Block watu aina hii katika Mitandao ya Kijamii na Instant Messaging App

Block watu aina hii katika Mitandao ya Kijamii na Instant Messaging App

Pole sana, hua si block mtu yoyote kama unaona wewe ona tu.

.
giphy.gif
 
Kwa ujumla mimi natak platiform ambayo nitakuw nayo active sana ni hii jamii forum
Huko facebook napunguz matumiz ya ku post na comment kwa 87%


Mabos wangu 4 washachezea block nasaka staffu ambayo nikama nyoka fulan
 
Kwa ujumla mimi natak platiform ambayo nitakuw nayo active sana ni hii jamii forum
Huko facebook napunguz matumiz ya ku post na comment kwa 87%


Mabos wangu 4 washachezea block nasaka staffu ambayo nikama nyoka fulan
upo vizuri sana mzee baba. tisha sana
 
Mimi hata no ya simu ya boss wangu sijaisave najua nikiingia grp la whtsapp la kazini ntazikuta hivyohivyo kwa wakuda wote wa kazini sina haja ya kuwa na no zao
 
Maisha ni mchanganyiko wa matukio mbali mbali kulingana na nyakati zilizopo, yapo matukio yanayotufurahisha na yapo matukio yanayotukwaza.......

Matukio yanayotufurahisha yanatupa furaha na sababu ya kuishi na kufurahia uhai na afya ambayo Mungu ametujaalia....matukio yanayotukwaza yanatupa huzuni mioyoni mwetu lakini hutuwezesha kukua kifikra na kimaamuzi

Mchanganyiko wa matukio yote haya ndio yanaleta msawazo wa maisha ya mwanadamu.....

Siku utakayoanza kuishi kulingana na mitazamo au utashi wa watu wengine kwenye maisha yako ndio siku utakayojiweka rasmi kwenye jela ya fikra hali ya kuwa upo huru kimwili....

Makwazo, vijicho, husda na wivu ni sehemu ya hulka za kibinadamu kwenye jamii zetu na hazikimbiwi bali kwa kuishi kulingana na nyakati zilizopo........

Ukijitenga na kila lenye makwazo kwako utajikuta umebakia mwenyewe au utajikataa mwenyewe......
 
mimi nawaacha ila sina tabia ya kupost chochote.
 
Mimi situmii kabisa mtandao wowote zaidi ya JF na Youtube pia sifuatilii mambo ya celebrities kabisa achana na kero ndogo'ndogo bali kuna tatizo kubwa zaidi kwenye kutumia social media.

Watu wanaotumia Instagram, Facebook, Whatsapp, tiktok, twitter na mitandao mengine ya kijamii ndio watu wenye huzuni zaidi duniani japo sio wote ukiondoa wafanyabiashara wanaotumia kutangaza bidhaa zao.

Imagine wewe unainga Instagram unakuta picha za watu na marafiki zao au masuperstar wanakula bata mara hotelini mara baharini mara amepiga picha kwenye ndege anaelekea marekani sijui na blah blah nyingine alafu unajiangalia wewe unaona vitu vya ajabu ajabu tu then baada ya hapo furaha yako yote inatoweka unabaki na mawazo tu ya maisha na wapi nilikosea.

Au unaingia tiktok unakuta kila mtu ana girlfriend high class mara watu wanacheza viwimbo vya ajabu ajabu huku wakicheka alafu unajiangalia wewe unahisi kama popo aliyepangoni peke yake na ile pride na furaha yako yote inatoweka ghafla.

Even Elon Musk alisema kwamba siku ya kwanza kujiunga Instagram anaona kila mtu amepiga picha kali huku anacheka kwa furaha alafu anajiangalia mwenyewe anaona humu kila mtu ana furaha alafu mimi niko na mawazo na sad muda wote then unaingia huzuni.
Baada ya hapo Elon musk akafuta account yake ya Instagram.
Elon akasema sababu wale watu wanaishi maisha fake zile picha na videos ziko edited na software kali na kile kinachoonekana kwenye picha ni part tu ya maisha yao na sio kwamba maisha yao yote yako vile.
Imagine mtu powerful duniani anajua kuhusu hili.

Nirudi kwenye point yangu kwamba kila mtu anayefanya show off mitandaoni na followers wao ndio the saddest japo sio wote nadhani.
Ni sababu inawalazimu kufake kila kitu ili kupata approval kutoka kwa followers wao, approval ni zile likes.
Na wasipopata ile approval au likes wanakuwa wanaumia ndani kwa ndani na mawazo juu.
Wanafata mkumbo na kufanya chochote kile ili mradi wawe part ya hiyo jamii ndio maana utakuta watu wanafanya mambo ya ajabu.
Wanaishi kwa tabu sana na sio kama wanavyotaka sababu wasipofuata kile followers wake wanataka basi atakosa hiyo approval na kujihisi yuko alone.

Social Media ni toxic kama hupati faida kutoka kwake, hata baadhi ya waliosoma hii post wanatakuwa wanajiona kama nimewaongelea wao.

Ndio maana mimi natumia JF tu sababu hamjuani na hakuna mtu anapost vitu personal ni mada tu kujadili kitu fulani specific na natumia youtube sababu ni sehemu ambayo inahusu vitu fulani specific na sio mambo binafsi ya watu japo zipo channel zinapost mambo binafsi ya watu.
Very powerful,nilitamani uendelee kuandika.
 
Back
Top Bottom