage inaitwa Forever wameittribute kwa Lucky--mule wanakili hawakujua kama kuna mkali wa Reggae yupo Afrika anaitwa Lucky dube

3. Tecnolojia.
Bob ameishi nyakati ambazo teknolojia ya vifaa vya muziki haikuwa imeadvance kama zama za luck dube..

BUT BOB NI MUASISI NI SAWA NA LEO TUULIZANE RANKIM/KRS ONE NA KINA FAT JOE/JA RULE NANI WAKALI.. Lucky kimsingi kama Peter Tosh--asingefariki---ndio angekua wa kulinganishwa nae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reggae music is a mission not a competition... kuna bob, Tosh, Culture, Bunny, Dube, Alpha Blond na wengine wengi kila mmoja ana ladha yake na hisia zake mambo ya kushindanisha wakushi kama team zenu za wanamuziki wa bongoflava ziishie huko huko bongoflevani
 
Ngoja kidogo na mimi nitie neno.....

Tunapozungumzia reggae basi tunazungumzia movements yaani miziki ya reggae ni movements.....

Ndio maana kwenye reggae mashairi ni muhimu kuliko beats kwa sababu kinachokusudiwa ni ujumbe tu......na kama ilivyo movements zinatofautiana kulingana na hadhira au nyakati......
Maudhui ya reggae za kina Bob Marley ilikuwa ni kumkomboa mtu mweusi na kupigania umoja baina na usawa duniani......

Ambapo maudhui ya reggae za kina Lucky Dube zinalenga ukandamizwaji wa haki, usawa na amani kwenye jamii......bila ya kusahau usaliti na ubadhilifu wa viongozi wa kiafrika.........

Kwa kifupi muziki wa reggae huwezi ifananisha na miziki mwingine kwa kuwa yenyewe ni zaidi ya miziki.......

Mwanamuziki wa reggae anaweza hata kupiga show bure ilimradi tu kuwe na hadhira.......

Ni kama kumlinganisha Malcolm X na Martin Luthier King......wote ni wanaharakati na kila mmoja anatumia njia tofauti kwenye harakati zake....lakini likiwa ni moja......
 
Hii ni sawa na kulinganisha dume ka ngombe na dume la mbuzi nani mkali,hawa ni watu wawili tafauti kuwalinganisha sio haki,ingawa bob anabaki kuwa the best ever,lucky dube mshindanishe na kina alpha blondy.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lucky Dube ni muumini kwenye kanisa ambalo askofu ni Bob Marley.

Dube huimba mapambio by default.
 
yeah ehe BOB kumlinganisha na DUBE mmmm hapana,ila DUBE mpambanishe na akina Alpha Blondy etc etc
 
Ushabiki tu hapo. Kila mmoja amefanya kwa uwezo wake na kupata wafuasi hivyo sioni umuhimu wa kuwapambanisha. Wameimba vipindi tafauti, vifaa, midundo, mfumo na aina ya lugha wametofautiana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Time and Space tells.....
Bob;
Kwa wakati wake alitunga na kuimba sana kuhusu Liberation Struggles & Movements za mtu mweusi coz kwa wakati wake hadhi na thamani ya mtu mweusi na haswa bara la Africa ilikuwa chini sana and thats why akaimba sana kuhusu ukombozi. And thats why akaimba nyimbo kama Africa Unite, Buffalo Soldier, Zimbabwe, Redemption Songs etc, etc.

Lakini wakati huo pia kwa kuwa reggea ni nyimbo za dini, mapenzi, harakati na umoja pia akawa anaimba nyimbo kuhamasisha upendo na mshikamano kwa wote nyimbo kama One love, Stir it up etc, etc. So kimsingi Bob focused alot on Liberation.

Lucky Dube;
Wakati wake Liberations sehemu kubwa zilikuwa tayari ila kukawa sasa kuna vitu kama classes & class struggles within the society. And kimsingi wakati wa presentations wa kazi zao Dube alikuwa with a very limited auduence mwa maana kwamba Dube audience yake kubwa ilikuwa based in Africa.

On the other hand Marley had a wider scope of audience. Coverage yake ilikuwa worldwide.
 
Back
Top Bottom