leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,585
- 3,179
Akiongea katika kipindi cha Tuongee Asubuhi Star Tv, Bituro Kazeri anadai:
Nadhani ni wakati mwafaka sasa kutambua kuwa kuna kundi limeamua kuwaaminisha watanzania kuwa:-
[HASHTAG]#Unafiki[/HASHTAG] na uzalendo ni kitu kimoja
[HASHTAG]#Uongo[/HASHTAG] katika siasa ni halari
[HASHTAG]#Uongo[/HASHTAG] wa kiongozi haupiswi kuhojiwa
Watanzania tuamke na kusema hapa hapana.
- Uzalendo ni hali ya kuunga mkono kila jambo linalofanywa na serikali na kama hukubaliani na kinachofanyika basi usiliseme jambo hilo hadharani.
- Amefananisha uzalendo na wa kimakundi kuwa tayari kuunga mkono kwa hali na mali imani ya kundi na kuipigania
- Atolea mfano kukamatwa kwa ndege nchini Canada na kudai kuwa Zitto Kabwe na Tundu Lissu hawakuwa sahihi kusema hadharani kukamatwa kwa ndege walipaswa kukaa kimya ama kuiambia serikali kwa siri
- Uzembe wa serikali haupaswi kusemewa hadharani kama lipo tatizo unaweza kumwandikia barua rais huwa anajibu.
- Ukikuta baba au mama kakaa vibaya hapaswi kumwambia, ni utovu wa nidhamu.
- Kitendo cha wapinzani kusema kuwa kuna njaa haikuwa kitendo cha kizalendo, walipaswa kupeleka maoni yao serikalini na ikatathmini.
- Rais hushauriwa na sio kukosoa
- Uzalendo mzuri ni ule mkosoaji hapaswi kumuaibisha Rais
- Padri wakati anahubiri hupaswi kunyosha mkono na kusema padri umekosea.
- Kitendo cha Zitto Kabwe kutoka na data kuikosoa serikali si cha kizalendo lakini pia hana mandate ya kutoa data hizo, mwenye mandate ni TRA na ndiye tunaepaswa kumwamini.
- Ukosoaji wa hadharani usubiri 2020 kwani ndio mwaka wa kampeni za uchaguzi.
- Mzalendo anapaswa kuunga mkono jambo lolote hata kama unajua sio kweli
Nadhani ni wakati mwafaka sasa kutambua kuwa kuna kundi limeamua kuwaaminisha watanzania kuwa:-
[HASHTAG]#Unafiki[/HASHTAG] na uzalendo ni kitu kimoja
[HASHTAG]#Uongo[/HASHTAG] katika siasa ni halari
[HASHTAG]#Uongo[/HASHTAG] wa kiongozi haupiswi kuhojiwa
Watanzania tuamke na kusema hapa hapana.