hapana mkuu,fahamu kuwa unabii kuhusu ukristo unazidi kuwa dhahiri, pale ulipotabiri haya yote kuwa watu wataiacha kweli na kufuata mafundisho yadanganyayo, na kuwa kama muda usingalifupishwa hata watakatifu wasingeliokoka. tofauti ya ukristo na dini nyingine ni kuwa ukristo umetabiriwa kutoweka wakati imani za watu wengine wakijitabiria kuimarika. na haya yameandikwa katika bibilia na sio porojo tu.hivyo ni ishara kuwa maandiko yanazidi kutimia na kuwa watakaovumilia mpaka mwisho ndio watakaookoka. katika ukristo mungu haangalii cheo chako bali moyo wako, hivyo hata watu wakikupa daraja la juu kama papa, nabii, mtume, mfalme , raisi, lakini mungu anaweza asikutambue kama sauli aliitwa mfalme wa israel lakini mungu hakumtambua bali alimkubali kijana daudi. hivyo si wote wamwitao bwana bwana watakaouona ufalme wake. yesu alishasema ''makwazo hayana budi kuwepo ila ole wake yule akwazae..''. hapa ni ishara kuwa bibilia ilichosema miaka aidi ya elfu 2 iliyopita kinazidi kuwa dhahiri siku hata siku.