Hamerkop ama Fundi Mchundo kwa kiswahili, ni ndege mwenye kiota kikubwa kuliko ndege wote, kina sehemu mbili sebuleni na chimbani na inasemekana anakinakishi kwa hali ya juu sana, zamani ulikua unaweza kuona kiota chake pale makumbushon ya Taifa lakini huwa anajenga rafu sana na ndege wengi hukitumia kiota chake ila adui mkubwa ni nyoka ambaye hula mayai yake
kwa kweli, hapo anatoa ishara ya kuvuta mademu, atazunguka sana kuwasumbua si kama binadamu maji mara moja, fika viunga vya City Garden DSM utafaidi vituko vyao, BUT uwe na muda wa kutosha
unaweza usimpende sana kwa kuwa hana mvuto lakini kwa waliokulia vijijini na hata mijini anapatikana sana huyu, anaitwa common bulbul ay yellow vented bulbul (angalia ana njano fulani kwa chini) kiswahili huyu ndyo shorwe bwenzi (ana kibwenzi)
............upekee wake ni kwamba huyu ndiye song star of africa, ana milio mingi sana na hasa nyakati za asubuhi akishindana na spoted morning thrush