Blog ina miaka 2 lakini hali mbaya!

Ushauri mwingi uliopewa humu hauna uhalisia na umetoka kwa members wengi ambao hawamiliki blog ama website.

Kwanza tambua msingi wa watembeleaji kwenye blog kwa sasa ni Search engine(Google search), kwa maana unapaswa ujue keywords watu wanazoandika kwenye google pindi wakiwa wanasachi kwenye google

Hizi hapa chini ni takwimu za watembeleaji kwenye tovuti yangu ambao wote ni wateja wanaotaka kununua bodhaa fulani
View attachment 2936020
Hawa wote wanatokea google.

Unaiona hii jamiiforums, kwa takwimu za wakati huu (saa tano dakika 45 asubuhi) kuna watembeleaji 9,807 huku wanachama 1,119 tu, unajua hao watembeleaji 8,688 wanatokeo wapi? Ni Google kwa asilimia kubwa

Unajua hata forums zilisemwa zimekufa ila zipo forums zinafanya vizuri mfano Jamiiforums na hata kuna nyingine naiona inaitwa Jamiitalk.

Ni ngumu kueleze kiundani sababu ya watembeleaji kuwa wachache kama bila kuona blog yenyewe
Ukiacha SEO,njia gani nyingine unatumia kupata traffic?hapa namaanisha unaboost au tunashare?
 
Ukiacha SEO,njia gani nyingine unatumia kupata traffic?hapa namaanisha unaboost au tunashare?
Situmii njia nyingine yoyote zaidi ya seo, japo ni risk kutegemea channel moja ya traffic hasa kipindi hiki Google wamekuwa wakifanya updates za algorithms mara Kwa mara
 
Tatizo la watanzania wengi uwa wanakwenda na trend na sio ujuzi wa jambo husika na hii ni matatizo ya kuwa atuna mazoea ya kuweka longterm plan . Maana aitakuwa rahisi mtu kukuamisha mawazo Kwa jambo ambalo aliko katika mpango wako matokeo yake unakuta tayari umepoteza rasilimali fedha,muda ,na msongo wa mawazo unakukumba
 
Back
Top Bottom