Biography Ya Regia Mtema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biography Ya Regia Mtema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sanctus Mtsimbe, Mar 23, 2012.

 1. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160


  Uandishi wa Kitabu cha Marehemu Regia Mtema (Biography)

  Kamati Teule iliyochaguliwa kuanzisha Taasisi ya Regia Mtema Foundation imedhamiria kufuatilia kuandikwa kwa kitabu cha Marehemu Regia Mtema kufuatia azimio lililoafikiwa katika kikao cha kwanza cha Marafiki wa Regia pale British Council na baadaye kuwekewa uzito katika kikao cha Kamati Teule.

  Kamati Teule sasa inapenda kutoa fursa ya kualika mtu au kampuni yeyote ambayo inaweza kuifanya kazi hiyo ya uandishi kwa uharaka, ustadi na ubora wa hali ya juu. Itahitajika kujua mchanganuo wa gharama zote za zoezi zima.

  Kazi hii inatarajiwa itahusisha kuweka kumbukumbu ya historia ya Regia, Kazi mbalimbali alizofanya, picha nk. nk.

  Kama wewe ni mojawapo wa waandishi wa Biography au unamfahamu yeyote, tafadhali naomba tuwasiliane moja kwa moja kwa PM au kupitia barua pepe sam@danimex.com.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wazo zuri, nafikiria namna nitakavyoweza kushiriki kwani naamini vizazi vijavyo kujua mchango wa Regia.
   
 3. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Karibu sana. Unaweza kutoa Mchango wako wa hali na mali.

  Kama una Mwandishi mzuri unamfahamu tafadhali tujulishe.
   
 4. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri ila maelezo hayatoshelezi, Ushiriki upi? kwa cost zipi? n.k
   
 5. Sabasaba

  Sabasaba Member

  #5
  Mar 24, 2012
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  kuna JF member anaitwa mtambuzi anajitolea sana kutoa matukio mbalimbali ya kihistoria na kesi mbalimbali, kimsingi najua anachokifanya, ni mwandishi mzuri kwa kujitolea, kwa vile umetangaza na mchanganuo wa gharama, basi atakufaa zaidi!!! ni wazo tu!
   
 6. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  bomba la idea natamani ingekuwa tayari mtaani tuanze kununua na kuwekeza kwa ajiri ya watoto wetu na vizazi vijavyo
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nafikiri mngeanza na Wangwe kwanza kabla ya regia..anyway uamuzi ni wenu
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Mtu Mmoja,
  Sitaki kuamini kuwa Tanzania tumefikia kwenye level ya kukashfiana kiasi hiki. Na sitaki kuamini kuwa wewe binafsi ni mtu katili. Inawezekana ulikuwa na hasira wakati unaandika hii post lakini niseme inaleta tafsiri mbaya, inastua.
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Sijaona mahali Santus ama mwingine yeyote ameandika kuwa kitabu kikiandikwa Regia atafufuka katika mwili?
  Na sijui anachoshwaje kwa kukumbukwa?
   
 10. 2

  2015 Senior Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wangwe hakuwa anajichanganya na watu km regia
   
 11. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #11
  Mar 25, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Uandishi uwe wa kuwavutia wasomaji bila kuwachosha. Isiwe uandishi kama ule wa kitabu cha historia cha kawaida tu.
   
 12. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #12
  Mar 25, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ushauri, wape kazi waandishi zaidi ya watatu ili mwisho uje uchague kazi bora zaidi kati ya zilizoandikwa na waandishi hao badala ya kumtumia mmoja tu na kupata ladha na vionjo kutoka kwa mtu mmoja tu.
   
 13. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mimi nadhani ingekuwa vyema endapo ingeandikwa thread then watu wakafunguka kwa kutoa maoni kwa kiasi gani na namna gani walimfaham Rejia mtema. Experiences zitakazo patikana ndizo haswaa ziingie katika uchapwaji!
   
 14. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #14
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hata mie inanishangaza sana watu humu walivyo bize na huyo Regia ! Ni mtoto wa juzi tu, sasa iweje amefanya makuuuuubwa mpaka muunde tume ya vitabu !? Sanasana mtaandika shule alisoma ! Hayo Mahaba yenu bakini nayo moyoni mwenu msimgeuze mradi, ushauri jengeni kisima au shule ili apate sadaka 'tul jaari'ah'
   
 15. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Wangwe ni Mbunge wa kuchaguliwa na Regia ni wa kuteuliwa ! Sasa yupi alikuwa na watu !? Hivi Regia aliwahi kuolewa ? Isije ikawa ....................!
   
 16. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,966
  Likes Received: 1,786
  Trophy Points: 280
  kawepo muda mchache lakini kafanya makubwa..labda kama hukuwa ukifuatilia kazi zake.. na hata cku ya kumuaga pale karimjee wabunge walishauriwa na spika waige na waishi kama regia..nadhani hata yeye alijua hawezi kuishi kama regia..ni vema japo hayupo lakini akaendelea kuishi..kama visima alishajenga mwenyewe..na shule alishachangia mabati..so kama ni sadaka alishaikamilisha mwenyewe..
   
 17. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #17
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hayo makubwa ya muda mchache ni yapi !? Wakati mwingine hata Baba akileta kitoweo nyumbani mnamsifia wakati ni wajibu wake ! Alifanya kazi ya kipato gani mpaka awe na uwezo wa kuchangia mashule na kujenga visima ? Hata EL akifa leo, tutaambiwa na Nape tuige mfano wake ................................. aaaaah ! Mnatuchosha banaa !
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  azo zuri sana

  Ila naona taarifa ipo kimini sana....

  Changanua mpango, resources, timelines (kama zipo etc)

  Ombi binafsi: Napenda kujua kama wanafamilia wameridhia?? kwani wao na hasa twin wanajua a-z ya mtu wetu
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Sera za wanaccm bwana! Sasa kuolewa ama kutokuolewa kunahusikaje hapa?
   
 20. kholo

  kholo JF-Expert Member

  #20
  Mar 25, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 411
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ahsante, hayo pia ni mawazo ya mtu mwenye akili zake timamu. We cannot blem on you maana your thinking capasity myt be low or some gb in yo memory are empty au hukujua ulichokua unaandika au umesahau topic inahusu nini. Topic inahusu kuweka kumbukumbu kwa ajili kwa vizaz vijavyo, kuwaeleza Regia alikuwa nani ktk ulingo wa siasa za tz na kama mbunge, alikuwa na uwezogani binafsi ambao si tu wabunge wote female wa ccm bali hata wabunge 10 male "kama si wote" wa ccm hawakuwa nao, so we need contributio, view, opinion and critics as well.
  IT IS NOT IMPORTANT IF YOU DONT FEEL!!!
   
Loading...