Block watu aina hii katika Mitandao ya Kijamii na Instant Messaging App

Block watu aina hii katika Mitandao ya Kijamii na Instant Messaging App

smarte_r

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2013
Posts
4,582
Reaction score
12,246
tunaishi katika ulimwengu wa kidigitali ambao umerahisisha mawasiliano.

hii ni orodha ya watu ambao hupaswi ku-interact nao kwenye social platforms.

platform ninazozizungumzia hapa ni zile zenye wafuasi wengi tanzania. nazo ni Facebook,Instagram, Twitter, Whatsapp nk.

HR wako
kama umeajiriwa, usiruhusu HR wako aone content zako unazopost kwenye mitandao ya kijamii. hata kama ni mshikaji wako, piga block haraka sana. ipo siku utakuja kunishukuru.

Mkuu wako wa Idara
huyu ni boss wako, jitahidi asijue mambo yako unayo share kwenye social platforms. try to avoid any casual interaction with him/her on social media.

ipo siku utamuomba ruhusa ya uongo ya siku kadhaa. katika ruhusa hiyo labda
utamdanganya unaumwa, umefiwa na mtu wako wa karibu au unauguza nk, halafu anaona umepandisha picha kwenye status yako upo eneo la starehe unakula bata na rafiki zako.

unadhani atakufikiriaje?.please block this person as soon as possible, you will thank me later.

whatsapp ina option ya ku-select nani aone status zako na nani asione. don't wait to change your privacy settings.

Mfanyakazi mwenzako ambaye hana Maelewano mazuri na wewe
usiruhusu interaction yoyote na mtu huyu kwenye social platforms. keep him/her away.

hata kama atakutumia friend request, usi accept.mpige block instagram, facebook, twitter na whatsapp status.

the only place anaweza kuona content zako ni kwenye whatsapp group la pamoja la idara yenu.

Mwanafamilia ambaye ana wivu sana na mafanikio yako
katika familia zetu za kiafrika ni kawaida kuwa na yule ndugu ambaye hafurahii chochote kizuri kuhusu wewe. this person is a number one hater of your success.

mtu wa aina hii hapaswi kuona status zako whatsapp au picha zako za instagram. piga block fasta.

Hawala/Mchepuko wako(hii ni kwa wale walio ndani ya Ndoa)
sehemu peke ambayo itakukutanisha wewe na hawala/mchepuko wako ni lodge na maeneo mengine ya starehe yenye privacy ya uhakika, period.

hawala/mchepuko wako hapaswi kupata access ya yale unayo share kwenye kurasa zako za mitandao ya kijamii. hata kama mlikutania huko, baada kuanzisha mahusiano, mpige block. pia usimruhusu aone status zako za whatsapp.

Bullies
waliobuni social platforms hawakuweka kitufe cha block kwa makosa. walijua wapo psychopath wanaopata furaha kuwafanyia usumbufu watu wengine. bully anaweza kuwa ni mtu anayekujua au hakujui lakini akaingia katika mkumbo wa kuku bully bila sababu. chochote unachopost yeye ana ki-judge negative. piga block mtu wa aina hiyo.

.......ONGEZA WENGINE.......

NB: njia pekee ya kudumu katika kujiepusha na kero zinawezoweza kujitokeza kutokana na niliyoandika hapo juu, ni kuacha kutumia mitandao ya kijamii.

achana na facebook,instagram na twitter. na kama inawezekana, pia achana na jamiiforum.

if you can't avoid all that, create a ghost account with a fake username.limit yourself from sharing anything on social media. use that ghost profile account silently to view/read other people's content

kama unatumia whatsapp, usipost chochote kwenye status na wewe mwenyewe usijizoeshe kutazama status za watu wengine.
.
 
Acha hizo nasemaje nipe mkono..!
FB_IMG_16375661873040740.jpg
 
Wablock watu ambao wewe binafsi uunaona hautaki status zako wazione hao watu.

Na sio uambiwe tu kwamba block HR wakati wewe unaona kabisa HR ni mtu muhimu wa kuona status zako,maisha sio kukariri wengine wanaaemaje alafu wewe ukaiga,kila mtu ana circumstance zake za maisha hatufanani.

Kuna watu wameblock baba wakwe zao wakati wengine wanaangaliana status freshi tu.
 
Mimi situmii kabisa mtandao wowote zaidi ya JF na Youtube pia sifuatilii mambo ya celebrities kabisa. achana na maswala ya kero ndogo'ndogo bali kuna tatizo kubwa zaidi kwenye kutumia social media.

Watu wanaotumia Instagram, Facebook, Whatsapp, tiktok, twitter na mitandao mengine ya kijamii ndio watu wenye huzuni zaidi duniani japo sio wote ukiondoa wafanyabiashara wanaotumia kutangaza bidhaa zao.

Imagine wewe unaingia Instagram unakuta picha za watu na marafiki zao au masuperstars na celebrities wanaenjoy maisha, wanakula bata mara hotelini mara baharini mara amepiga picha kwenye ndege anaelekea marekani sijui na blah blah nyingine alafu unajiangalia wewe na kujilinganisha nao unaona vitu vya ajabu ajabu tu haueleweki, then baada ya hapo furaha yako yote inatoweka unabaki na mawazo tu ya maisha na wapi nilikosea.

Wale wengine wenye tamaa ya maisha mazuri bila kufanya kazi wala kutoa jasho ndio wanapoanza kupotea hapa.

Au unaingia tiktok unakuta kila mtu ana girlfriend mkali high class mara watu wanacheza viwimbo vya ajabu ajabu huku wakicheka alafu unajiangalia wewe unahisi kama popo aliyepangoni peke yake na ile pride na furaha yako yote inatoweka ghafla.

Even Elon Musk alisema kwamba siku ya kwanza kujiunga Instagram mara anaona kila mtu amepiga picha kali huku anacheka kwa furaha alafu anajiangalia mwenyewe anaona humu kila mtu humu ana furaha alafu mimi pekee ndio niko na mawazo na sad muda wote then unaingia huzuni, mawazo na frustration juu.
Baada ya hapo Elon musk akafuta account yake ya Instagram.

Elon akasema sababu ya yeye kufuta account yake ni kwamba wale watu wanaishi maisha fake zile picha na videos ziko edited kwa effects na software kali na kile kinachoonekana kwenye picha ni part tu ya maisha yao na sio kwamba maisha yao yote yako vile. Imagine mtu powerful duniani anajua kuhusu hili.

Nirudi kwenye point yangu kwamba kila mtu anayefanya show off mitandaoni na followers wao ndio the saddests japo sio wote nadhani.

Ni sababu inawalazimu kufake kila kitu ili kupata approval kutoka kwa followers wao, approval ni zile likes.
Na wasipopata ile approval au likes wanakuwa wanaumia ndani kwa ndani na mawazo juu na kujiona hawana thamani hasa akilinganisha likes zake na za mwingine hapo ndio anaumia zaidi.

Wanafuata mkumbo na kufanya chochote kile ili mradi wawe part ya hiyo jamii ndio maana utakuta watu wanafanya mambo ya ajabu.

Wanaishi kwa tabu sana na sio kama wanavyotaka wao sababu wanaogopa wasipofuata kile followers wake wanataka na kupenda basi atakosa hiyo approval na kujihisi yuko alone, mpweke, asiye na thamani, feeling of emptiness, asiyependwa na yoyote. ni gereza na mfungwa wa kujitakia.

Social Media ni toxic kama hupati faida kutoka kwake, hata baadhi ya waliosoma hii post watakuwa wanajiona kama nimewaongelea wao.

Ndio maana mimi natumia JF tu sababu hamjuani na hakuna mtu anapost vitu personally, ni mada tu kujadili kitu fulani specific na natumia youtube sababu ni sehemu ambayo inahusu vitu fulani specific na sio mambo binafsi ya watu japo zipo channel zinapost mambo binafsi ya watu.
 
Back
Top Bottom