Billionaire Samweli Lema wa Arusha Ndani ya Segerea

ukiona hivyo ujue Lema kahusika kwenye wizi...Mohamed amefanya biashara na watu wengi kwa nini akamatwe lema peke yake? Walikuwa washirika kwenye wizi
 
Wabongo bwana mnamuhukumu mtu mtathani nyie ndio mahakimu hamjajua hata anatuhumiwa kwa kosa gani au anamashtaka mangapi mnashangilia sana kuona tajiri anapelekwa rumande au afilisiwe awe maskini kamanyie au aishi kama shetani mhaa watz nomaaa sana full majungu na roho mbaya
 
Ingekuwa inafaa ningekuongeza like ya tano mkuu
 
ukiona hivyo ujue Lema kahusika kwenye wizi...Mohamed amefanya biashara na watu wengi kwa nini akamatwe lema peke yake? Walikuwa washirika kwenye wizi

Sikatai lakini kama ungejua hata kwa 2% nilichokueleza basi usinge andika ulichoandika unless unapenda kubishana wakati msingi wa hoja either huna au hujui unachosema.Labda nikusaidie kiduchu wakati wa kuwasilisha online VAT return kila mwezi kuna mambo yafuatayo utataikiwa kufanya

VAT output.
a. mauzo yanayotozwa VAT
b.mauzo yanayotozwa kiwango sifuri
c.mauzo yaliyo samehewa kodi

VAT inputs
a.Manunuzi ya hapa nchini yanayotozwa VAT
b.Manunuzi ya nje yanayotozwa VAT
c.Manunuzi ya nje yanayostahili marejesho ya VAT
d.Marejesho ya VAT ya mwezi uliopita

Ukimaliza section hiyo unakwenda kwenye sheet ambayo utaingiza VRN za wateja wote walikuuzia bidhaa au kukupatia huduma.Ukiingiza VRN automatic inakuletea jina la likuuzia bidhaa au kukupatia huduma automatic sasa kama ni magumashi system itakugomea kabisa.Kitu cha kushangaza VRN ilikuwa inaleta jina kama kawaida kwahiyo kama ni kosa basi lilitakiwa kuangaliwa kuanzia BRELA na TRA.

Natumaini kama ulikuwa unataka kuelewa basi utakuwa umeelewa na siku nyingine utakuwa mdadisi mzuri si kukubali kila kitu unachoambiwa kabla haujafanya uchunguzi wako mwenyewe na kuridhika.
 
Kama jamaa Shule ni ndogo ni vizuri aka ajira director ambaye anauelewa ambaye anaweza ku question vitendo vya muhasibu. Kwa sababu kwa hali ya sasa Kama ame sign mahesabu yake ya mwaka pamoja na muhasibu wake, hivyo yeye amekubali kwamba mahesabu yapo sawa .
 
Watu wa Arusha kwa kupenda kujiita mabilionea heri wa dar wanakula mahindi na chumvi na kikao na kuendesha passo
 

Finance Manager wa NEWL Mr Migire ni CPA (T) & MBA bado kuna Chief Accountant ni CPA bado senior acct bado kuna ACC payable,Acc Recevable & cost.ukinda vitengo vingine Procurement,Transport & Technical wapo wasomi kibao kuanzia wazungu,wahindi hadi wachina.

Kama ni kuwatumia wasomi jamaa kawajaza kweli kweli.
 
Hakuna ufisadi uliofanywa na CCM mkuu. Ulifanywa na watu wakiwa ndani ya CCM na wengine wengi wako upinzani sasa. Weka mambo sawa usipotoshe watu.
Yumo ndani ya ile kesi, ni ktk msako wa wale wote walioshiriki ktk mchezo ule
 
Mkuu uko deep sana inaoneka wewe ni insider au una strong ties na jamaa in good will.
 
Sasa wewe hapa unatetea bila kufanya uchunguzi wa kutosha ambao unataka ufanyike. Kama issue iko kama ulivyoelezea basi atapata haki yake. Ndio maana mpaka sasa tukasema anaitwa mtuhumiwa. BTW mimi nina uzoefu na wafanyabiashara wengi wa Tanzania, wakubwa kwa wadogo. Wafanyabiashara utakaowakuta yuko clean kwenye shughuli zao ni wa kuhesabu, au niseme sijui kama wapo! Hii inatokana na hali halisi ya mazingira ya biashara ya nchi yetu! Ukitaka kila kitu kiwe halali hutafanikiwa kwenye biashara yako. Kwa mfano watu wengi wanaomiliki kampuni za ujenzi kama huyu bwana ni kuhonga ili uapate tenda serikalini ni kama sheria. Na ukija kwenye mambo ya kodi tena ukiamua kufanya kila kitu clean basi utaumia...
 

Mkuu macho_mdiliko sitetei naeleza mambo jinsi ninavyoyajua.Utakuja kushangaa Jamhuri inashindwa kesi nyingi si kwamba mawakili wa serekali ni wazembe au wanashirikiana na watuhumiwa lahasha unakuta msingi wa kesi tangu mwanzo umejikita katika siasa badala ya sheria.
 
Mkuu uko deep sana inaoneka wewe ni insider au ma strong ties na jamaa in good will.

Mkuu Matola nimefanya biashara na NEWL muda mrefu nawajua wafanyakazi wake wengi hata hichi nilichoandika ni kwasababu ya huo uhusiano baada ya malipo yangu kukwama kwasababu ya kukosa saini ya mkurugenzi.Nimezungumza na wataalamu wake kuanzia procurement na Accountant wake.
 
Umemaliza mkuu, shinikizo haswa na kupenda sifa na kufedhehesha watu kunakofanywa na serikali ndio kumemfikisha Lema hapo.
 
Anaye sign financial accounts as director ni nani? Yeye mwenyewe au hao ma expert.?
Kwenye ku sign financial statement ni Watu wawili director wa kampuni na chief accountant. Sasa ikiwa yeye na chief accountant wali sign it means na yeye Ana husika . Jingine ni responsibility ya mngt kuweka a good accounting system and control , sasa ikiwa yeye anaji involve na vitu asivyokuwa na knowledge navyo ni shida, ikiwa ni ma expert waliofanya hizo kazi/shughuli basi anaweza kujitetea kwa kuwasukumia wahusika hayo matatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…