Habari za usiku note,
Natumai mwisho wenu wa wiki unaenda vizuri.
Bila kupoteza maudhui, hii ni kali kuliko sigara looh....
Humu JF ndo nimekutana na binamu nyama ya hamu. Na hii imedhihirisha atafutaye hachoki akichoka keshapata. Kuna binamu yangu wa mbali kidogo mie bila kujua wala kutambua kumbe ananipenda bana, na pendo hilo sio nwee wala nwii ni pendo la mapenzi. Mie najua utani tuu, alipoona simuelewi si akaanza kunifukunyua.... akajua ID yangu ya JF na akaanza kunichombeza. Nilimpotezea nikijua ni milupo ya humu JF hakukata tamaa.... mwaka mzima ananifukuzia nikasema isiwe shida njoo SA as a date kisha baada ya hapo tutaona itakuwaje. Akaniambia hataki kufikia hotelini na akasisitiza afikie kwangu.
Nakatisha maelezo na kiufupi ile nimetokea Ortambo airport kumpokea si ndo nashangaa ni binamu....... macho yalintoka. ...
Kwanza mdogo kwangu miaka 10 nikamwambia kwangu sikupeleki utafikia hoteli. Tumebishana nikamwambia ukiniletea mizengwe mi naomba emergency off days naenda zangu TZ nakuacha hapa. Ndo akakubali kufikia hoteli.... baada ya majadiliano ya kina.... binamu akataka nyama ya hamu.
Nilijikuta nampiga keleb moja (kibao cha shavuni) kisha nikamtukana na kuondoka. Binamu kanichefua maana mi simpendi na ni mdogo kwangu halafu anaanzaje kuwaza ngono kwa binamu yake ambaye ni sawa na dada yake?
Nimemblock kwenye njia zangu zote za mawasiliano na amenifanya mawasiliano yoyote yanayonitafuta ambayo siyafahamu basi sijibu wala sipokei yaani nakacha.
Sitaki hata kujua kama bado yuko SA au ameshaondoka.... maana alikuja jana jioni.
Au mie sikuelewa nyama ya hamu ni nini labda kama sio matusi? Mnisaidie kunielewesha ......
Kasie.