Binti yako wa form I akipata mimba...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,342
38,995
A. Utamtafutia mahali ili aitoe?
B. Utamsaidia kuitunza na kulea mjukuu ili arudi shule?
C. Utamshakizia (kumfukuza) kwa familia ya kijana awajibike?
D. Utamkatishia masomo ili alee mtoto wake?

Itakuwaje kama mtu akiyempa mimba ni wa karibu sanakatika familia yako?
 
Heart

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
2,674
1,693
Personally,nitamkemea sana ili tambue alichokifanya ni makosa tena sana tu.. Kufanyana bila kinga. Kufanyana katika umri mdogo. Na kufanyana bila kuzingatia kuwa kuna magonjwa tele sasahiv. Halafu ama baada ya kumchamba vilivyo..sasa ndo nitafanya mchakato wa kumlea wa kumlea mjukuu wangu,huku huyu binti nikimrudisha shule. Nitafanya hayo yote nikiamin kuwa hilo kosa hatolirudia tena.
 
Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,708
1,282
A. Utamtafutia mahali ili aitoe?
B. Utamsaidia kuitunza na kukea mjukuu ili arudi shule?
C. Utamshakizia (kumfukuza) kwa familia ya kijana awajibike?
D. Utamkatishia masomo ili alee mtoto wake?

Itakuwaje kama mtu akiyempa mimba ni wa karibu sanakatika familia yako?

It can't be undone so forward is the best.
 
Nicole

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
4,274
2,512
kwanza kwa sehemu kubwa itakuwa uzembe wangu kutomlea vyema huyo binti ndo mana akapanua mapaja yake mapema na kusahau masomo...kama mzazi i will b a failure ingawa kuna exceptions ya vibinti ambavyo vinapenda dushelele kuliko shule...
 
nyumba kubwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
10,312
8,344
Kuna mshikaji wangu anasema ni kazi saaana kulea watoto wa kike...yeye ana watoto wawili wote wa kike...na mwenzie mwenye watoto mchanganyiko akaunga mkono hoja...akasema ni very complicated kulea mtoto wa kike...akiomba ela lazima ampe anahofia atapewa na mabuzi...wa kiume akila inatosha akiomba ela anachukua kiboko.

Sasa sijuhi kama kuna ukweli...mimi nachojua sikuwahi wapa wazazi wangu pressure...ila nina madada zangu walikuwa ni pasua vichwa. Hiyo ilikuwa enzi za mwalimu...kwa sasa sijuhi hali ya ulezi ikoje.

Ila once mtoto ameshapata mimba mi naona ni too late...hata kumkanya haina maana tena utapelekea anywe vidonge ajiue bureee. kutoa mimba dhambi; lea mjukuu, akikisha mtoto anarudi shule na asome sana maana ameshapata funzo...elimu ndio itakuwa mumewe kwani tumejijengea imani kuwa ukishazaa kuolewa ni vigumu sana...ajiandaa kuishi single na elimu ndio funguo.
 
mbalisana

Member
Dec 15, 2011
46
42
kwanza kwa sehemu kubwa itakuwa uzembe wangu kutomlea vyema huyo binti ndo mana akapanua mapaja yake mapema na kusahau masomo...kama mzazi i will b a failure ingawa kuna exceptions ya vibinti ambavyo vinapenda dushelele kuliko shule...
, inategemea na situation, malezi ni magumu na mara nyinyi tabia njema ya mtoto ni neema tu ya Mungu, yapo malezi mabaya lakini watoto wa siku hizi Ciello wala sio uzembe wa wazazi ni kupekenyua kwao yasiyowahusu, watoto hawajihurumii. unaweza ukawa na watoto 6 akatokea mmoja kama ulimpa jirani akulee anakusumbua balaa. na unaweza ukawa mlezi mbaya sana lakini ajabu anatokea mtoto mwenye tabia njema tofauti na malezi mabaya aliyopewa. wazazi wanashida sana
 
Nicole

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
4,274
2,512
kabisa, nshashuhudia binti alipata ujauzito akiwa fomu2, akazaa akarudi shule...haikupita mwaka akanasa tena...kuna wengine vichwa ngumu hawajifunzi hata chembe...
Siyo wote ambao hujifunza.

Wengine hurudia makosa tena na tena na kukuacha na bumbuazi.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,342
38,995
Lakini tukiunganisha na ile hoja yangu ya wiki iliyopita - inawezekana binti hajui jinsi mimba inavyopatikana na anaombea kuwa asipate? Je inawezekana wapo mabinti (yumkini wapo wadada wakubwa) ambao wakipata ashki hawajui jinsi nyingine yoyote ya kushughulikia isipokuwa kwenda kupata dushelele! (gademu hili jina linatisha sijui nani alikuja nalo!!)?
 
Nicole

JF-Expert Member
Sep 7, 2012
4,274
2,512
hawajui kwani hawapewi hiyo elimu...kibaya zaidi wanapokuwa kwenye hatari ya kupata mimba (heat period) ndo wanaenda kugegedwa pekupeku ...wangekuwa wanajua nadhani siku hizo wangeshindia maji moto....

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,530
Simpo. Kwa vile ameamua kukua kabla ya wakati wake, basi wazo jema ni kumpeleka kwa mwenzake ili wawajibike kwa shughuli yao. Hapa hakuna cha kuangalia sijui amalizie shule au nini. Tatizo la wazazi wengi ni kuwadictate watoto wao. Mie hulea kwa kuwapa options za maisha. Huwapa black and white of what they can land in if they rat on some people. So if she decided to become a dog why should you fight to make her a lioness?
 
Mpogoro

JF-Expert Member
Dec 7, 2008
386
55
A. Utamtafutia mahali ili aitoe?
B. Utamsaidia kuitunza na kukea mjukuu ili arudi shule?
C. Utamshakizia (kumfukuza) kwa familia ya kijana awajibike?
D. Utamkatishia masomo ili alee mtoto wake?

Itakuwaje kama mtu akiyempa mimba ni wa karibu sanakatika familia yako?

Nimeipenda hii!Nitaenda na B hapo yaani "Utamsaidia kuitunza na kukea mjukuu ili arudi shule".Nafikiri kwangu hii ndio namna pekee anaweza kujifunza kutokana na makosa yake. Unalea mimba,anazaa anaona wenzake wanavyosogea wakati yeye analea lakini wakati huo huo unamjenga kisaikolojia ili aweze fanya shule muda muafaka utakapofika!
 
HoneyBee

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
912
859
Option B. Mimba si mwisho wa maisha. You fall you dust yourself off and move forward. Siwezi kumpeleka kwa kijana kuanza maisha sababu bado ni mtoto ingawa anaweza kuzaa. Nitajitahidi kuwa muwazi kwenye haya mambo mapema sana, akishavunja ungo tu. Sio tu kukemea ngono na mimba, bali pia kumuelimisha juu ya reproduction, na jinsi ya kuzuia mimba. Whether we like it or not, kids will grow up and have sex. We are responsible for giving them the information they need to make wise decisions. Kitu kingine, baba wa binti ni muhimu sana kwenye hii issue. Kina baba kuweni karibu na binti zenu. Tell them they are smart, beautiful and special and they won't yearn to hear it from every man out there. Kuna binamu yangu alipewa mimba na mwalimu wake. Kuulizwa kwanini alikubali kulala na mwalimu alisema "kwasababu aliniambia mimi mzuri". Imagine!

Watch this when you get the chance
Sex, lies and ignorance
 
kiwatengu

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
16,301
12,883
mkuu huku kwetu kusini watoto wanahusudu sana ngono kwa sababu wanafundishwa na wazazi wao, u cant believe mwaka huu 2012 tu! watoto wa form one wa 2 na wa form two wa 5. wa shule moja! wamepata mimba, acha hao ambao wamekimbia shule bila kupimwa!!
 
snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,377
22,819
well!
binti akipata mimba mrudishe shuleni akasome!
huwezi amini atakuvokusuprise kwa kuwa binti anayejitambua ajabu!
ila ni experience ngumu maelezo hakuna,
kulea mtoto ukiwa mwenyewe mtoto!
DAH! honeyBee na The Boss u speak my mind i see!
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,538
13,440
hawajui kwani hawapewi hiyo elimu...kibaya zaidi wanapokuwa kwenye hatari ya kupata mimba (heat period) ndo wanaenda kugegedwa pekupeku ...wangekuwa wanajua nadhani siku hizo wangeshindia maji moto....

Umenikumbusha mbali, kwenye hiyo Maji ya Moto.

About the topic, thank God kuwa siku hizi kuna options ya kukatisha masomo na kuendelea; ila kwa zamani wazazi wengi waliwasaidia kutoa mimba za binti zao.

Siku hizi inapungua sana kwa vile uwezekano wa kurudi shule.
 
andate

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
2,651
981
Umenikumbusha mbali, kwenye hiyo Maji ya Moto.

About the topic, thank God kuwa siku hizi kuna options ya kukatisha masomo na kuendelea; ila kwa zamani wazazi wengi waliwasaidia kutoa mimba za binti zao.

Siku hizi inapungua sana kwa vile uwezekano wa kurudi shule.
Thank to Ali Hassan Mwinyi, yeye ndiye aliruhusu mwanafunzi(hata wa shule ya serikali) kuendelea na masomo baada ya kujifungua, imewasaidia wengi sana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom