Bituro Kazeri: Uzalendo ni kuunga mkono kila jambo lifanyikalo katika Taifa na kutokosoa hadharani

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,585
3,179
Akiongea katika kipindi cha Tuongee Asubuhi Star Tv, Bituro Kazeri anadai:
  • Uzalendo ni hali ya kuunga mkono kila jambo linalofanywa na serikali na kama hukubaliani na kinachofanyika basi usiliseme jambo hilo hadharani.
  • Amefananisha uzalendo na wa kimakundi kuwa tayari kuunga mkono kwa hali na mali imani ya kundi na kuipigania
  • Atolea mfano kukamatwa kwa ndege nchini Canada na kudai kuwa Zitto Kabwe na Tundu Lissu hawakuwa sahihi kusema hadharani kukamatwa kwa ndege walipaswa kukaa kimya ama kuiambia serikali kwa siri
  • Uzembe wa serikali haupaswi kusemewa hadharani kama lipo tatizo unaweza kumwandikia barua rais huwa anajibu.
Update
  • Ukikuta baba au mama kakaa vibaya hapaswi kumwambia, ni utovu wa nidhamu.
  • Kitendo cha wapinzani kusema kuwa kuna njaa haikuwa kitendo cha kizalendo, walipaswa kupeleka maoni yao serikalini na ikatathmini.
  • Rais hushauriwa na sio kukosoa
  • Uzalendo mzuri ni ule mkosoaji hapaswi kumuaibisha Rais
  • Padri wakati anahubiri hupaswi kunyosha mkono na kusema padri umekosea.
  • Kitendo cha Zitto Kabwe kutoka na data kuikosoa serikali si cha kizalendo lakini pia hana mandate ya kutoa data hizo, mwenye mandate ni TRA na ndiye tunaepaswa kumwamini.
  • Ukosoaji wa hadharani usubiri 2020 kwani ndio mwaka wa kampeni za uchaguzi.
  • Mzalendo anapaswa kuunga mkono jambo lolote hata kama unajua sio kweli
My Take:
Nadhani ni wakati mwafaka sasa kutambua kuwa kuna kundi limeamua kuwaaminisha watanzania kuwa:-

[HASHTAG]#Unafiki[/HASHTAG] na uzalendo ni kitu kimoja
[HASHTAG]#Uongo[/HASHTAG] katika siasa ni halari
[HASHTAG]#Uongo[/HASHTAG] wa kiongozi haupiswi kuhojiwa

Watanzania tuamke na kusema hapa hapana.
 
sasa hapo anaonyesha dhahiri ni nan Muhusika wa Shambulio la Lissu.
Kwa kifupi ajuwe kabisa Tanzania sio ile ya miaka 47, sio kila jambo ni ndio mzee.... sasahivi Watanzania tunajuwa kuhoji na kudadisi....kwa Tafsi yake Uzalendo ni Ndio Mzee, Kujipendekeza, unafiki na kupiga ngonjera za kuisifu serekali.
 
Amani ya Bwana iwe nanyi!

Kimantiki kuna hoja yenye kuhitaji tafakuri yakinifu.

Kwa mfano 'si raia wote wa Korea Kaskazini wanaomkubali Kiongozi wao, lakini wamejitoa mhanga kuhakikisha kile Kiongozi anakisimamia kinatekelezeka'.

Kwanini hatujiuzi kuwa wasomi wengi ambao wamepata maharifa yao kupitia kodi za wanyonge si wazalendo?
 
Patriotism: Is it really hypocrisy? Mimi ninafikiri nikimpenda mtu nitamkosoa ili asikosee tena. Mfalme juha alikataa kujijua kuwa yuko uchi hadi alipochekwa!! Tunangojea kuchekwa na nani!!
 
Kaongea ukweli mtupu huwezi ukaisaliti nchi yako kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa.

Makosa ya serikali ya awamu ya tano wewe kama mwanasiasa mzuri unaweza ukatumia kwenye kampeni za uchaguzi mkuu 2020.

Kwa sasa mwacheni Rais Magufuli atekelezee sera zake.
 
Uzalendo ni kuangalia maslahi yako kama u mnufaika ndo tasfiri yake, kazi ya mwanasiasa yeyote ni kuongea na penye udhaifu kwake ndo mtaji.
 
Amani ya Bwana iwe nanyi!

Kimantiki kuna hoja yenye kuhitaji tafakuri yakinifu.

Kwa mfano 'si raia wote wa Korea Kaskazini wanaomkubali Kiongozi wao, lakini wamejitoa mhanga kuhakikisha kile Kiongozi anakisimamia kinatekelezeka'.

Kwanini hatujiuzi kuwa wasomi wengi ambao wamepata maharifa yao kupitia kodi za wanyonge si wazalendo?
Kwahiyo unataka kulinganisha TZ na NK? Basi nasi tutengeneze hydrogen bombs na tutengwe na dunia. Badala ya kulinganisha tz na nchi zilizostawi kiuchumi, kidemokrasia na kisiasa wewe unatulinganisha na nchi isiyoheshimu haki za raia, demokrasia na utawala wa sheria
 
Back
Top Bottom