GE2025 Biteko: Samia ni msikivu, atawapa Katiba mpya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
"Mgombea wetu umetufundisha mengi na umethibitisha kwamba utu kwako ni kipaumbele na pia kazi ndiyo msingi wa maendeleo kwamba hata kama tutakaa kama Taifa tukazungumza mambo mengi tutakavyo kama hatufanyi kazi maendeleo ni ndoto na maendeleo yoyote hayawezi kutokea kama hakuna utu. Umethibitisha utu, umejenga daraja la maridhiano kwenye nchi yetu, kila mtu amesikilizwa hata walioomba Katiba mpya ukasema lisiwe jambo la kutamkwa tu, ukaliweka kwenye Ilani hii ili kwamba liwe deni kwako kwamba katika kipindi kijacho cha miaka mitano utawapatia Katiba mpya kama walivyoomba.

"Mama umetufundisha mengi, umetufundisha kuwavumilia watu, umetufundisha kuwaheshimu watu lakini pia umetufundisha kutenda zaidi badala ya kusema. Wewe ni tofauti na wengi unasema kidogo, unatenda zaidi kwamba katika kipindi chote cha Uongozi wako umekuwa mwalimu wetu wengi kwamba kazi ndiyo utakayopimwa nayo hutapimwa kwa aya utakazozisema au kughani bali utapimwa kwa maendeleo yanayotokea kwa watu tena yasiyotamkwa kwa mdomo bali yanayoonekana kwa macho.

Soma pia: Samia asisitiza katiba mpya itakamilika awamu ya sita

.... Na sisi hapa hatuuchukulii uchaguzi huu poa. Tunauchukulia uchaguzi huu kama uhusiano wa maisha yetu na tutakuchagua kwasababu moja, umetupenda na ukatupendelea. Sisi hatusikilizi maneno ya watu, sisi Bukombe tunajua neno moja tu kuwa umetupendelea, Hatukuwa na soko la Kisasa, Mama Samia ametuletea soko la Kisasa. Tunajua neno moja tu tulikuwa hatuna maji, mama ameleta maji, hatukuwa na Vyuo, Mama ametuletea vyuo viwili tena dabo dabo kwenye Wilaya yetu, Tunajua neno moja, Watoto wetu walikuwa wakitaka kwenda High school ilikuwa lazima waende nje ya Wilaya, Mama ametuletea High school, tunajua neno moja kuwa Bukombe ilivyokuwa na ilivyo leo ni tofauti, Mbingu na ardhi.

"Tumekubaliana tarehe 29 shughuli zote tunaahirisha, tukupigie kura ili tuendelee kufaidi upendo wako."- Dkt. Doto Biteko, Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe Mkoani Geita na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati akimuombea Kura Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Viwanja vya shule ya Msingi Ushirombo Wilayani Bukombe leo Jumapili Oktoba 12, 2025.
 
Hakuna katiba bora ya kupewa na Samia! Kama amegoma kuwapa wananchi Tume huru ya uchaguzi, ndiyo aje awape Katiba bora? Atakachokifanya hapo ni kubadilisha tu jina la hii katiba mbovu ya 1977, na kuiita Katiba mpya.

Wananchi tusikubali kuendelea kudanganywa na huyu mama aliyezungukwa na kundi baya la Wahuni. Kwanza ukimuuliza zile 4R zake zimeishia wapi, hawezi kuwa na majibu ya kueleweka.

Halafu wanasiasa wasituone wananchi hatuna akili. Wananchi tulishapendekeza Katiba tuitakayo tangu miaka ya 2010's! Ni hawa hawa wanasiasa ndiyo waliamua kuuvuruga mchakato kwa kuleta mivutano yao ya kipuuzi.

Kwa hiyo kama ni ishu ya Katiba, basi irejeshwe Bungeni ile Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba, na wataalamu na makundi ya wanazuoni ndiyo wapewe kipaumbele cha kuwa wajumbe wa bunge la Katiba! Badala ya kujaza wanasiasa wabinafsi.
 
😄😄😄😄.atawapa katiba mpya.
Hyo katiba mpya inahusu nini?
 
Huyu mburundi nae atulie, hicho cheo alichopewa kisicho kuwepo kwenye katiba, kisimlevye hivyo.

Huyo Mama Samia, si ndo alisema Katiba ni kajitabu tyuuh, na akasahau hako kajitabu ndo kalikompa yeye Urais.

Lol
 
Maelekezo Maalum kuhusu tarehe 29 Oktoba.

Siku hiyo kazi ni rahisi sana

Viongozi wa CCM tunaishi nao mitaani; Nyumba zao zipo mitaani kwetu, mali zao zipo mitaani kwetu.

Ofisi za CCM zipo mitaani kwetu. Ofisi za Umma nazo zipo mitaani kwetu

VItuo vya kupigia kura vipo mitaani kwetu

Mawaziri, Wabunge na Madiwani tunaishi nao mitaani kwetu, familia zao na ndugu zao tunaishi nao mitaani kwetu

Tukafanye kazi iliyotukuka hiyo Oktoba 29 hadi hawa Mafisadi watuheshimu na wakome kutuchezea na kutuua.

Share na mwenzako
 
Kwa mambo aliyofanya Rais hawezi kutoka katiba mpya alafu suala la katiba sio matakwa ya Rais ni wananchi
 
Rasimu ya Warioba tunataka mfumo wa serikali tatu Tanganyika nayo irejee ulingoni.
 
Ndiyo afaidi utu wa Samia Kwa kumteua yeye siyo sisi watanzania Kwa ujumla anao tutumikia
 
"Mgombea wetu umetufundisha mengi na umethibitisha kwamba utu kwako ni kipaumbele na pia kazi ndiyo msingi wa maendeleo kwamba hata kama tutakaa kama Taifa tukazungumza mambo mengi tutakavyo kama hatufanyi kazi maendeleo ni ndoto na maendeleo yoyote hayawezi kutokea kama hakuna utu. Umethibitisha utu, umejenga daraja la maridhiano kwenye nchi yetu, kila mtu amesikilizwa hata walioomba Katiba mpya ukasema lisiwe jambo la kutamkwa tu, ukaliweka kwenye Ilani hii ili kwamba liwe deni kwako kwamba katika kipindi kijacho cha miaka mitano utawapatia Katiba mpya kama walivyoomba.

"Mama umetufundisha mengi, umetufundisha kuwavumilia watu, umetufundisha kuwaheshimu watu lakini pia umetufundisha kutenda zaidi badala ya kusema. Wewe ni tofauti na wengi unasema kidogo, unatenda zaidi kwamba katika kipindi chote cha Uongozi wako umekuwa mwalimu wetu wengi kwamba kazi ndiyo utakayopimwa nayo hutapimwa kwa aya utakazozisema au kughani bali utapimwa kwa maendeleo yanayotokea kwa watu tena yasiyotamkwa kwa mdomo bali yanayoonekana kwa macho.

Soma pia: Samia asisitiza katiba mpya itakamilika awamu ya sita

View attachment 3487502

.... Na sisi hapa hatuuchukulii uchaguzi huu poa. Tunauchukulia uchaguzi huu kama uhusiano wa maisha yetu na tutakuchagua kwasababu moja, umetupenda na ukatupendelea. Sisi hatusikilizi maneno ya watu, sisi Bukombe tunajua neno moja tu kuwa umetupendelea, Hatukuwa na soko la Kisasa, Mama Samia ametuletea soko la Kisasa. Tunajua neno moja tu tulikuwa hatuna maji, mama ameleta maji, hatukuwa na Vyuo, Mama ametuletea vyuo viwili tena dabo dabo kwenye Wilaya yetu, Tunajua neno moja, Watoto wetu walikuwa wakitaka kwenda High school ilikuwa lazima waende nje ya Wilaya, Mama ametuletea High school, tunajua neno moja kuwa Bukombe ilivyokuwa na ilivyo leo ni tofauti, Mbingu na ardhi.

"Tumekubaliana tarehe 29 shughuli zote tunaahirisha, tukupigie kura ili tuendelee kufaidi upendo wako."- Dkt. Doto Biteko, Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe Mkoani Geita na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati akimuombea Kura Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Viwanja vya shule ya Msingi Ushirombo Wilayani Bukombe leo Jumapili Oktoba 12, 2025.
Muda iliyotakiwa zaidi hajafanikiwa,hapa sijui anapanga hili litokee wakati upi?
 
Back
Top Bottom