Binadamu hatoweza kuishi nje ya Dunia, labda afanye hivi.....

samsun

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
7,386
Reaction score
5,968
Naamini mko poa,kumekuwa na juhudi za mataifa mengi yaliyoendelea kisayansi na kiteknolojia za kuchunguza na kufatilia mambo ya anga za mbali ili pamoja na mambo mengine,lakini kubwa kuliko yote ni kuona kama kuna siku binadamu atahama hapa Duniani na kuweza kwenda kuishi ktk anga za mbali.

Mimi nasema haitowezekana ktk hali hii ya binadamu wa mifupa na nyama.Hebu tuangalie kwanini nasema hivo,kwa mfano tunaambiwa ili tuweze kufika ktk Nyota iliyo karibu yetu kabisa itakuchukua safari ya MIAKA 4.2 YA MWENDO WA MWANGA, sasa fanya hesabu hii hapa. Mwanga unasafiri kwa kasi ya Kilomita 1,080 milioni kwa saa = na miles 671 milioni kwa saa au ni sawa na kusema 186,000 per sec. Kwahiyo tufanye hivi, 671 milion miles per/hour x 24 x 365 x miaka 4 na miezi 2 = (jibu) ????.

Nadhani hapo mmeona jinsi hesabu za kukituma tu chombo kwenda kuchunguza ilivyo na ugumu,sembuse kupeleka binadamu ambaye anatakiwa kula kila baada si chini ya masaa 7 -12 na hiyo safari haina kupumzika sehemu ni non stop.Pia atakuwa anapitia ktk hali za hewa tofauti tofauti.

Mimi nadhani binadamu labda aanze kufikiria kuwahusisha viumbe wengine ktk azma yake ya kujua huko anga za mbali kukoje na kuna nini,kwa mfano labda kuwatumia majini au wanga na hata wachawi ili kufika huko kinyume cha hapo binadamu aondoe kichwani mwake kwamba ipo siku atafika huko.

Wewe unaonaje au unafikiriaje..... haya tiririka.
 
Mkuu una hoja moja tu ya umbali. Kwanza, nje ya dunia kisayansi ni kuanzia anga za juu (space), ambako tayari binadamu ameishi kwa mwaka mzima. Pili, nyota na sayari ni vitu viwili tofauti. Binadamu ana-explore habitable planets na siyo nyota, kwa sasa Mars imepewa priority kwa sababu ya ukaribu na tabia zake (Mars inafikika kwa miezi kadhaa tu).Hoja ya umbali ni sawa, lakini hujaweka angalizo la teknolojia mpya. Kuna uwezekano ikagunduliwa teknolojia ya kusafiri angalau fraction ya speed ya light. So, si suala la "hatoweza" ni suala la lini ataweza.
 
Mbn wadau wapo international space station wanakaa mwaka au zaid wanapokezana..au space still ni dunian mkuu?
 
Umepiga mahesabu ya kufika kwenye nyota, hebu tupe na hesabu za kuifikia sayari ya Mars alafu ndo tuanze mjadala
Umbali kutoka Duniani hadi Mars huwa unabadirika mno kwani hakujawa na vipimo maalum,lakini inaelezwa kuwa zinapokuwa karibu kabisa na hii inakuwa kila baada ya miaka miwili kutokea ukaribu huu ni 33milion miles to 55milion miles, na zinapokuwa mbali ambao ni umbali wao wa kawaida ni 225milion km to 401milion km na muda wakwenda ukikisiwa ni wa miezi 6 - 8.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Mkuu una hoja moja tu ya umbali. Kwanza, nje ya dunia kisayansi ni kuanzia anga za juu (space), ambako tayari binadamu ameishi kwa mwaka mzima. Pili, nyota na sayari ni vitu viwili tofauti. Binadamu ana-explore habitable planets na siyo nyota, kwa sasa Mars imepewa priority kwa sababu ya ukaribu na tabia zake (Mars inafikika kwa miezi kadhaa tu).Hoja ya umbali ni sawa, lakini hujaweka angalizo la teknolojia mpya. Kuna uwezekano ikagunduliwa teknolojia ya kusafiri angalau fraction ya speed ya light. So, si suala la "hatoweza" ni suala la lini ataweza.
Kuna mdau hapo juu nimemdadavulia kuhusu Mars Planet, ina kisiwa kuwa NASA watapeleka binadamu kwenye sayari ya Mars ifikapo 2030.Ili Mars aweze kuishi binadamu,ni lazima kwanza ipandwe miti kwa wingi ili kutengeneza hewa ya oxgeny,lakini kabla ya hapo kutahitajika operation maalumu ya kwenda kuchimba visima kwa kuwa juu ya uso wa Mars maji hayatembei. Kumbuka haya yote yatakuwa yanafanyika kwa gharama ya trilions of dollars na kila hatua inakisiwa kufikiwa kila baada ya miaka 50+ na inakisiwa kuwa kuna hatua zipatazo si chini ya 7.
 
Je yule jamaa aliyeishi miaka mamilioni iliyopita pale Oldvai Gorge angeweza kuamini kuwa leo watu wangeweza kwenda Chato kwa kupitia Chato Airport juu kwa juu?Achana kabisa na kitu vinaitwa Brain.Magufuli ameshasema tuache kulemalemaa na kujiliza huku tukiwa tumepakata silaha.Wewe umepewa mamilioni ya cells za ubongo na bado unalialia maana yake nini?
 
Kwa kifupi Mars kwenda binadamu inawezekana,lakini kuwafanya binadamu yakawe makazi yao ndipo ulipo ugumu hasa kwenye swala la rasilimali fedha,kwani mataifa mengi kwa sasa hilo sio ktk vipaumbele vyao. Lakini tukiamua kwenda kudili na hawa viumbe wa ajabu wanaotembea kutoka Dar to New York kwa kufumba na kufumbua, hili swala linalochelewesha (pesa) kwenda huko na kwingine Ulimwenguni lisingekuwepo.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
The way technological advance zinavyokwenda mwendokasi,never say never
 
Je yule jamaa aliyeishi miaka mamilioni iliyopita pale Oldvai Gorge angeweza kuamini kuwa leo watu wangeweza kwenda Chato kwa kupitia Chato Airport juu kwa juu?Achana kabisa na kitu vinaitwa Brain.Magufuli ameshasema tuache kulemalemaa na kujiliza huku tukiwa tumepakata silaha.Wewe umepewa mamilioni ya cells za ubongo na bado unalialia maana yake nini?
Ni kweli brain ndio kila kitu na ndio iliyoniongoza mimi kuandika uzi huu,na hata hilo ninaloliona ni matumizi mazuri sana ya brain yangu. Kwanini tunaendelea kusumbuka na vitu vyenye njia za mkato ......... Na lengo sio kuwa tumia vibaya.
 
hii ni sayansi vitu vinaenda kitafiti na kimajaribio, ww unasema haitowezekana kwa sababu ya distance kwa nini umekuja kwenye hitimisho la namna hiyo?.
 
The way technological advance zinavyokwenda mwendokasi,never say never
Technology inayozungumziwa hapa ni ya kuzidi mwendo wa mwanga ambao ni 299,792,458 mitre/per sec.Kinyume cha hapo ni kuendelea na hii ya kutumia miezi 6 - 8 kwenda Mars ambayo binadamu atapelekwa 2030.
 
hii ni sayansi vitu vinaenda kitafiti na kimajaribio, ww unasema haitowezekana kwa sababu ya distance kwa nini umekuja kwenye hitimisho la namna hiyo?.
Hizo tafiti na majaribio ndio vimenifanya niseme hivyo.
 
Mtoa mada una kitu ambacho ulilenga kukisema bahati mbaya umeshindwa kukiwakilisha vizuri nadhani ulichoandika ni issue ya kufikirika zaidi na uelewa wako umekuwa tofauti kidogo na ulichokusudia maana nje ya dunia sio kwenye nyota.
 
Kuna mdau hapo juu nimemdadavulia kuhusu Mars Planet, ina kisiwa kuwa NASA watapeleka binadamu kwenye sayari ya Mars ifikapo 2030.Ili Mars aweze kuishi binadamu,ni lazima kwanza ipandwe miti kwa wingi ili kutengeneza hewa ya oxgeny,lakini kabla ya hapo kutahitajika operation maalumu ya kwenda kuchimba visima kwa kuwa juu ya uso wa Mars maji hayatembei. Kumbuka haya yote yatakuwa yanafanyika kwa gharama ya trilions of dollars na kila hatua inakisiwa kufikiwa kila baada ya miaka 50+ na inakisiwa kuwa kuna hatua zipatazo si chini ya 7.

Nadhani unafikiria upande mmoja tu
1: sio kweli kuwa Mars yote imefanyiwa exploration ili kuona kama kuna maji au hakuna, ni sehemu ndogo tu ndio imefanyiwa huo utafiti kwa sababu chombo kilichotumwa huko (Rovers) kimefikia eneo moja na Mars ni kubwa tu, so conclusion ya kusema Mars hakuna maji na kunahitajika visima vingi ili mwanadamu aishi nayo haina msingi, kuna uhakika gani kuwa kuna underground water kule?

2: kwa nini ipandwe miti ndio binadamu aishi?, hakuna uwezekano wa Binadamu kuwa genetically modified ili waweze kuishi hayo maeneo?, hapa Duniani kuna watu wanaishi kwenye joto kali sana na wengine kwenye baridi kali sana, wengine jangwani, wengine kwenye misitu minene sana

3: Kama unasema hakuna oxygen kwenye Mars, hiyo miti itaotaje? Maana lazima ipate maji, ambayo ni combination ya hydrogen na oxygen (H2O)
 
Technology inayozungumziwa hapa ni ya kuzidi mwendo wa mwanga ambao ni 299,792,458 mitre/per sec.Kinyume cha hapo ni kuendelea na hii ya kutumia miezi 6 - 8 kwenda Mars ambayo binadamu atapelekwa 2030.
what makes you think,that in the future,Technology will not catch up with the speed of light? Usisahau many things we take for granted today were deemed impossible then
 
Nadhani unafikiria upande mmoja tu
1: sio kweli kuwa Mars yote imefanyiwa exploration ili kuona kama kuna maji au hakuna, ni sehemu ndogo tu ndio imefanyiwa huo utafiti kwa sababu chombo kilichotumwa huko (Rovers) kimefikia eneo moja na Mars ni kubwa tu, so conclusion ya kusema Mars hakuna maji na kunahitajika visima vingi ili mwanadamu aishi nayo haina msingi, kuna uhakika gani kuwa kuna underground water kule?

2: kwa nini ipandwe miti ndio binadamu aishi?, hakuna uwezekano wa Binadamu kuwa genetically modified ili waweze kuishi hayo maeneo?, hapa Duniani kuna watu wanaishi kwenye joto kali sana na wengine kwenye baridi kali sana, wengine jangwani, wengine kwenye misitu minene sana

3: Kama unasema hakuna oxygen kwenye Mars, hiyo miti itaotaje? Maana lazima ipate maji, ambayo ni combination ya hydrogen na oxygen (H2O)
#3. Karudie kusoma tena,nimesema kabla ya kupanda miti ni lazima kuchimbwe visima ili ipatikane oxygen. Lakini kwa hali ya hewa ya sasa haiwezekani kwa binadamu kuishi.

Kimsingi mimi sijashawishika kama ipo siku binadamu wataweza kuishi Mars.Jaribu kupitia majibu yangu niliyotoa hapo juu.

Na ndio maana naona ndani ya solar system ( japo nimesema nje ya dunia) yetu hakutapatikana maisha,labda nje ya solar system na kwenyewe ndio kumenifanya niweke hii hoja hapa ili nyinyi mniambie kwanini tusitumie hawa viumbe wanaotembe kwa speed ya kufumba na kufumbua ??
 
Nachokupinga ni kusema hakuna maji Mars wakati utafiti umefanywa kipande kidogo tu? Je Sayari yote imeshakuwa explored?
 
Back
Top Bottom