Binamu ni nyama ya hamu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binamu ni nyama ya hamu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tall, Mar 29, 2010.

 1. T

  Tall JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Kuna jamaa yangu hapa yupo standby anasubiri ushauri ili afanye kweli/achumbie.

  Bado hawajafanya lolote hadi sasa(HAWAJAGUSANA) ndio maana spidi yake kali, yaani kilomita 1000 kwa saa. Mchumba anaemtaka ni binamu yake kabisa.

  Bahati nzuri hapa JF kuna mashehe,wachungaji,watu na busara zao na watu wa kila kabila,mnasemaje RUHSA KUOA BINAMU AU SI RUHSA?
   
 2. bht

  bht JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mmh!!!
  waarabu hao?
   
 3. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Mimi Mchungaji na mwana-kabila langu mzuri sana, yaani naijua mila vizuri..........kwetu ni kosa kubwa, haitakiwi hata kidogo.......sijui wengine
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kama ni waislam wanaruhusiwa kwa sana tu na dini yao kuoana.

  and i do agree binaamu ni nyama ya hamu (dont ask me how) heheh
   
 5. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Huyo ni sawa tu na dada yako!

  Leo umeanza na binamu kesho utatwambia mtoto wa babamdogo!


  Mbona wanawake wazuri na wafaao wengi tu? Hiyoni tamaa tu imewafunika!
   
 6. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Asante Mkubwa kwa hapo kwenye blue, pamoja daima
   
 7. bht

  bht JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hii mpya sana kwangu G...

  nidhani ni tabia ya waarabu tu and has nothing to do with Islam!!
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  muulizeni dini yake kwanza.........kama ni muislam hana tatizo, x-paster alituwekea aya hapa inayompa ruhusa ya kufanya hivyo. (akija am sure atatumwagia tena)

  ila kimaadili watu wengi wa bara wanaona ni kama ndugu na haipendezi, lakini watu wa pwani na visiwani wanaoana binaamu bila wasi wasi wowote.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0

  bht, uislam haumshurutishi mtu kuoa binamu wake au mtoto wa shangazi, lakini unakupa ruhusa ukitaka.

  ndo maana hiyo tabia iko sio kwa waislam waarabu tu, hata waislam weusi watu wa west africa ( hasa hapa nazungumzia mfano wa watu wa Senegal nnaowajua) wengi wameoana binaamu, because they have a right katika misingi ya dini yao.
   
 10. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  binamu? hiyo ni dhambi mbaya sana! aachane nae tena wakatubu! kijijini kwetu unatakiwa uchinje ng'ombe kutoa nuksi!
   
 11. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Kaka/dada yangu, hebu nifafanulie hapo kwenye blue tafadhali.

  Umenitoa kwa knock out! Please do the needful.
   
 12. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  zamani ilikuwa kawaida kuoa ndani ya familia...... yaani kuoa dada yako ama binamu yako...... na hii ilichangiwa zaidi na uchache wa watu (rejea zama za adamu na nuhu)..... laini baada ya wanadamu kuzaliana na kuongezeka sana ilifanywawa machukizo kwa Mungu na wanadamu (rejea zama za musa)......... hivyo hadi leo ni machukizo....

  Lakini kitaalam........... kwa binamu yako kuna uwezekano mkubwa sana wa kupatikana dominant gene za ukoo wenu amabzo pia zinapatikana kwako............ matokeo yake yataonekana kwa vizazi vyao kama watajaliwa watoto wani watakuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na matatizo ya genetic imbalances na hivyo genetic disorders............

  kwa ujumla tunaweza usema watoto wao wanaweza kwa viumbe dhaifu comparatively........... (comparatively weak breeds) wakiwa na uwezo mdogo wa IQ, kinga ya mwili NK...... haya pia yatategemea recessive genes zitakuwa na nafasi gani katika respective metabolism.....

  Matatizo kama haya ndiyo wazazi wetu waliamini ni laana kuoa mtu wa damu moja na wewe kwani kama walibahatika kupata watoto, basi waalipata watoto dhaifu, .............. imani kama hiyo ilishamiri kutokana na uelewa mdogo wa facts za kisayansi za kuchanganya damu...

  Leo kutokana na uelewa wa kisayansi, inathibitika kisayansi pasipo shaka kuwa technically si vyema kuoa mtu wa ukoo mmoja na wewe..........
   
 13. bht

  bht JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mwana riadha
  mwana kamati
  aaaaah nini sasa huelewi hapo, punguza ninihiii biggy
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
 15. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Aisee binafsi naona ni kinyaa kabisa; cousin wangu nimeanza kumwona since tukiwa 3yrs old; na hata simtambulishi kama cousin; namwita Dada! sasa mtu kama huyo unaanzia wapi kumtamani? Well mshauri aachane na na huo upuuzi; kwa sababu za kisayansi na hata za kijamii!
   
 16. D

  Dear Member

  #16
  Mar 29, 2010
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Lol hii ni balaa,
  kwa kweli mbona kuna wanawake wengi tu huku mjini wamekushinda nini hadi utake kula na ndugu.
  unajua kama sisi familia zakiswahili za kubebana tokea mkiwa wadogo na binamu yako unamuona kama kaka yako kabisa,tena unamtambulisha kwa watu kuwa huyuy ni kaka yangu.
  sasa inakuwaje mnataka kuoana,
  pili hii ni inawezakuleta matatizo ya kwenye ukoo kuna magonjwa ya kurithi kama albino,kansa,sikoseli,kifafa na kadhalika yanaweza yasiishe maana watoto wenu watazaliwa na chembechembe za matatizo hayo kwa sababu damu ni moja,lakini kuna chance kubwa ya kuepuka kama ukiolewa na ukoo wa mbali kutofautiana matatizo ya kurithi,
  na zamani kama sisi kwetu walikuwa tena wanakataza wazee kuoana kama mmetoka kijiji kimoja kwa kuhofia kuwa mkawa ndugu.yaani mke wako anatakiwa atoke kijiji kingine cha mbali
   
 17. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Mwambie Dear; labda ata reconsider!:mad:
   
 18. A

  Abraham Lincon Member

  #18
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heri ya mwaka mpya! Natumaini muwazima wa afya njema. Nauanza mwaka kwa huu msemo wa binamu nyama ya hamu ambao umezoeleka sana hapa nchini Tanzania. Yapo baadhi ya makabila ambayo nimesikia yanaruhusu ndoa za mtu na binamu yake lakini pia yapo makabila kama kabila langu yanayoamini kuwa binamu ni ndugu wa damu na kwamba hawaruhusiwi kabisa si tu kuoana bali hata kukutana kimwili (nadhani unaelewa ninachomaanisha hapa). Rafiki yangu ni moja kati ya watu ambao amekumbwa na mkasa wa mapenzi unaohusisha binamu. Mapenzi yao yalianza kama igizo lakini baadaye binti akapata ujauzito na sasa ana mtoto kidume mwenye umri wa miezi sita. Aliyeanzisha mchezo alikuwa msichana kwa kigezo hicho cha binamu nyama ya hamu. Alivaa kihasarahara na kujipitishapitisha mbele ya binamu yake kwa lengo la kuamsha hisia za kimapenzi za binamu yake kwake. Baada ya kuvumilia kwa muda fulani, binamu uvumilivu ukamshinda kwani msichana aliumbwa akaumbika kikike hasa. Wanaume kadhaa wa kadha walimtupia macho kila alipokatiza. Baada ya kuonja binamu akachonga mzinga na matokeo yake ndiyo huyo mtoto wa kiume akazaliwa. Binti japo si muaminifu katika masuala ya mapenzi alimpenda binamu na hata ndugu walipotaka kujua mimba ile aliyobeba ilikuwa ya nani alimtaja binamu yake. Mtoto amefanana sana na binamu kiasi cha kutosha kuamini ni mtoto wake. Ndugu wamesikitishwa na kitendo hicho lakini wameamua kutoshupalia sana jambo hilo wakiamini msemo ule 'maji yakimwagika hayazoleki'. Hata hivyo hawaafiki ndoa kati yao. Binamu anajutia sana kitendo alichofanya na anaomba ushauri na mtazamo wenu wana jamii. Japo kitendo kilishafanyika, lakini, je, ni sahihi binamu kumkamua binamu wake? Kwa nini na afanye nini hivi sasa? Ni matumaini yangu atapata ushauri mzuri toka kwenu wanajamii. Ni matumaini yangu pia ushauri huo uta'base' katika misingi mbalimbali kama ya kidini, kiutamaduni nk. Mungu awabariki.
   
 19. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wakati mwingine tuyalaumu na mazingira maana kama hawa watu wangekuzwa katika dhana ya kuheshimiana kama ndugu basi huyo dada asingelikuwa anavaa kihasara na huyo kaka angemuheshimu huyo dada kama ndugu na kama dada, sasa yakutokea yametokea, tamaa imeshachukua mimba ikazaa mauti, No way! wawaruhusu waoane kwa manufaa ya huyo mtoto, maana mtoto kashazaliwa haibadiliki tena na malezi ya upande mmoja si mazuri katika dunia ya leo.
   
 20. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  maji yamekwisha mwagika
   
Loading...