Binti anapouona utupu wa baba yake . . . . !!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,261
2,000
Siku ya tukio,baba aliaga asubuhi kuwa anakwenda kazini,baba ni mfanya biashara wa simu za viganjani
"
Ilipofika muda wa mchana mama yake na binti akamuagiza aende kwa rafikie mama yake ili akamwambie awahi kwani walikua na miadi ya kwenda msibani.
"
Mama wa binti huyu hakutaka kumpigia rafiki yake simu kuhofia kuambiwa yuko njiani wakati mtu hajaoga.
"
Pia nyumbani kwa rafiki yake hapakua mbali,hivyo hakuona vibaya kumtuma binti yake
"
Binti alipofika nyumbani kwa rafiki yake mama yake akaona apitie nyuma ya nyumba ili azungumze na mwenyeji kupitia dirishani kisha arudi fasta.
"
Binti alipofik alikwenda moja kwa moja dirishani,alipotupa macho ndani kabla hajazungumza kitu,alimuona baba yake akiwa mtupu kabisa akiwa kitandani na rafiki wa mama yake.
"
Walioko ndani hawakumuona,ilibidi arudi haraka alikotoka.
"
Alipofika akamwambia mama yake kuwa hajamkuta rafiki yake.
"
Sasa binti anajiuliza kama amwambie mama yake,lakini pia anajiuliza kama atapata laana kuuona utupu wa baba yake "aksidentale"!
"
Nimemwambia atulie asiseme chochote kwani kusema kuna maana ya kuwatenganisha wazazi wake.
"
Kuhusu laana nimemwambia asihofu kwani hakukusudia kuuona utupu wa babae,hivyo hakuna laana.
"
Wewe una mawazo gani hapa?
 

Mu-sir

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,621
2,000
Asimwambie mama yake bali amwonye yule mwanamke kama anaweza au atumie mtu mwingine kwani sio vizuri lakini akimwambia mama yake sio vizuri ataleta migogoro home
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Hakuna laana yoyote! Laana inatokana na masononeko ya mzazi. Kitendo cha mzazi kusononeka kwamba bintiye ameona utupu wake ndiyo husababisha laana. Kama binti ameona kwa bahati mbaya na amenyamaza kimya basi hakuna chochote kitakachotokea, zaidi ya msongo wa mawazo wa kwake binafsi tu.

Lakini siku atakapotamka neno kwa mamake au kwa watu wengine kiasi cha kumfanya babake ajue kwamba bintiye aliuona utupu wake, huo ndiyo utakuwa mwanzo wa matatizo. Hata kukuambia wewe kafanya makosa sana. Ole wake babake akijua kwamba alimuona akiwa uchi!
 

Chum Chang

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
999
0
Ili awe na amani lazima lisemwe kwa watu wazima aidha kama wewe ni mtu wa makamo basi kafanya vizuri sana na atasahu mda si mrefu aidha wewe na yeye lifikisheni kwa mtu mnae muamini najua atatoa nasha zake na bint atakuwa na amani
Kuh lana sidhanikama kuna lana yoyote itakayo mfika
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,813
2,000
Maskini, anahitaji ushauri nasaha. Kwa mtoto wa kike na babake, that is traumatising. Nae muambie tabia mbaya kuchabo madirisha ya watu. Sio vizuri kukaeibia sirisha la mtu huku unaangalia ndani, angewwza kumkuta uchi hata huyo mama akiwa alone.

Na hahitaji kumuambia mama. Ila huyo mama mwingine dawa yake ni kumpa body lingua tu. Kila ukimuona huna time nae afu unamkata jicho tu. Atajistukia na watabaki wanahisi kama unajua, ila usiwakosee heshima.
 

Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
60,628
2,000
Hapo wala hakuna ugumu sana, zaidi ya athari za kisaikolojia ambazo huyo binti atakua amepata.
Muhimu ni atafute nduguze wenye busara, wakampige masingi huyo mwanamama jirani.
 

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,261
2,000
Asimwambie mama yake bali amwonye yule mwanamke kama anaweza au atumie mtu mwingine kwani sio vizuri lakini akimwambia mama yake sio vizuri ataleta migogoro home

Unadhani ni rahisi kumvaa mwanamke anae"tembea" na baba yako?
Kwanza kiafrika yule ni mama yake,kuna ugumu hapo!
 

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Jul 28, 2008
2,502
1,195
anyamaze kimyaaa asifungue mdomo hata siku moja. tatizo ni kwamba, akimwambia mama yake u ndugu zake, babake akijakusikia kuwa alionwa utupu wake na binti wa miaka 24, itamharibia sana mahusiano na baba yake, baba yake itamsononesha maisha yake yooote na babake hata kuwa na raha yeyote hata kumuona. atakosa upendo wa baba kwasababu baba atapoteza ujasiri mbele zake maisha yote. akimwambia mamake, mamake atawaka tu mwezi mmoja baadaye watapendana na baba yake watakuwa kitu kimoja na kumgeuka uyu binti na wataanza kusema kuwa alitakiwa anyamaze kwasababu alitaka kuwatenganisha. ukisambaza utapata shida sana na utaathirika kisaikolojia zaidi ya hapo ulivyo sasa. nyamaza kimyaaa maisha yako yote. usimwambie mtu yeyote.

mbona watu wengi wameuona utupu wa wazazi wao...ni africa tu, ila ulaya wazazi uwa wanakutwa wakiduu mara nyingi tu, wakienda kuogelea mbona midudu ya baba zao inaonekana imeduna waziwazi?...lakini kwa africa ni embarrassment ambayo haielezeki hivyo nakushauri nyamaza kima tafadhali.
 

waubani

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
542
250
Kwa hiyo wewe unaona ni sawa kwa mtu anaejithamini kukutwa na hali kama hii?

Hivi unajua kuficha uchi ni ustaarabu tuu ulioletwaga na wazungu Africa? Generation nyingi zilianzia kutembea uchi uchi JE walikuwa wanalaaniwa?? kama uchi ni laana binadamu wangezaliwa na nguo.MACHO HAYANA LAWAMA KAMA MATENDO
 

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,261
2,000
Hivi unajua kuficha uchi ni ustaarabu tuu ulioletwaga na wazungu Africa? Generation nyingi zilianzia kutembea uchi uchi JE walikuwa wanalaaniwa?? kama uchi ni laana binadamu wangezaliwa na nguo.MACHO HAYANA LAWAMA KAMA MATENDO

Unaamini katika dini?
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,676
2,000
hakuna cha laana wala nini, tena mie ningemvaa mdingi na kumchimba biti......namweleze nikimuona tena tu namwambia maza, then nampa warning na small hausi....meanwhile namwambia maza kuwa makini na shosti wako sio mtu mzuri tena maneno hayo nitamwambia maza mbele ya mdingi.
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,813
2,000
hakuna cha laana wala nini, tena mie ningemvaa mdingi na kumchimba biti......namweleze nikimuona tena tu namwambia maza, then nampa warning na small hausi....meanwhile namwambia maza kuwa makini na shosti wako sio mtu mzuri tena maneno hayo nitamwambia maza mbele ya mdingi.

hahaha, aminia. Mbona utaanza kumblackmail mdingi. Ukisema kitu tu anajump. Aisee, watu wabaya. Nilivyo na wivu na babangu, ntakufa!
 

promiseme

JF-Expert Member
Mar 15, 2010
2,709
1,195
Jamani mashoha wengine!! ah mie ndio mana staki mashosti wanizoelee mumewangu,yani anakosa hata roho ya imani kwa shosti wake sasa kwa lipi mpaka amsaliti shogake? huyo binti kama ni mie sina haja yakutafuta shangazi wala mjomba kumweleze 24yrs ni mkubwa na anaweza kumueleza Baba yake bila hata kumwambia kua nimekuona uchi au umevaa nguo
muhimu hapa ni usaliti sio kumuona uchi,na binti nae pia anamakosa huwezi kwenda nyumbani kwa mtu ukachungulia dirishani hata kama angekua dadaako sio tabia nzuri.............
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom