Binamu ni nyama ya hamu?

Umeambiwa binamu ni nyama ya hamu, lakini wakati mwingine inabidi mtu utafakari zaidi japo ni halali yako.
 
Hakuna mila za kitanzania. Kaulize wazee wa kwenu. Kuna makabila hata dada tu wa mama mdogo unajiolea kwa raha zako.
 
hapa JF utapewa majibu mengi sana,mengine sahihi mengine ya kupotosha,but kimsingi ni wewe au nyie kwa pamoja kuongea na wazazi,kwa sababu suala la kuoa binamu linachukuliwa tofauti kutoka kabila moja na jingine,mimi kwetu nina mjomba na baba mdogo wote wameoa binamu zao na life linasonga(usiniulize kabila langu,ni m-TZ) kwa hiyo ulizia kwa wana ukoo wako utapata majibu sahihi zaidi!!!!
 
Kama kampenda, mwambie inaruhusiwa, aende kwao akachumbie kama kawaida, na hiyo si kwa waislamu peke yao hata wakristo wanaoana, mm dada yangu kaolewa na mtoto wa shangazi yangu, na nasikia shangazi alikuwa anampenda tangu akiwa mdogo. Na wamefunga ndoa ya kanisani katoliki.
 
Mi siungi mkono ila nilivyouliza kuna mtu aliniambia kuwa binamu si ukoo wako kwa hiyo waweza kuonja ila si kuoa
 
Ni upuuzi binamu yako kumwita nyama ya hamu!
Binamu zangu tunaheshimiana sana na tunapendana sana; kuna mambo ambayo siwezi ku-share na m2 mwingine tofauti na binamu yangu ila si mambo ya kuwa mtupu bila nguo.
 
Back
Top Bottom